Mbosso(WCB) vs Aslay, nini kitatokea?

Mbosso(WCB) vs Aslay, nini kitatokea?

Asley ameonekana kuwa Moto wa kukalia mbali baada ya Maromboso kutoa nyimbo zake mbili, Amekubali na Aleelee, ambazo zimeonesha wazi mapungufu yake katika kupangilia Sauti.

Inahitajika juhudi kubwa sana, Maromboso kufikia kiwango cha sauti na mashairi bora, kumpiku Asley..
 
Kushindana na mengine mengi ni mbwembwe... mwisho wa siku binafsi ningependa kuona wakifanikiwa kwenye muziki na kiuchumi... mambo ya kuwa masikini wenye majina.... cha muhimu shows za kutosha, collabo za uhakika, kukua nje ya tz na kuishi vizuri kulingana na thamani ya kipaji
 
Ahahaaaaaaaaaaah...
Naona watu wengi hawajui vizuri uwezo wa Mbosso..!
Lakini Aslay mwenyewe anajua Mbosso ni nani..!
Lakini muda utawajibu..!
 
Wadau wanasupport beef wanadai linakuza mziki.
 


Kwa wasiomfahamu Marombosso ni kijana hapo kwenye video, ambae alikuwa miongoni mwa wanaounda Yamoto band.

Kwa sasa ametoka kupitia WCB.

Wakati yupo Yamoto walikuwa wanachuana vikali na Aslay na inasemekana ni moja ya sababu kundi kuvunjika ni hivi vipaji viwili.

Kwa kutazama muono wa mbali tutarajie mchuano mkali ambao siwezi kuuita bifu bali ni mchuano wa vipaji toka kwa aslay na mbosso.

Nini kitatokea baada ya mchuano huo kuanza rasmi? Tuvute subira.

Aslay na yule katuni kam hamorapa ,sauti hovyo ,utunzi zero,uzoefu zero sura Mungu anajua

Eti kundi lilivunjika kwa kushindana ,acha upuuzi kijana
 
wcb ndo habari ya bongo hata kama hauna kipaji lazma utakubaliwa tu ..
 
Mleta mada angalau umeleta mfananisho unaoendana!!

Sie wengine tulikuwa tunaangalia tu walivyokuwa wanajaribu kumpambanisha Aslya na Diamond baada ya kuwa wameshindwa kwa Darasa!!! Tukaonya hapa, msimvimbishe kichwa dogo akajiona tayari ameshakuwa heavy weight manake yupo bado sana kuweza kumshindanisha na mtu mwenye fans base ya kufa mtu Afrika Mashariki yote and beyond!

Watu wakamjaza... wakamjaza... nasikia hivi sasa analia lia! Mara aandike barua kwa mama... mwanamuziki unaandika barua kwa mama badala ya kutunga wimbo kwa mama kumwelezea maswahibu yako!!!

Waliojulia muziki ukubwani wanadhani muziki is all about kuingia studio na kutoa hit song! Yes, muziki upo hivyo... lakini hakuna muziki pasipo tasnia ya muziki!

Na kwa kujibu swali la mleta mada, Maromboso atampoteza Aslay kwa sababu Mboso amezungukwa na watu wanaojua muziki na tasnia ya muziki!

All in all, I cry for Beka Flavor...

Jamaa una chuki za waziwazi kwa Aslay
 
Hoja mbovu kabisa! Unaweza kutaja sababu moja tu iliyokufanya uone nina chuki na Aslay?!

Kujua mziki ukubwani, amebaki kuandika barua kwa mama, mziki si kuingia studio tu nk
 
Kujua mziki ukubwani, amebaki kuandika barua kwa mama, mziki si kuingia studio tu nk
Yaani Aslay ninaemjua tangia akiwa mdogo anaimba ndo hivi sasa niseme amejulia muziki ukubwani?!

Wachangiaji hapa ndio nimewaita "waliojulia muziki ukubwani" na kwamba wanadhani music is all about kuingia studio na kutoa hit song! Aidha, kwavile hawafahamu tasnia ya muziki na fitina zake, wanadhani kujua kuimba ndo kila kitu wakati muziki ni zaidi ya kujua kuimba!

Na hoja hapa ni kutoa tahadhali kwa watu kuacha kuwavimbisha vichwa hawa madogo kwa sababu muziki ni zaidi ya kujua kuimba bali kufahamu jinsi tasnia inavyoenda! Na kwa kufahamu hilo ndo maana nikasema there's no way unaweza kumpambanisha au kumlinganisha Aslay na Diamond simply because Aslay anajua kuimba au anafanya hit songs!!

Na hili nililiongea sana hata wakati wa Ruby na kuwaambia watu waache kumvimbisha kichwa Ruby wakati bado hana ubavu wa kusimama mwenyewe!!! Lakini na yeye alivyo stupid, mitandao ya kijamii ikamjaza na kuanza kujiona another Jide!!!

Kuhusu Barua kwa Mama, of course, msanii unatakiwa kuweka feelings zako kwenye sanaa yako na sio kutafuta sympathy for nothing. Kilio cha Diamond cha kwenye SIKOMI kina tofauti gani na kilio cha Aslay?! Tofauti kubwa ni kwamba wakati mmoja kilio chake ni dhidi ya wapenzi wake mwingine kilio chake ni dhidi ya Walimwengu!!!

Lakini mwenzake hakutaka kulia lia bila faida; akaamua kutengeneza track na hiyo track bado inakimbiza Youtube!! Social conscious songs huwa zinakamata sana hisia za watu... sasa badala ya kuandikia mashairi na kutoa ngoma ili apige hela, anaishia kuandika Instagram... wtf!
 
Huwezi kuwaza kumshindanisha aslay na mbosso hata kidogo kwani wapo level tofauti kabisa.... Angalia historia ya asley kwenye muziki kabla na baada ya Yamoto Band,ni wazi kabisa aslay alitumika Kama chachu kuwainua kina mbosso na beka na wengineo ndani ya Yamoto Band na kuthibitisha hilo hata baada ya kundi kusambaa bado asley ameendelea kung'ara zaidi it's Like kundi lilimbana Sana sasa unawezaje kumlinganisha msanii mkubwa na underground ambaye anataka kutoka kupitia majina makubwa ya wasanii wenzake na lebo zenye majina
 
Huwezi kuwaza kumshindanisha aslay na mbosso hata kidogo kwani wapo level tofauti kabisa.... Angalia historia ya asley kwenye muziki kabla na baada ya Yamoto Band,ni wazi kabisa aslay alitumika Kama chachu kuwainua kina mbosso na beka na wengineo ndani ya Yamoto Band na kuthibitisha hilo hata baada ya kundi kusambaa bado asley ameendelea kung'ara zaidi it's Like kundi lilimbana Sana sasa unawezaje kumlinganisha msanii mkubwa na underground ambaye anataka kutoka kupitia majina makubwa ya wasanii wenzake na lebo zenye majina
hatujadili historia tunajadili uwezo walonao kwa sasa historia weka pembeni
 
Back
Top Bottom