Mbona Olympics kimya sana, Ushiriki wetu ukoje kwenye jukwaa kubwa la kidunia ?

Mbona Olympics kimya sana, Ushiriki wetu ukoje kwenye jukwaa kubwa la kidunia ?

Yoda

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2018
Posts
48,475
Reaction score
70,102
Kuanzia wiki hii hadi katikati ya mwezi wa nane kuna mashindano makubwa sana ya Olympics yanayoendelea huko Paris, Olympics ni mashindano makubwa zaidi baada ya kombe la dunia.

Mashindano ya nwaka ya Olympics yana thamani ya karibia dola bilioni 10 za Kimarekani, haya ndio mashindano yanayokutanisha nchi nyingi zaidi duniani.

Jambo la kushangaza hakuna hamasa kutoka katika mamlaka kwa ushiriki wetu ukilinganisha na mashindano madogo ya football kama ya AFCON na CAF champions league.

Kama tulikuwa tunataka kutangaza nchi na utalii wake hili ndio lingekuwa jukwaa kubwa zaidi kuwekeza nguvu huko kwa kuhakikisha ushiriki wetu unakuwa mkubwa sana, Olympics pia ina pesa na faida nyingi sana hata kwa mchezaji mmoja mmoja kuliko AFCON.
20240727_115501.jpg
20240727_115515.jpg
 
Tunahitaji ushiriki wa nguvu Olympics
 
Back
Top Bottom