SAYVILLE
JF-Expert Member
- Mar 25, 2010
- 7,895
- 12,975
Utaratibu wa kutoa post za "Thank You" kupitia mitandao ya kijamii kwa wachezaji au makocha wa benchi la ufundi wanaokoma kuitumikia timu umekuwa ni utaratibu mpya ulioanza kutumiwa na timu zetu hivi karibuni. Ukiangalia kwa makini namna tangazo la "Thank You", imeonekana kama ni unafki fulani kwa maana limekuwa linatumika zaidi kwa wachezaji ambao wameonekana hawana msaada tena kwa timu husika. Sijaona Thank You ikitumika kwa mchezaji aliyeuzwa au kwa kocha aliyeondoka huku club ikiwa bado inamuhitaji.
Sijaona Yanga wakipost Thank You kwa kocha msaidizi Cedric Kaze aliyekuwa mtu muhimu sana kwa misimu kadhaa pale Yanga. Inaonyesha kuondoka kwake pale Yanga kulikuwa kutokana na kutokubaliana mambo fulani fulani ya kimkataba.
Niliwahi kutabiri kuwa Yanga hawatapost Thank You kwa kocha wao wa viungo, Helmy Gueldich "Manywele" ambaye mashabiki wengi wa Yanga walikuwa wanaombea aendelee kuwepo pale Yanga. Nilisema huyu hawatatoa taarifa bali mtashangaa tu hayupo na nilikuwa sahihi, jamaa ameondoka kimya kimya bila taarifa yoyote kutolewa na Thank You yake haikutoka.
Je, huu uungwana tunaojaribu kuuonyesha kwa kutoa Thank You unatoka kweli moyoni kwa viongozi na watendaji wa vilabu hivi au hizi Thank You's zina maana nyingine?