Mbona ujenzi barabara Makongo juu wasua sua sana! JASCO shida nini!

gango2

JF-Expert Member
Joined
Aug 31, 2011
Posts
1,956
Reaction score
2,274
Takribani miezi 4 sasa imeisha toka ujenzi wa barabara hii ya makongo juu kuzinguliwa (November 1) lakini ujenzi wake umezidi kusua sua kiasi kwamba unatia mashaka kama kweli mradi huu upo au ni danganya toto.

Miezi 4 sasa hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika na hata hii kampuni ya JASCO Constructions inatutia mashaka katika hili. Kumekuwa na sintofahamu sana kwani utendaji wao wa kazi kwa kiasi fulani unaleta sana usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii: haya ni maendeleo ya ujenzi

NOVEMBER 1: Ujenzi kuzinduliwa na mkuu wa Mkoa, na magari mengi ya JASCO yakaja tukapata matumaini ujenzi unaanza. Ujenzi ulipoisha nao wakaondoka (wakapotea wiki 5). wakarudi dec 13.

DECEMBER 13: Vikawekwa vibao vingi sana, Punguza mwendo (20km/h) ujenzi unaendelea, na tena wakafunga kile kipande cha kuanzia Makongo CCM mpaka ardhi wakaandika ujenzi unaendelea, wakapotea tena (wiki 4) (na vibao wakaviacha hapo)

JANUARY MWANZONI: Wakaja tena wakaitoi ile lami kipande cha kama KM1 kasoro pale ardhi, kisha wakapotea tena (wiki 4). wakatuacha tunakula vumbi hata kile kipande kilichokuwa na lami

FEBRUARY Mwanzoni: Wakaja wakakata miti pembezoni mwa barabara halafu hawakuitoa waliyoikata wakapotea tena (wiki 2)

February katikati, wakaanza kumwaga vifusi (siku nzima unakuta wamemwaka vifusi 4 - 5 tu)

Yaani kwa kifupi ujenzi wa barabara hii ni kero na unatia mashaka maana vifusi vimemwagwa bila barabara kutinduliwa na tayari wamevishindilia. Sasa hiyo r/lami itayowekwa hapo, sijui...

now tunaanza mwezi wa 5 lakini hatuoni ile speed ambayo tulitegemea. JASCO shida nini maana hata vitendea kazi haviko site.

UPDATE
Takribani mwaka sasa umepita tangu ujenzi wa barabara hii ulizinduliwa na leo tarehe 2 OCTOBER 2020, hakuna kinachoendelea,

Mbaya zaidi hali ya barabara imekuwa mbaya zaidi hasa kipande kila cha KM 1 Kilichokuwa na lami pale ardhi kutinduliwa na Mkandarasi kukitelekeza!

kipande hiki kwa sasa hakipitiki gari zinadunda kama mpira wa miguu! JASCO kila siku wanakuja wana mwaga vifusi na wanaondoka!

shida nini?
 
Mchawi hela.. Kama ni mkandarasi angekuwa mzembe asingefikisha hata wiki ungekuta katimuliwa
 
Nasikia Rugemalila na Daniel Yona wamegoma nyumba zao zisivunjwe hapo Makongo.
 
Nafikiri ifike mahali pia maslai ya watumiaji wa barabara yaangaliwe. Kweli barabari imekuwa kero sana kwa wakazi wa Goba, madale, makongo hata Mbezi
 
Pia hao Jasco hua wanakuja wanagusa gusa kama wiki moja wanapotea mwezi mzima na ndani ya hiyo wiki moja vifaa vyao vinaharibika wanaanza kutengeza hapo hapo barabarani

Hii kampuni ni yanani? Nna wasiwasi nayo asijekua Delmonte kabadili jina kaja kivingine. Maana Delmonte ni tapeli wakimataifa
 
Ya wahindi wa huko Mwanza.
 
Takribani miezi 4 sasa imeisha toka ujenzi wa barabara hii ya makongo juu kuzinguliwa (November 1) lakini ujenzi wake umezidi kusua sua kiasi kwamba unatia mashaka kama kweli mradi huu upo au ni danganya toto.

Miezi 4 sasa hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika na hata hii kampuni ya JASCO Constructions inatutia mashaka katika hili. Kumekuwa na sintofahamu sana kwani utendaji wao wa kazi kwa kiasi fulani unaleta sana usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii: haya ni maendeleo ya ujenzi

NOVEMBER 1: Ujenzi kuzinduliwa na mkuu wa Mkoa, na magari mengi ya JASCO yakaja tukapata matumaini ujenzi unaanza. Ujenzi ulipoisha nao wakaondoka (wakapotea wiki 5). wakarudi dec 13.

DECEMBER 13: Vikawekwa vibao vingi sana, Punguza mwendo (20km/h) ujenzi unaendelea, na tena wakafunga kile kipande cha kuanzia Makongo CCM mpaka ardhi wakaandika ujenzi unaendelea, wakapotea tena (wiki 4) (na vibao wakaviacha hapo)

JANUARY MWANZONI: Wakaja tena wakaitoi ile lami kipande cha kama KM1 kasoro pale ardhi, kisha wakapotea tena (wiki 4). wakatuacha tunakula vumbi hata kile kipande kilichokuwa na lami

FEBRUARY Mwanzoni: Wakaja wakakata miti pembezoni mwa barabara halafu hawakuitoa waliyoikata wakapotea tena (wiki 2)

February katikati, wakaanza kumwaga vifusi (siku nzima unakuta wamemwaka vifusi 4 - 5 tu)

Yaani kwa kifupi ujenzi wa barabara hii ni kero na unatia mashaka maana vifusi vimemwagwa bila barabara kutinduliwa na tayari wamevishindilia. Sasa hiyo r/lami itayowekwa hapo, sijui...

now tunaanza mwezi wa 5 lakini hatuoni ile speed ambayo tulitegemea. JASCO shida nini maana hata vitendea kazi haviko site.

