Mbona sioni ulinzi wa kutisha kwa viongozi wakubwa wa Kenya?

Mystery

JF-Expert Member
Joined
Mar 8, 2012
Posts
15,843
Reaction score
31,057
Nimekuwa nikifuatilia kwa Karibu Sana, kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa Kenya, sijaona msururu wa walinzi wa viongozi hao, wakilindwa na ulinzi wa kuwalinda viongozi hao, pamoja na uhasama mkubwa, uliokuwepo huko Kenya, Katika kipindi chote cha uchaguzi huo.

Muda huu naangalia TV za Kenya, zikimuonyesha Rais mteule wa Kenya, William Ruto, akitoa hotuba yake, bila kulindwa na mlinzi yoyote!

Hali ni tofauti Sana hapa kwetu Tanzania, kwa kuwa Kila tunapowaona viongozi waandamizi wanapofanya shughuli za kisiasa, wakilindwa na walinzi wengi mno, na hata na bunduki za moto!

Hilo nalo linaweza likawa linaongeza gharama za uendeshaji wa nchi yetu na hivyo kuona msururu wa tozo tunazokamuliwa sisi watanzania 🥺
 
Viongozi wanaoingia madarakani kihalali huwa hawahitaji ulinzi usiobeba uhalisia. Ukiona viongozi wanajiwekea ulinzi usio wa kawaida, jua wako madarakani kwa shuruti.
 
Hata Mimi naamini, bila wasiwasi wowote kuwa Hawa viongozi wetu tulionao hapa nchini, wanajihami Sana, kwa kuwa siyo chaguo la watanzania!
 
Ulinzi wa Tanzania sometimes unashangaza. Sio presidential guards pekee, hata vikosi vingine kuna mambo ya kuibua hisia ila tukisema hapa watakuja wazalendo uchwara wapinge.

Utashangaa kwenye maonyesho ya uhuru komando wa JWTZ amebeba mizigo kibao kama gunia, mojawapo ya mizigo hiyo ni sufuria la kupikia. Karne ya 21 unabeba viazi field badala ya kubeba MREs? Lile tukio ni la 2020 kama sikosei.
Bado kuna maonyesho ya kupinga ngumi tofali na kupigwa mijeledi mgongoni, hata uwe na jeshi zima linalopiga ngumi chuma na kupigwa nguzo za umeme mgongoni haliwezi ongeza ulinzi kwa uwezo huo.

Yule Hamza pale Salender alifyatuliwa risasi nyingi na kukoswakoswa wakati alikuwa sehemu wazi. Maaskari waliotumika ni hawa wakamata wezi na tukio lilidumu dakika nyingi kabla hawajarespond sasa sijui kama tuna dedicated counter terrorism ya kupambana na magaidi wenyewe.

Tuna woga na amani ya asili, ila kusema tuna ulinzi imara huwa nakataa
 
Kuna vitu viwili ambavyo inabidi tuvitofatishe. Ulinzi wa kishamba vs ulinzi wa kitaalam. Hapa kwetu kuna ulinzi wa kishamba au kilimbukeni au wa kizamani. Ulinzi wa walinzi kusambaa kila mahali na bunduki kama wako tayari kuua mtu muda wowote.
Bongo mtu analindwa kama nyumba 😂😂😂 au gari! Wenzetu wanalinda kwa intelijensia
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa Karibu Sana, kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa Kenya, sijaona msururu wa walinzi wa viongozi hao...
Tanzania viongozi huiba Uchaguzi ndo maana hawajiamini.Hujui bila vitisho watauwawa. Uzuri siku Mungu husimama na raia. Rais Magufuli.
 
Umesema kweli,siku tukivamiwa hapa tutajijua hatujui tutachakazwa kama watoto
Nyerere ndiye alikuwa mnunuaji wa silaha na mzingatiaji wa ulinzi, alikuwa muangalifu kipindi kile vita za Afrika zilikuwa nyingi. Tunazo silaha zilizonunuliwa na Nyerere nyingi mno kama vifaru na artillery. Na kushiriki vita nyingi kama Angola na Msumbiji kulitupatia uzoefu na training ground kwa wanajeshi na maofisa.
Hata usalama wa taifa ya Nyerere ilikuwa exceptional, wakati ule maadui wakubwa kama kama Bureau of State Security (BOSS) ya South Africa kwa mabeberu, pamoja na ukomavu wake na uwezo wake kimataifa tulienda nayo sambamba na kutengua hujuma zao. Leo hii tuna hawa baadhi yao ukiwagusa bar wanakutisha 'unajua mimi nani?'.

