Dan Zwangendaba
JF-Expert Member
- Apr 25, 2014
- 5,814
- 8,118
Kitu gani ambacho hakiendi so far?Mambo tele hayaendi vizuri ni mazuzu tu wanaona hali ni shwari.
Nimekaa na kutafakari sana bila majibu, hasa kuhusiana na namna malalamiko yanazidi kuongezeka mitandaoni.
1. JPM aliacha Elimu bila malipo, je sasa hivi wanalipishwa?
2. JPM kaacha mradi wa umeme, je huo mradi hautekelezwi?
3. JPM kaacha mradi wa SGR, je huo mradi hautekelezwi?
4. JPM aliacha ujenzi wa Dodoma, je ujenzi Dodoma hauendelei?
5. Kuna barabara zilikuwa na makandarasi wakifanya kazi, je ujenzi imesimama?
6. JPM aliendeleza kutoa mikopo kwa wanafunzi, je mikopo haikutoka?
7. JPM aliendeleza miradi ya kukarabati barabara zilizoharibika, je leo kazi hiyo haiendelei?
8. JPM alifufua shirika la Ndege, je ununuzi wa ndege ulisimama? Mbona zile ameongeza na oda ya nyingine 4.
Mbali ya hivyo, huyu mama ameongeza miradi yake kwa muda mfupi kabisa.
1. Kuondoa majengo yote ya tembe katika shule za msingi nchi nzima.
2. Kujenga madarasa yote yanayohitajika Ili kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzaniaa kuondoa kile kinachoitwa "second selection" ya kwenda sekondari.
3. Kununua mitambo ya kuchimba.
4. Ununuzi wa mashine za MRI kwa hospital zote za Taifa, kanda na mikoa nchi nzima.
5. Ujenzi wa vyumba na vifaa vya ICU 72 katika ngazi ya Taifa, mikoa na Halmashauri (baadhi)
6. Ununuzi wa Mashine za X ray 85.
7. Usimikaji wa vinu 44 vya hewa ya Oksijeni.
8. Ununuzi wa magari ya wagonjwa 395 (20 yakiwa ya kisasa zaidi) nchi nzima.
9. Ujenzi wa vituo vinne vya Telemedicine
10. Utekelezaji wa miradi ya maji
11. Mpango wa Bima ya Afya kwa wote (Universal Health Care) ambapo Bilioni 149 zimetolewa.
12. Kifunga mashine za Dialysis kwa hospitali za Rufaa za mikoa 6 ya Tanga, Mtwara, Mara, Arusha, Kagera na Kigoma.
13. Kujenga vyuo vya VETA 32.
14. Kununua mitambo 5 ya kujenga ya mabwawa ya maji.
15. Magari 25 ya kuchimba visima vya maji (ni wastani wa magari 5 kila kanda).
16. Kutengeneza madawati 462000+ Ili watoto wenu wasikae chini.
17. Ajira zimeanza kufunguka (both government and private)
18. Vitanda vya wagonjwa 2700
19. Mitaa yenu leo walau unaanza kuonekana maana kila jiji ilikuwa kama unapita Kibera tu pale Kenya.
20. Msio wafanyabiashara hamuwezi kuelewa namna wenye pesa zao benki walivyokuwa na wasiwasi. Wasiwasi huo sasa haupo.
Sasa tuulizane, huyu mama alipaswa afanye nini zaidi kwa miezi yake hii minane madarakani? Watanzania nna shida gani? Kwanini mnakuwa driven na uzushi uzushi na hisia au deceived na watu kwa maslahi yao?. Tuulizane ni kipi alichokuwa anafanya JPM Samia hafanyi? Kama mnataka ale mahindi njiani au kimetolea kashfa mtu katika halaiki hilo for sure hamtayaona kwa Samia kwasababu sio sehemu ya malezi yake.