Mbona Stori ya Tanzania kupewa Bilioni 2.6 na Marekani imeripotiwa sana. Kuna nini?

Mbona Stori ya Tanzania kupewa Bilioni 2.6 na Marekani imeripotiwa sana. Kuna nini?

Ukiachana na hizo TZS 2.6b za Ebola, kuna mkataba wa TZS 8 trillion wa afya waliupitisha majuzi.

Serikali inasema haitotoa taarifa za kiafya za watu. Nchi nyingine ziligoma kutoa taarifa zikanyimwa pesa, Tanzania ina nini?

Pia wanasema mkataba huo utaifanya Tanzania iweze kutengeneza yenyewe 80% ya dawa inazohitaji ifikapo 2030.

Watu wengi huko mitandaoni wanasema hii misaada itaokoa maisha ya wengi bila kujali viashiria vya hatari.
Ghana walikataa kwakuwa taarifa za watu zitakuwa wazi..

Yaani mifumo ya tehama wanaifunga wao US, wanakuwa na access ya mifumo yetu ya Afya..

Siku ukienda US Embassy kuomba Visa, ukitaja jina lako tuu..wanajua mwaka Jana ulilazwa Mwananyamala kwa shida hii....au ulikuwa Mkoa flani Tarehe flani ukaenda Hospital ya Mkoa huo kwa shida flani ...

Taarifa wanakuwa nazo..labda uwe unatibiwa private, au dawa za asili
 
Kwenye bajeti 1 trillion ni kwa ajili ya safari za viongozi wa Serikali. Daah hii nchi bhana wanaotuongoza inabidi wajitafakari sana
 
hela ndogo 2.6B 😂😂😂 ila vijana wa Jamii Forum bana.

unadharau 2.6B!??


fedha za kuchukua tahadhari tu hizo na pia mlidai mahusiano yetu yamevurugika imekuaje tena
Walitaka kuiangusha dola ya Tanzania ambayo ina miaka 65 ya uhai juu ya uso wa dunia.

Wakataka Trump aivamie nchi yetu aondoke na Samia, wanasahau nyuma ya huyo Mama nguvu kubwa kiasi gani ipo.
 
Juzi tu hapa, zilikua zinapigwa kelele kwamba, wapinzani wanampango wa kuleta Ebola, alafu leo tunapokea pesa za msaada wa Ebola... Siasa ni hatari sana...


Cc: Mahondaw
 
Hiyo pesa tungewaomba wale jamaa wa Katoro wasingetunyima.
Juzi tu hapa, zilikua zinapigwa kelele kwamba, wapinzani wanampango wa kuleta Ebola, alafu leo tunapokea pesa za msaada wa Ebola... Siasa ni hatari sana...


Cc: Mahondaw
Walitaka kuiangusha dola ya Tanzania ambayo ina miaka 65 ya uhai juu ya uso wa dunia.

Wakataka Trump aivamie nchi yetu aondoke na Samia, wanasahau nyuma ya huyo Mama nguvu kubwa kiasi gani ipo.
Habari Mbaya sana kwa Vibaraka maana mlikua mnasema Uhusiano wa Tanzania na Marekani umeisha kumbe unazidi kuimarika. Ni pigo kubwa sana kwenu Poleeni Sana.
 
Habari Mbaya sana kwa Vibaraka maana mlikua mnasema Uhusiano wa Tanzania na Marekani umeisha kumbe unazidi kuimarika. Ni pigo kubwa sana kwenu Poleeni Sana.
Pigo kubwa kwao hao waliotegemea kumuona Trump akiivamia Tanzania kisha akamchukua SSH.

Adui wa Tanzania ni ujinga unaoishi vichwani mwa watanzania bila kulipa kodi yoyote, mtu asiyependa cha kwake ni rahisi sana kumtawala.

Nakumbuka namna wazungu walivyokuwa wakitucheka kwa jinsi tulivyoshambulia kurasa za Aston Villa baada ya Mbwana Samatta kununuliwa na timu ile, ujinga ule ndio huu wa kutaka kuiona Tanzania inaumizwa kimataifa.
 
Back
Top Bottom