Mbona kelele zinazidi kuna shida gani!?

Mbona kelele zinazidi kuna shida gani!?

The Phylosopher

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2015
Posts
1,968
Reaction score
2,957
Nimekaa na kutafakari sana bila majibu, hasa kuhusiana na namna malalamiko yanazidi kuongezeka mitandaoni.

Ukiyasikiliza kwa makini hayo malalamiko lazima yakuchanganye. Wapo wanaoona Hali ni shwari na wanaona tunaelekea kuzuri.

Wengine wanaona tumepotea na tunazidi kupotea hivyo tunahitaji mwokozi haraka iwezekanavyo.

Kutofautiana kwa wanadamu wenye akili timamu ni jambo la kawaida, ila kinachonishtua kwa sasa huu mvurugano uko miongoni mwa makada wa vyama vyote vya siasa.

Wako CCM lakini pia wako wapinzani wanaofurahia na kuchekelea utawala huu lakini pia wako wasioridhika kabisa.

Ndipo likanijia swali:
Tatizo letu la msingi ni lipi!?
 
Tatizo letu kubwa siku zote ni nchi kuongozwa na maono ya mtu mmoja zaidi kuliko taasisi zilizosimikwa kwenye Katiba bora.Kelele hazitaacha kuwa nyingi bila katiba mpya inayojisimamia yenyewe zaidi.
 
Kwanza natanguliza samahani kwa wanabeijing wote…tunawapenda sana mmetuzaa na kutulea mpaka tunaitwa watu wazima mchango wenu ni mkubwa sana kwa kweli…mtazamo wangu ni huu naomba kusema hivi…

Wamama naomba wabaki kuwa wasaidizi na wababa waendelee kuwa vichwa..hii ni principal tangia uumbaji..huu ni ukweli mchungu samahani sana jamani kwa wale nitakao wakwaza

Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote
 
Tatizo kubwa ni mfumo unaotumika kiutawala hauendani na kuzazi cha sasa kwenye kupanga na kupata maendeleo imala na ya kudumu katika nchi yetu.

Kuna watu wachache wa kizazi kile wanapambana kucha kutwa na kujiaminisha kwamba katiba iliyopo ni bora na itawawalinda kwenye machafu yao.
Na wanajua siku ikipatikana katiba mpya kuna hatari ya vijana hawa kukabidhiwa nchi.
Na huko ndo kuna machafu ambayo kizazi kile wanajalibu kuyafunika.

Vyombo vya usalama na wazee wachache ndio wanao ng'ang'ana na mambo haya.
Lakini naamini m1 m1 wataondoka na katiba itatengenezwa na vijana wataingia ikuru.
Wanachofanya hawa wazee ni sawa na kunyea kitandani halafu wanaambiwa watoke watu wasafishe chumba wao wanaona aibu.

Wanatakiwa waondoe aibu zao chumba kisafishwe na kipangwe upya.
Hapo ndio tutapata maendeleo angalau kwa asilimia 40 mwendo wa maendeleo utaongezeka.
 
Sikh mia za mwanzo nilimuelewa sana na alikuwa anaeleweka bila utata.
Baada ya hapo nadhani alipata washauri nje ya wale Siku 100.
Wanamharibia kikwelikweli.
 
Mkuu kuna upande mmoja wapo ng’ambo hii ya mto yenye rutuba na wengine wako ng'ambo ile ya mto yenye mawe na michanga na daraja limevunjwa.Sasa kama vilio ni vingi basi jua walioko jangwani ndiyo wengi zaidi na wanapaza sauti ili nao wavuke mto.
 
Kwanza natanguliza samahani kwa wanabeijing wote…tunawapenda sana mmetuzaa na kutulea mpaka tunaitwa watu wazima mchango wenu ni mkubwa sana kwa kweli…mtazamo wangu ni huu naomba kusema hivi…

Wamama naomba wabaki kuwa wasaidizi na wababa waendelee kuwa vichwa..hii ni principal tangia uumbaji..huu ni ukweli mchungu samahani sana jamani kwa wale nitakao wakwaza

Mungu ibariki Tanzania na watu wake wote
Malkia was Uingereza, angel markle ni wanaume??
 