Ni jana tu nilibahatika Kukutana na Dada mmoja hivi ambaye Mumewe ni Mkandarasi wa Nyanja mbalimbali ambapo amejenga Miundombinu kadhaa na Muhimu kabisa hapa nchini akaniambia ya kwamba hadi hivi sasa Kampuni ya Mumewe inaidai Serikali pesa iliyobakia kama Tsh Milioni 800 na kila wakienda Dodoma kuonana na Waziri husika huwa anawajibu kuwa Serikali haina Hela kwa sasa kwani nayo inasubiri Pesa kutoka kwa Mataifa Wafadhili. Na Waziri husika akamwambia Mumewe na wenye Hisa Wenzake katika hiyo Kampuni kuwa Kipaumbele cha sasa cha Mheshimiwa Rais ni Miradi mikubwa mikubwa Kwanza ambayo itamuinua kuelekea katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu na kuwataka waendelee kuwa Wavumilivu kuhusu Kulipwa Kwao kwani hata Yeye ( Waziri ) hana la Kufanya na anasikiliza tu Maagizo kutoka juu ( kwa Bosi wake ) Kiutawala. Na nikaenda mbele zaidi na Kugundua kuwa kuna Makampuni mengi sana ambayo yamefanya Kazi na Serikali lakini hadi hii leo hawajalipwa hadi Kupelekea Kampuni zingine Kushidwa Kujiendesha na Kufunga kabisa. Tutafichwa na kuambiwa maneno matamu kila uchao ila ukweli ni kwamba nchi ( Serikali ) haina Pesa ila inajitutumua tu kutaka Kuonyesha kuwa ina Fedha za Kutosha. Rais ana Vipaumbele vingi, analazimisha vyote vitekelezwe wakatai hali ya Uchumi kwa sasa kwa nchini Tanzania ni mbaya kutokana na sababu mbalimbali japo nyingi ni kutokana na Sera zake na Kudanganywa Kwake na Wasaidizi wake bila kusahau Washauri wake wakuu wa Kiuchumi hasa Watu wa TRA na BOT.
 
Ujenzi mwingine unao Sua Sua ni wa mwai kibaki road/old bagamoyo road Kazi inayofanyika pale haieleweki zaidi ya kuweka foleni
Inawezekana Hao wakandarasi Wanajuana na wakubwa

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Takribani miezi 4 sasa imeisha toka ujenzi wa barabara hii ya makongo juu kuzinguliwa (November 1) lakini ujenzi wake umezidi kusua sua kiasi kwamba unatia mashaka kama kweli mradi huu upo au ni danganya toto.

Miezi 4 sasa hakuna maendeleo yoyote yaliyofanyika na hata hii kampuni ya JASCO Constructions inatutia mashaka katika hili. Kumekuwa na sintofahamu sana kwani utendaji wao wa kazi kwa kiasi fulani unaleta sana usumbufu kwa watumiaji wa barabara hii: haya ni maendeleo ya ujenzi

NOVEMBER 1: Ujenzi kuzinduliwa na mkuu wa Mkoa, na magari mengi ya JASCO yakaja tukapata matumaini ujenzi unaanza. Ujenzi ulipoisha nao wakaondoka (wakapotea wiki 5). wakarudi dec 13.

DECEMBER 13: Vikawekwa vibao vingi sana, Punguza mwendo (20km/h) ujenzi unaendelea, na tena wakafunga kile kipande cha kuanzia Makongo CCM mpaka ardhi wakaandika ujenzi unaendelea, wakapotea tena (wiki 4) (na vibao wakaviacha hapo)

JANUARY MWANZONI: Wakaja tena wakaitoi ile lami kipande cha kama KM1 kasoro pale ardhi, kisha wakapotea tena (wiki 4). wakatuacha tunakula vumbi hata kile kipande kilichokuwa na lami

FEBRUARY Mwanzoni: Wakaja wakakata miti pembezoni mwa barabara halafu hawakuitoa waliyoikata wakapotea tena (wiki 2)

February katikati, wakaanza kumwaga vifusi (siku nzima unakuta wamemwaka vifusi 4 - 5 tu)

Yaani kwa kifupi ujenzi wa barabara hii ni kero na unatia mashaka maana vifusi vimemwagwa bila barabara kutinduliwa na tayari wamevishindilia. Sasa hiyo r/lami itayowekwa hapo, sijui...

now tunaanza mwezi wa 5 lakini hatuoni ile speed ambayo tulitegemea. JASCO shida nini maana hata vitendea kazi haviko site.

Naona mkandarasi JASCO yuko busy na barabara ya Chanika maeneo ya Buyuni, japo utendaji wao unatia shaka.
 
hakuna barabara iliojaa vibopa kwenye road reserve kama hiyo ya makongo juu. Daniel Yona ana miliki kimtaaa kizima huko juu kwahyo sakata lakuvunja nyumba linawaletea shida

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo barabara sijui ina siri gani, maana inajengwa tu midomoni utafikiri mpira wa yanga unaochezwa midomoni na kwenye magazeti
 
Hii barabara ya Makongo juu I bet haitajengwa hivi karibun.
Miti ilikatwa na Tanesco kwa ajili ya usalama wa nyaya za umeme na sio utanuz wa barabara

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom