Mbona wasema kosa langu?

Mbona wasema kosa langu?

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Posts
33,771
Reaction score
41,027
Sasa umeolewa na una mme unayesema unampenda. Tumekutana baada ya miaka hii yote. Tulikuwa marafiki wa karibu hadi watu "walidhania". Sasa tumekutana unanilaumu.. kwanini sikukuomba moyo wako. Umesahau kuwa ni wewe uliyekuwa ukiniita "kaka"..? Leo wanilaumu wadai kuwa ulikuwa unasubiri nikuombe....

sijui nilie, nicheke, au nisikitike?
 
Haikuwa ridhiki yako.Tafuta mwingine kama bado huna,usije ukavuruga ndoa ya watu!
 
Mzee Mwanakijiji,
Cha mtu mavi uki....................................................,Temea chini mzee wangu kilishamilikiwa,usimuharibie mdada maisha yake.Kwa ushauri wangu ukimuona njia hii pita njia ile.Usije mtia najisi bure.
 
Sasa umeolewa na una mme unayesema unampenda. Tumekutana baada ya miaka hii yote. Tulikuwa marafiki wa karibu hadi watu "walidhania". Sasa tumekutana unanilaumu.. kwanini sikukuomba moyo wako. Umesahau kuwa ni wewe uliyekuwa ukiniita "kaka"..? Leo wanilaumu wadai kuwa ulikuwa unasubiri nikuombe....

sijui nilie, nicheke, au nisikitike?

Lakini mbona dada zetu huwa hawasemi kama amempenda mtu? ona sasa, pole MM.
 
Sasa umeolewa na una mme unayesema unampenda. Tumekutana baada ya miaka hii yote. Tulikuwa marafiki wa karibu hadi watu "walidhania". Sasa tumekutana unanilaumu.. kwanini sikukuomba moyo wako. Umesahau kuwa ni wewe uliyekuwa ukiniita "kaka"..? Leo wanilaumu wadai kuwa ulikuwa unasubiri nikuombe....

sijui nilie, nicheke, au nisikitike?

Mwambie asubirie next life..labda utamkonsida.
 
Sasa umeolewa na una mme unayesema unampenda. Tumekutana baada ya miaka hii yote. Tulikuwa marafiki wa karibu hadi watu "walidhania". Sasa tumekutana unanilaumu.. kwanini sikukuomba moyo wako. Umesahau kuwa ni wewe uliyekuwa ukiniita "kaka"..? Leo wanilaumu wadai kuwa ulikuwa unasubiri nikuombe....

sijui nilie, nicheke, au nisikitike?

Usilie, usicheke, wala usisikitike, wa kumhurumia ni huyo dada, ana matatizo makubwa moyoni na unahitaji kusaidiwa/msaada wako.

Wakati mlipokuwa marafiki wakaribu hata watu wakadhania, mwenzako alishakufungulia moyo ila tatizo lake ni 'uafrika' alikuwa anasubiri mpaka wewe uanze.

Naamini hilo na wewe uliliona na llijua, ila hukuanza labda kwa vile hakuwa chaguo lako, au muda wako kuamua ulikuwa bado.

Wakati aliyefunguliwa moyo haoni, wakatokea wengine, wao hawakufunguliwa moyo bali walikuja na ushawishi mkubwa na ahadi ya altareni, moyo ukafunguliwa, vigelegele vikapigwa.

Baada ya vigelegele, picha halisi za watu huanza, unajikuta ulivyodhania ndivyo, sivyo!.

Madada zetu wengi, hujikuta anampenda kwa moyo mwingine lakini ameolewa na mwingine for whatever reasons, nyingi ni 'marriages of convenience' mostly for security not for love.

Sasa mmekutana baada ya miaka mingi, ili kulinda siri ya moyo wake, lazima adanganye 'mume nampenda, ni kweli anampenda ila moyo ni kwako!

Just be close na huyo dada kwa kiwango ambacho kitafanya watu wasidhanie, atakufungulia moyo wake kuhusu maisha yake na wewe utapima utamsaidiaje.

Angalizo: Wako dada zetu wengi tuu wana maisha mzuri, nyumba, gari, pesa lakini wako kwenye mateso ya moyo, hivyo vingine vyote ni bure, ukimsaidia mtu wa aina hii hata kwa liwazo tuu la moyo 'not doing', unapata baraka kwa Mungu.
 
tatizo ni kuwa enzi "hizo" nilimdondokea lakini nilimheshimu kwa sababu alikuwa ananiita sana "kaka" na sikujua kuwa na yeye ananizimia.. wazazi wetu walikuwa ni marafiki na kwa kweli tumekua pamoja. Ni mambo haya ya masomo yakatutupa mabara tofauti na kupoteana kukaja... lakini sasa...ndiyo majaribu hayo.

Kama mwenye ndoa haiheshimu ndoa yake, wasio na ndoa wanatakiwa waiheshimu... ?
 
MM, kwa vile na wewe unamheshimu sana, chukulia kwamba anakupa taarifa ya yale yaliyokuwa yanausibu moyo wake kwa wewe kutotambua alikuwa ne kakudondokea. Heshima mbele mkuu asibadilishe misimamo yako ya maisha
 
MM jitahidi kushinda majaribu hayo,kama wakati ule uliweza kwa kigezo cha kaka bila shaka hata sasa hautashindwa.Muombe mwenyezi Mungu akuongoze katika hili!!!
 
Sasa akimletea mumewe vitimbi akaachika akitumaini tutakuwa pamoja itakuwaje? Oh well..haya mambo nasikia hayana kanuni..
 
Back
Top Bottom