Mbosso badilika, gemu itakushinda

Mbosso badilika, gemu itakushinda

Ahlan wasahlan wanajukwaa,

Huyu kijana wa kuitwa Mbosso "Khan Mushedede" kutoka viunga vya WCB kiundashi, melody na hata jinsi anavyoimba yuko njema.

Shida yake ni moja tu: habadiliki, kila siku nyimbo zile zile, uandishi ule ule, mahadhi yale yale. Kila wimbo anataja maandazi, kachori, chapati, mishikaki; mara nisugue, mara nikande, mara nibebe, mara niteme n.k.

Kiukweli inabidi abadilike kama anataka kufika mbali na kudumu kwenye gemu kwa muda mrefu. In short, mashabiki wamemchoka. Ushahidi ni huu wimbo wake mpya wa ate; mahadhi yale yale, uandishi ule ule, hadi mashabiki wameamua kumchana abadilike wamemchoka.

Yangu ni hayo tu.

"Njoo kichwa kichwa ule za uso saba"
Ngoja apitie hapa aone maandazi yake,kachori,kachumbali yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huu uzi hauchoshi wala hauboi,
Sijui Mboso alipita huku akajionea sambusa zake na kachori zilivyokinaisha.
 
Back
Top Bottom