Sasa umeolewa na una mme unayesema unampenda. Tumekutana baada ya miaka hii yote. Tulikuwa marafiki wa karibu hadi watu "walidhania". Sasa tumekutana unanilaumu.. kwanini sikukuomba moyo wako. Umesahau kuwa ni wewe uliyekuwa ukiniita "kaka"..? Leo wanilaumu wadai kuwa ulikuwa unasubiri nikuombe....
sijui nilie, nicheke, au nisikitike?
Usilie, usicheke, wala usisikitike, wa kumhurumia ni huyo dada, ana matatizo makubwa moyoni na unahitaji kusaidiwa/msaada wako.
Wakati mlipokuwa marafiki wakaribu hata watu wakadhania, mwenzako alishakufungulia moyo ila tatizo lake ni 'uafrika' alikuwa anasubiri mpaka wewe uanze.
Naamini hilo na wewe uliliona na llijua, ila hukuanza labda kwa vile hakuwa chaguo lako, au muda wako kuamua ulikuwa bado.
Wakati aliyefunguliwa moyo haoni, wakatokea wengine, wao hawakufunguliwa moyo bali walikuja na ushawishi mkubwa na ahadi ya altareni, moyo ukafunguliwa, vigelegele vikapigwa.
Baada ya vigelegele, picha halisi za watu huanza, unajikuta ulivyodhania ndivyo, sivyo!.
Madada zetu wengi, hujikuta anampenda kwa moyo mwingine lakini ameolewa na mwingine for whatever reasons, nyingi ni 'marriages of convenience' mostly for security not for love.
Sasa mmekutana baada ya miaka mingi, ili kulinda siri ya moyo wake, lazima adanganye 'mume nampenda, ni kweli anampenda ila moyo ni kwako!
Just be close na huyo dada kwa kiwango ambacho kitafanya watu wasidhanie, atakufungulia moyo wake kuhusu maisha yake na wewe utapima utamsaidiaje.
Angalizo: Wako dada zetu wengi tuu wana maisha mzuri, nyumba, gari, pesa lakini wako kwenye mateso ya moyo, hivyo vingine vyote ni bure, ukimsaidia mtu wa aina hii hata kwa liwazo tuu la moyo 'not doing', unapata baraka kwa Mungu.