Tanzania ya sasa haina changamoto kiulinzi na nchi isiyo na changamoto ni ngumu kushawishi wanasiasa kujipanga. Hata Niger walikuwa hivihivi ila magaidi walivyoshika kasi na kusumbua ikafanya transformation ya haraka pamoja na umaskini wake uliokithiri. Leo hii magaidi unawasikia Nigeria na utajiri wote ila Niger wanapambana nao.
 
Nimekuwa nikifuatilia kwa Karibu Sana, kipindi chote cha uchaguzi mkuu wa Kenya, sijaona msururu wa walinzi wa viongozi hao, wakilindwa na ulinzi wa kuwalinda viongozi hao, pamoja na uhasama mkubwa, uliokuwepo huko Kenya, Katika kipindi chote cha uchaguzi huo.

Muda huu naangalia TV za Kenya, zikimuonyesha Rais mteule wa Kenya, William Ruto, akitoa hotuba yake, bila kulindwa na mlinzi yoyote!

Hali ni tofauti Sana hapa kwetu Tanzania, kwa kuwa Kila tunapowaona viongozi waandamizi wanapofanya shughuli za kisiasa, wakilindwa na walinzi wengi mno, na hata na bunduki za moto!

Hilo nalo linaweza likawa linaongeza gharama za uendeshaji wa nchi yetu na hivyo kuona msururu wa tozo tunazokamuliwa sisi watanzania [emoji3064]
Wanamuiga super power usa

Sent from my SM-J250F using JamiiForums mobile app
 
Nyerere ndiye alikuwa mnunuaji wa silaha na mzingatiaji wa ulinzi, alikuwa muangalifu kipindi kile vita za Afrika zilikuwa nyingi. Tunazo silaha zilizonunuliwa na Nyerere nyingi mno kama vifaru na artillery. Na kushiriki vita nyingi kama Angola na Msumbiji kulitupatia uzoefu na training ground kwa wanajeshi na maofisa.
Hata usalama wa taifa ya Nyerere ilikuwa exceptional, wakati ule maadui wakubwa kama kama Bureau of State Security (BOSS) ya South Africa kwa mabeberu, pamoja na ukomavu wake na uwezo wake kimataifa tulienda nayo sambamba na kutengua hujuma zao. Leo hii tuna hawa baadhi yao ukiwagusa bar wanakutisha 'unajua mimi nani?'.

Tanzania ya sasa haina changamoto kiulinzi na nchi isiyo na changamoto ni ngumu kushawishi wanasiasa kujipanga. Hata Niger walikuwa hivihivi ila magaidi walivyoshika kasi na kusumbua ikafanya transformation ya haraka pamoja na umaskini wake uliokithiri. Leo hii magaidi unawasikia Nigeria na utajiri wote ila Niger wanapambana nao.
Yes TISS ya awamu ya kwanza ilikua super na elewa msafara wa Rais ulikua na gari 3 tu,ukiachilia mwongoza msafara mwenye pikipiki, na kipindi hicho ni viongozi 4 tu waliokua na blue lights leo hii hadi jaji, speaker, igp,cdf etc etc eti nao wanatumia blue lights, it's craze, President Khama wa Botswana muda mwingi alikuwa anasafiri kwa kutumia pikipiki!
 
Viongozi wanaoingia madarakani kihalali huwa hawahitaji ulinzi usiobeba uhalisia. Ukiona viongozi wanajiwekea ulinzi usio wa kawaida, jua wako madarakani kwa shuruti.
Hawa watawala wetu wanaojilimbikizia ulinzi, wanajihami kwa sababu ni wezi wa kura🥺
 
Kuna vitu viwili ambavyo inabidi tuvitofatishe. Ulinzi wa kishamba vs ulinzi wa kitaalam. Hapa kwetu kuna ulinzi wa kishamba au kilimbukeni au wa kizamani. Ulinzi wa walinzi kusambaa kila mahali na bunduki kama wako tayari kuua mtu muda wowote.
Ushamba ni kubeba bunduki hadharani ?
 
Ushamba ni kubeba bunduki hadharani ?

Wakati flani CS Matiangi alilazimika kutoa breakdown ya Walinzi wa Naibu wa Rais Ruto. Idadi ilikuwa zaidi ya 200. Nimesoma mahali Matiangi katimkia Ausralia.
 
Back
Top Bottom