Mbona wanaoshangilia Viti Maalum vya CHADEMA ni CCM?

Mbona wanaoshangilia Viti Maalum vya CHADEMA ni CCM?

Mdee amekubali vipi kuingia kwenye huu mtego wa hawa nyumbu...wamemlipa shilingi ngapi
 
Hata mjinga lazima ashangae. Iweje CCM ndio wanapambana kuwatetea hawa wabunge wa viti maalumu CHADEMA? Yaani CCM ghafla wamekuwa watetezi wa CHADEMA. Sasa nimeamini CCM hawana hata chembe ya aibu.

Watanzania amkeni, hawa CCM hawana utu hata chembe, tafuteni dawa nyingine ya kudeal nao tofauti na hii ya sanduku la kura. Haishangazi waliingiza kura fake na bila aibu wakajitangaza wameshinda kwa kishindo.
Leo Gazeti la Uhuru na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) linawatetea akina HALIM ( 640 X 640 ).jpg
 
Cha ajabu mi ndo naona aibu kwa vituko vyao, wao (mihimili) wala kama vile wapo sahihi, hii nji hii aaa!
 
CCM wameshika ndoano na wanawake wa Chadema ni ile nyama ya kwenye ndoano na samaki ni pesa ya mabeberu...Maccm hayawapendi hao wanawake wa Chadema bali pesa za mabeberu
 
Watetezi wa haki za wanyonge!
Hata mjinga lazima ashangae. Iweje CCM ndio wanapambana kuwatetea hawa wabunge wa viti maalumu CHADEMA? Yaani CCM ghafla wamekuwa watetezi wa CHADEMA. Sasa nimeamini CCM hawana hata chembe ya aibu.

Watanzania amkeni, hawa CCM hawana utu hata chembe, tafuteni dawa nyingine ya kudeal nao tofauti na hii ya sanduku la kura. Haishangazi waliingiza kura fake na bila aibu wakajitangaza wameshinda kwa kishindo.
 
Yani CHADEMA nilikuwa nakiamini na kukipigania,but sasa ni chama cha hovyo kabisa.Nitakaa tu bila ufuasi wowote ule
 
Ninawapa taarifa tu wanachama wa CCM ambao wanawaunga mkono wanawake 19 wa CHADEMA walionajisi katiba ya chama na kutengeneza uasi, Chadema kina wafuasi na wanachama zaidi ya milion 12 msitegemee yatokee mnayofikiria yanaweza kutokea. CHADEMA kitachukua hatua kali kwa mujibu wa sheria na katiba ya chama na hakitamuonea huruma.

ETI WANAWAKE WAPEWE HAKI YAO?
Hi ni kauli ya kijinga kabisa na ya kupuuzwa. Wanawake wa Chadema hawajapuuzwa mahali popote ispokua ni lazima waitumie na watii maamuzi ya chama ambayo hayalengi kuzuia mtu kwenda bungeni ispokua ni kukataa nafasi 19 feki ambazo zilitokana na uchaguzi feki. Tunajua kabisa fika kua uchaguzi huu ungekua huru na wa haki CHADEMA kusingekuwa na viti 19, ni zaidi ya hapo. Tungekua na na wabunge zaidi ya 100 wa majimbo.
Huu ulaghai wa makusudi unaratibiwa na ccm pamoja na kinachoitwa NEC kulazimisha Chadema kupamba matapishi hauwezi kufanikiwa.

ETI WANAWAKE HAWA WANA FAMILIA NA MADENI.
CHADEMA hakilei viongozi kiwe kama njia ya wao kulea familia zao badala ya kwenda kuhangaika na matatizo ya wananchi. Hakiwezi kula haramu eti kuna watu wana familia. Siasa siyo njia pekee ya kumfanya mtu alee familia yake, ni mapambano yanayolenga kuilea jamii yote.

ETI CHADEMA KIWAONEE WANAWAKE HURUMA?
Eti kwa sababu wao ni wanawake CHADEMA kukubaliane na ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi zilizofanywa na ccm, yaani kiendelee kuwachekea CCM eti kwa sababu kuna viti 19 vya wanawake. Hakuna huruma inayohalalisha haramu.
 
Hahaha Chadema ijitenge na COVID-19 ikibidi chama KIFUKIZWE ni sawa, ila COVID-19 ni hatari kwa Chadema.
 
Hata mjinga lazima ashangae. Iweje CCM ndio wanapambana kuwatetea hawa wabunge wa viti maalumu CHADEMA? Yaani CCM ghafla wamekuwa watetezi wa CHADEMA. Sasa nimeamini CCM hawana hata chembe ya aibu.

Watanzania amkeni, hawa CCM hawana utu hata chembe, tafuteni dawa nyingine ya kudeal nao tofauti na hii ya sanduku la kura. Haishangazi waliingiza kura fake na bila aibu wakajitangaza wameshinda kwa kishindo.
Maagizo toka juu ili wapate buku 7 ndo maana hata humu JF yamejaa na ujinga wao mpaka wachangiaji mahili wamehama wala haina mvuto tena. Lumumba yameteka JF hata mimi nitahama kama Mayalla ingawa sina njaa!
 
Hata mjinga lazima ashangae. Iweje CCM ndio wanapambana kuwatetea hawa wabunge wa viti maalumu CHADEMA? Yaani CCM ghafla wamekuwa watetezi wa CHADEMA. Sasa nimeamini CCM hawana hata chembe ya aibu.

Watanzania amkeni, hawa CCM hawana utu hata chembe, tafuteni dawa nyingine ya kudeal nao tofauti na hii ya sanduku la kura. Haishangazi waliingiza kura fake na bila aibu wakajitangaza wameshinda kwa kishindo.
Hawa CCM kwa kiwatetea wabunge wa viti maalum waChadema, wakati kwenye uchaguzi mkuu uliopita, wao ndiyo walikiwa mstari wa mbele kuhakikisha kuwa Chadema hawapati hata kiti kimoja kwa kuchaguliwa, inadhihirisha namna chama hiko kilivyo "machampion" wa wizi wa kura!
 
Back
Top Bottom