Mbona Mzee wa Komesho(AY) hakumualika Crazy GK kwenye harusi yake?

Mbona Mzee wa Komesho(AY) hakumualika Crazy GK kwenye harusi yake?

b566eddcd9c49e0073c2fc068d47ee22.jpg







Mtoa post unaonekana ww ni mtu usiejulikana
Huyu jamaa kunakitu hakipo sawa
Acheni Uzushi.
 
Hatahivyo uwezo wa GK katika utungaji wa mashairi na uchanaji uko juu sana kwa kulinganisha na hao matoz 2 wanaishi kwa maigizo.
Mkuu kwenye mashairi na kutunga hamna anayenkuta mwana FA,GK na kigugumizi chake hamna kitu,halafu maproducer wachache sana walioweza kumrekodia kutoka na na kigugumizi,P-Funk pekee ndo alikuwa anaweza,ndo maana pfunk alipoyumba kwenye uproducer Gk naye akapotea
 
Ametumia ule msemo wa BE DIFFERENT tusimpangie cha kuvaa kwani suti hana au hajui zinakopatikana? Ni mtu mzma labda kutokana na mishemishe zake aliona angechelewa kufika akaona mwana asiponiona atamaind ngoja nizame ki GK GK tu mbna Fresh
 
Yupo wapi sasa huyo GK? Halafu uwe unapunguza masikhara, maana katika wale vijana kila mtu alikua na style yake na kila mtu alikua anajitungia mashairi ya sehemu yake.
Gwamaka Kalihura a.k.a GK alikua na style yake iliyokua ina ficha na kubalance hali yake ya kigugumizi, pia iliyokua ina akisi mitazamo yake ya kupenda ugomvi na ubabe na matusi mengi. Hata majina aliyojiita yalionyesha ni mtu wa aina gani au aliyependa hali gani au aliyependa kuonekanaje. Ndiyo maa akawa anajiita King Crazy GK, Amiri jeshi mkuu, Bokasa etc

Wakati Ambwene Yessaya (AY) yeye alikua hana muda wa kuonya au kuelimisha au kutisha mtu kwenye mashairi yake, yeye aliamua kuja na mashairi yanayolenga ku burudisha zaidi. Yeye alipokua akitunga mashairi anafikiria zaidi jinsi watu watakavyo kuwa wana swing na party huko club na ndiyo maana aliamua kujiita Mzee wa Commercial.

Khamis Mwinjuma,a.k.a Mwanafalsa baadaye Mwana Fa, yeye alikuja na style ya mashairi ya kufikirisha zaidi, yenye nasaha, elimu, ya hali ya juu ambayo yamefungwa fungwa katika mfumo wa lugha unaohitaji kutuliza akili ili kumuelewa. Mashairi hasa ambayo yanahitaji uelewa katika usanifu wa kiswahili. Na mfumo wa utunzi wa kiswahili uliathiriwa na kuwa shaped na tabia yake ya tangu anakua ya kupenda kusoma na kuandika mashairi (Malenga).
Hawa vijana kila mmoja alikua na wapenzi wake ingawa Mwana Fa ndiye alikua na maneno yaliyokaa vichwani mwa watu wa Marika yote ingawa siku zote ilikua ngumu kuimba au kuyakarili mashairi yake zaidi ya kuyafurahia aimbapo alikua na misamiati iliyoishi kwa muda mrefu vichwani mwavwatu na ndani ya jamik.
Unaposema GK ndiye alikua na uwezo mkubwa kuliko wengine wote katika lile kundi lao, unakia umenionyesha wewe ni mtu wa aina gani, yaani ni mtu wa kubutua butua, piga mitama, ng"ado kwa ng'ado, mtaa kwa mtaa, utawachinja kama bokasa, amiri jeshi mkuu umesha lianzisha....yaani mtu wa hivyo
mkuu unajua sana kuwasoma watu
 
Ile East Coast ilijulikana kuwa ni ya watoto wa Upanga. GK akawazunguka wenzake, yeye na demu wake wakasajiri kampuni (East Coast Team) na wao wakawa ndiyo wamiliki huku wenzao wakiwa vibarua. Baadaye jamaa ndiyo wakazinduka usingizini na kujitenga naye mazima.
Sasa huo Ni ufala au ueled, mtu had kusajili kampun unamwita fala
Chuki hazna maana hiz
 
Back
Top Bottom