Mbona watu wanabeza sana magari aina ya Toyota

Mbona watu wanabeza sana magari aina ya Toyota

Morg

JF-Expert Member
Joined
Oct 20, 2018
Posts
1,301
Reaction score
1,788
Kuna magari aina ya Toyota lakini Yana nguvu na speed sana. Mfano, Toyota landcruiser V8 lina nguvu imara na speed Sana BMW akasome , Subaru zote hapa zinakaa keti kwa huu mnyama.

Lakini kumekuwa na hulka ya watu kuponda magari aina ya Toyota sijui kwanini.

tapatalk_1586695059196.jpg
 
Hivi hili Gari huwa na ukubwa to engine kiasi gani CC zake
 
V8 ni "Tai -yota, zingine zilizobaki Ndio Toyota, soo ni kula popcorn na kuvunga tukiwa na Toyota zetu life liende.
 
Tatizo wengI wakiongelea Toyota wanaongelea mitumba ya ya mwaka 2001 hadi 2005 ambayo iko nyuma miaka 19 na 15 kitekinolojia.

Kuna vyuma vya 2015 hadi 2019 wengine wote wakasome
 
Hilo gari achana nalo hadi ulaya na USA yapo sana sio kama yale mengne ni nadra sana kukuta crown london..
 
Mkuu Toyota wanafanya vizuri sana, kupitia Lexus wana gari nzuri zinashindana na gari zinazotoka ulaya.

Kuna mnyama anaitwa Toyota Supra wakina Benz, BMW na Audi habari yake wanaijua vyema.
 
Ukisikia Toyota hazipendwi sio zote mkuu,kuna Toyota nyingine hata baadhi ya magari ya Europe hayasogezi mguu...
 
Mwenyeuzi nadhani kuna kitu hakijakaa sawa..

Watanzania kuwatenganisha na toyota ni sawa na kuwatenga na chama cha mapinduzi... never..

Ungesema wamiliki wa Toyota wanayaponda magari mengine hapo ungeeleweka....

Usishangae mwenye Passo akajitunisha kuliko mwenye Foresta,Grand Vitara au Murano kisa passo yake ni Toyota.
 
Karibia 75%ya magari yote yanayopatikana Tz ni Toyota, na nadhani kwa Africa sisi ndo tunaongoza kuagiza haya magari, tunayapenda sana
 
Mwenyeuzi nadhani kuna kitu hakijakaa sawa..

Watanzania kuwatenganisha na toyota ni sawa na kuwatenga na chama cha mapinduzi... never..

Ungesema wamiliki wa Toyota wanayaponda magari mengine hapo ungeeleweka....

Usishangae mwenye Passo akajitunisha kuliko mwenye Foresta,Grand Vitara au Murano kisa passo yake ni Toyota.
Mwenye passo atajilinganisha na mwenye Nissan March/micra.
 
Kuna magari aina ya Toyota lakini Yana nguvu na speed sana. Mfano, Toyota landcruiser V8 lina nguvu imara na speed Sana BMW akasome , Subaru zote hapa zinakaa keti kwa huu mnyama.

Lakini kumekuwa na hulka ya watu kuponda magari aina ya Toyota sijui kwanini.

Zinazopondwa ni hizi
Porte
Fun cargo
Vitz nk
 
Back
Top Bottom