Mbona kila kitu haraka, kuna nini Simba?

Mbona kila kitu haraka, kuna nini Simba?

kilwakivinje

JF-Expert Member
Joined
Jan 4, 2014
Posts
6,184
Reaction score
9,407
Kocha kakanwa kabla jogoo hajawika. Mwingine kateuliwa kabla giza halijaingia, hili linaleta sintofahamu kuhusu hii skenfldo ya madawa ya kulevya. Serikali ichunguze kwa makini sana kuna shida mahala.

Panapofuka moshi tupawahi mapema kabla moto hujawaka kuokoa timu yetu.

Nachukia kuitwa Ngada FC, Yanga mtulie kidogo wakati huu tunapomtafuta huyu nyoka ndani na kusafisha jina letu.
 
Kocha kakanwa kabla jogoo hajawika
Mwingine kateuliwa kabla giza halijaingia, hili linaleta sintofahamu kuhusu hii skenfldo ya madawa ya kulevya. Serikali ichunguze kwa makini sana kuna shida mahala...
Hao wanaojitoa ufahamu wanasahu aliyekua mwenyekiti wao kesi ya mihadarati wanamsahau Yusuph Manji aliyepimwa mkojo
 
Kocha kakanwa kabla jogoo hajawika
Mwingine kateuliwa kabla giza halijaingia, hili linaleta sintofahamu kuhusu hii skenfldo ya madawa ya kulevya. Serikali ichunguze kwa makini sana kuna shida mahala.

Panapofuka moshi tupawahi mapema kabla moto hujawaka kuokoa timu yetu

Nachukia kuitwa ngada fc yanga mtulie kidogo wakati huu tunapomtafuta huyu nyoka ndani na kusafisha jina letu.
Poa poa mwana 🦁fc
 
Hata
usizunguke.taja fulani na fulani wanahusika.
usizunguke.taja fulani na fulani wanahusika.
Mazingira ni yote yanayotuzunguka na hiyo ndio maana ya mazingira, hata ulipo umezungukwa na mazingira. Mazingira iliyopo hivi sasa yanatofautiana na mazingira ya mwingine hivi sasa.
 
Kumkana mtu kwa sababu amepatwa matatizo ni michezo ya kitoto.

1. Unaposema hakuwa mwajiriwa, je nani alikua kocha wa makipa kwa muda wote ambao kblabu imecheza mechi za kitaifa na kimataifa?

2. Unaposema alikua na mkataba wa mwezi mmoja tu, mbona tumemuona kwenye klabu kwa zaidi ya mwezi mmoja? Hiyo miezi mingine alikua anauza Ice cream au?

3. Halafu mbona hamsemi huo mkataba wa mwezi mmoja ulianza lini na kumalizika lini?

4. Na alipomaliza mkataba, klabu ilitoa taarifa yoyote kwa umma?

5. Ni aibu timu kubwa kama Simba kukiri kwamba ilikua na kocha Vodafasta. Ni aibu zaidi kumtangaza kocha mpya wa makipa masaa matatu baada ya Mharami kukamatwa? Kwanini Kocha mpya atangazwe leo na sio jana au juzi?

6. TFF mjitathmini kwa hili. Kazi yenu sio kupanga ratiba ya ligi na kumfungia Manara. Ni kusimamia maendeleo ya soka. Mnaruhusuje klabu inayoshiriki mashindano ya kimataifa kuwa na Kocha wa mwezi mmoja? Hata housegirl hapewi mkataba wa mwezi mmoja siku hizi. Imekuaje kwa Mharami? Mikataba ya wachezaji na makocha inakua reviewed na TFF. Kwahiyo mlireview huu wa mwezi mmoja na mkapitisha?

7. Simba kumkana Muharami kunatoa tafsiri gani kwa Mgunda? Je na yeye akipata matatizo tutamkana kwamba hajawahi kuwa kocha wetu? Au tutasema tulimuazima kwa mkataba wa miezi miwili ambayo ilishaisha?

8. Hakuna dhambi yoyote kukiri kwamba Muharami alikua Kocha wetu wa makipa. Na kukiri hivyo haifanyi makosa yake yawe makosa ya klabu. Muharami amekamatwa katika shughuli zake binafsi, sio shughuli za kblabu. Kwahiyo hata kama tungekubali kwamba alikua kocha wetu, haifanyi tuhuma zake kuwa tuhuma za klabu.

9. Pia viongozi wakumbuke kwamba hizi ni tuhuma tu, ambazo hazijulikani kama ni za kweli au uongo, hadi pale Mahakama itakapothibitisha pasi na shaka (beyond reasonable doubts). Tumekimbilia haraka kujisafisha kana kwamba Muharami ameshakutwa na hatia na amehukumiwa. Je ikiwa mahakama itamwondolea hatia na kusema tuhuma zake si za kweli, tutaambia nini watu?

10. Kujisafisha kwa kumkana Mharami ni kujichafua zaidi. Na kukubali kuwa alikua kocha wetu, hakufanyi tuhuma zake kuwa tuhuma za klabu. Pigia mstari.!
 
Back
Top Bottom