Mbona mikoa mingine haitoi wasanii kwenye tasnia ya burudani?

kinjumbi one

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2015
Posts
1,695
Reaction score
2,144
Habari za weekend
Kuna mawazo yamenijia kichwani na nimeona niwashirikishe wadau. Ktk sekta ya burdani, kuna baadhi ya mikoa hapa tz sijasikia ikitoa mwanamuziki hata mmoja kulikoni?

Kwa mfano, ukiangalia miaka kumi iliyopita, kuanzia mwaka 2005 hadi 2008 naona tanga walifunika kwakua na vijana wanao ng'aa ktk muziki, vijana hao kama, Sumalee, MB dog, matonya, marehem sharo milionea, Na kadhalika, 2008 hadi leo, naona mkoa wa kigoma unaongoza gurudumu.

Ukiwa na vijana wake namba mmoja nchini, Ali kiba na Naseebu Abdul, ktk kipindi chote hicho ipo na mikoa mingine ikitoa msanii mmoja mmoja, au wawili, mfano kama mbeya, kuna akina izzo business, Raymond, na sugu, mkoa kama Arusha kuna akina John makini, na wenzie, mkoa kama mtwara, kuna Pasha, harmonize, nk.

Lakini kuna mikoa sijasikia kabisa ikitoa msanii hata mmoja, mfano kama mkoa wa Rukwa, mkoa kama Manyara, mkoa kama Lindi, mkoa kama singida, Mkoa kama shinyanga, sasa najiuliza, ina maana, ktk watu wote wa huko hakuna kijana hata mmoja mwenye kipaji cha kuweza kutoboa ki taifa?

Au wapo mimi siwajui? Ni nani kwa mfano?
 
Nikweli kunabaadhi ya mikoa enzi bendi zinatamba ndio Mara ya mwisho walitoa wasanii waliotoboa kitaifa btw main stream haiwezi Kuaccommodate wasanii wote wa tz acha wenye visu vikali waendele kutuburudisha
 
Hivi wasanii wanaotokea kigoma ndo wapi hao kina diamond,Alikiba,Abdu kiba,Recho,Banana Zorro,Qeen Darline etc waliozaliwa na kukulia Dar? Mbona km ndo hivyo basi young D atakuwa wa Mbeya.Joh Makin & Nikki 2,Aika,Ney wa mitego Kilimanjaro.Jokate Songea.Darasa Tabora kama ndo hivyo kila mkoa una wasanii km issue ni asili
 
Mkuu anapenda mambo hayo
 
Kuna mikoa haijawahi kutoa maraisi na mawaziri
Ni kwasababu Raisi anahitajika mmoja tu, tena ndani ya miaka 10, ili kufikia ma Raisi wa tano, inahitaji, miaka hamsini. Tofauti na muziki ambapo hata vijana 100 mnaweza kung'ara kwa pamoja. Ajabu sasa pamoja na fursa hiyo, bado kuna baadhi ya mikoa hamna kitu.
 
Hivi wasanii wanaotokea kigoma ndo wapi hao kina diamond,Alikiba,Abdu kiba,Recho,Banana Zorro,Qeen Darline etc waliozaliwa na kukulia Dar? Mbona km ndo hivyo basi young D atakuwa wa Mbeya.Joh Makin & Nikki 2,Aika,Ney wa mitego Kilimanjaro.Jokate Songea.Darasa Tabora kama ndo hivyo kila mkoa una wasanii km issue ni asili
Kwakuchukulia muktadha huo huo, ni yupi wa mkoa wa Rukwa? Ni yupi wa mkoa wa Manyara? Ni yupi wa mkoa wa Singida?
 
Ni kwasababu Raisi anahitajika mmoja tu, tena ndani ya miaka 10, ili kufikia ma Raisi wa tano, inahitaji, miaka hamsini. Tofauti na muziki ambapo hata vijana 100 mnaweza kung'ara kwa pamoja. Ajabu sasa pamoja na fursa hiyo, bado kuna baadhi ya mikoa hamna kitu.
Ona masela wangu sina jambo
 
Jay Moe, Juma nature, Jafaray, TID, KR Mullah, Inspector Haruni, Pasha, Isabela Mpanda hao wote wana asili ya Lindi au Mtwara
 
Hivi wasanii wanaotokea kigoma ndo wapi hao kina diamond,Alikiba,Abdu kiba,Recho,Banana Zorro,Qeen Darline etc waliozaliwa na kukulia Dar? Mbona km ndo hivyo basi young D atakuwa wa Mbeya.Joh Makin & Nikki 2,Aika,Ney wa mitego Kilimanjaro.Jokate Songea.Darasa Tabora kama ndo hivyo kila mkoa una wasanii km issue ni asili
Umenena mkuu
 
Back
Top Bottom