Kumkana mtu kwa sababu amepatwa matatizo ni michezo ya kitoto.
1. Unaposema hakuwa mwajiriwa, je nani alikua kocha wa makipa kwa muda wote ambao kblabu imecheza mechi za kitaifa na kimataifa?
2. Unaposema alikua na mkataba wa mwezi mmoja tu, mbona tumemuona kwenye klabu kwa zaidi ya mwezi mmoja? Hiyo miezi mingine alikua anauza Ice cream au?
3. Halafu mbona hamsemi huo mkataba wa mwezi mmoja ulianza lini na kumalizika lini?
4. Na alipomaliza mkataba, klabu ilitoa taarifa yoyote kwa umma?
5. Ni aibu timu kubwa kama Simba kukiri kwamba ilikua na kocha Vodafasta. Ni aibu zaidi kumtangaza kocha mpya wa makipa masaa matatu baada ya Mharami kukamatwa? Kwanini Kocha mpya atangazwe leo na sio jana au juzi?
6. TFF mjitathmini kwa hili. Kazi yenu sio kupanga ratiba ya ligi na kumfungia Manara. Ni kusimamia maendeleo ya soka. Mnaruhusuje klabu inayoshiriki mashindano ya kimataifa kuwa na Kocha wa mwezi mmoja? Hata housegirl hapewi mkataba wa mwezi mmoja siku hizi. Imekuaje kwa Mharami? Mikataba ya wachezaji na makocha inakua reviewed na TFF. Kwahiyo mlireview huu wa mwezi mmoja na mkapitisha?
7. Simba kumkana Muharami kunatoa tafsiri gani kwa Mgunda? Je na yeye akipata matatizo tutamkana kwamba hajawahi kuwa kocha wetu? Au tutasema tulimuazima kwa mkataba wa miezi miwili ambayo ilishaisha?
8. Hakuna dhambi yoyote kukiri kwamba Muharami alikua Kocha wetu wa makipa. Na kukiri hivyo haifanyi makosa yake yawe makosa ya klabu. Muharami amekamatwa katika shughuli zake binafsi, sio shughuli za kblabu. Kwahiyo hata kama tungekubali kwamba alikua kocha wetu, haifanyi tuhuma zake kuwa tuhuma za klabu.
9. Pia viongozi wakumbuke kwamba hizi ni tuhuma tu, ambazo hazijulikani kama ni za kweli au uongo, hadi pale Mahakama itakapothibitisha pasi na shaka (beyond reasonable doubts). Tumekimbilia haraka kujisafisha kana kwamba Muharami ameshakutwa na hatia na amehukumiwa. Je ikiwa mahakama itamwondolea hatia na kusema tuhuma zake si za kweli, tutaambia nini watu?
10. Kujisafisha kwa kumkana Mharami ni kujichafua zaidi. Na kukubali kuwa alikua kocha wetu, hakufanyi tuhuma zake kuwa tuhuma za klabu. Pigia mstari.!