Nimekaa na kutafakari sana bila majibu, hasa kuhusiana na namna malalamiko yanazidi kuongezeka mitandaoni.

Ukiyasikiliza kwa makini hayo malalamiko lazima yakuchanganye. Wapo wanaoona Hali ni shwari na wanaona tunaelekea kuzuri.

Wengine wanaona tumepotea na tunazidi kupotea hivyo tunahitaji mwokozi haraka iwezekanavyo.
Kutofautiana kwa wanadamu wenye akili timamu ni jambo la kawaida, ila kinachonishtua kwa sasa huu mvurugano uko miongoni mwa makada wa vyama vyote vya siasa.
Wako ccm lakini pia wako wapinzani wanaofurahia na kuchekelea utawala huu lakini pia wako wasioridhika kabisa.
Ndipo likanijia swali:
Tatizo letu la msingi ni lipi!?
Wewe ndio unapiga kelele ulizoea maisha ya kutuibia na kulamba viatu magufuli na viongozi wake.

Sisi watanzania tumetulia tulii. Sana sana tunawashauri viongozi wasiturudishe misri.
 
Sikh mia za mwanzo nilimuelewa sana na alikuwa anaeleweka bila utata.
Baada ya hapo nadhani alipata washauri nje ya wale Siku 100.
Wanamharibia kikwelikweli.
Ni kweli. Walimtisha. Wakamwambia asijifanye kuwa mwema kwa Watanzania..Naye akadanganyika.
 
Tatizo kubwa ni mfumo unaotumika kiutawala hauendani na kuzazi cha sasa kwenye kupanga na kupata maendeleo imala na ya kudumu katika nchi yetu.

Kuna watu wachache wa kizazi kile wanapambana kucha kutwa na kujiaminisha kwamba katiba iliyopo ni bora na itawawalinda kwenye machafu yao.
Na wanajua siku ikipatikana katiba mpya kuna hatari ya vijana hawa kukabidhiwa nchi.
Na huko ndo kuna machafu ambayo kizazi kile wanajalibu kuyafunika.

Vyombo vya usalama na wazee wachache ndio wanao ng'ang'ana na mambo haya.
Lakini naamini m1 m1 wataondoka na katiba itatengenezwa na vijana wataingia ikuru.
Wanachofanya hawa wazee ni sawa na kunyea kitandani halafu wanaambiwa watoke watu wasafishe chumba wao wanaona aibu.

Wanatakiwa waondoe aibu zao chumba kisafishwe na kipangwe upya.
Hapo ndio tutapata maendeleo angalau kwa asilimia 40 mwendo wa maendeleo utaongezeka.
Wakiwa tayari kibadilika Taifa litanufaika sana
 
Inategemea uko upande gani wa sarafu. Kuna upande wa wapigaji, na upande wa wasiokuwa wapigaji.
Usahihi zaidi: inategemea wewe ni mpigaji wa upande gani; uliopita au unaoingia au kurejea kilingeni?

Wasiokuwa wapigaji wengi ni watu wastaarabu na wavumilivu; huwa kimya wakishuhudia mtanange kati ya mashetani yanayogombania kuishi kama malaika.
 
Nimekaa na kutafakari sana bila majibu, hasa kuhusiana na namna malalamiko yanazidi kuongezeka mitandaoni.

Ukiyasikiliza kwa makini hayo malalamiko lazima yakuchanganye. Wapo wanaoona Hali ni shwari na wanaona tunaelekea kuzuri.

Wengine wanaona tumepotea na tunazidi kupotea hivyo tunahitaji mwokozi haraka iwezekanavyo.
Kutofautiana kwa wanadamu wenye akili timamu ni jambo la kawaida, ila kinachonishtua kwa sasa huu mvurugano uko miongoni mwa makada wa vyama vyote vya siasa.
Wako ccm lakini pia wako wapinzani wanaofurahia na kuchekelea utawala huu lakini pia wako wasioridhika kabisa.
Ndipo likanijia swali:
Tatizo letu la msingi ni lipi!?
Wewe ndio tatizo kwa kuwa umeshindwa kubaini tatizo.
 
Back
Top Bottom