round kick
JF-Expert Member
- Feb 3, 2025
- 345
- 1,145
Trump aliweka kodi asilimia 25 kwa bidhaa zinazotoka Mexico kama adhabu ya wao kutotia mkazo wa uvushaji wa madawa na wahamiaji haramu kuingia Marekani, Rais wa Mexico hakutaka kuonekana mnyonge akamwaga mboga kwa kuweka kodi asilimia 25 kwa bidhaa zinazotoka Marekani (Tit for Tat), Ni siku ya 3 rais wa Mexico pumzi imekata kaomba ligi iishe na kukubali kutuma wanajeshi elf 10 mpakani
Kupitia mtandao wake wa Truth na X(Twitter) Trump ameandika “Nimezungumza na Rais Claudia Sheinbaum wa Mexico. yalikuwa mazungumzo ya kirafiki sana ambapo alikubali mara moja kutuma wanajeshi 10,000 wa Mexico kwenye mpaka unaotenganisha Mexico na Marekani. Wanajeshi hawa watawekwa mahsusi ili kuzuia mtiririko wa fentanyl na wahamiaji haramu kuingia katika nchi yetu."
Trump aemongeza kuwa "Tulikubaliana pia kusitisha mara moja ushuru uliokuwa umepangwa kwa muda wa mwezi mmoja, kipindi ambacho tutakuwa na mazungumzo yatakayoongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje Marco Rubio, Waziri wa Hazina Scott Bessent, na Waziri wa Biashara Howard Lutnick, pamoja na wawakilishi wa ngazi ya juu wa Mexico."