Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mh Rais Samia Suluhu Hassan ameendelea kuonyesha kuwa anataka kulileta Taifa pamoja bila kuoneana na masikilizano kwa Watanzania wote.
 
Nimesafiri Dar Tunduma
Dar Mtwara
Dar Namanga
Dar Mwanza
Sijawahi kuona mti ambao unaweza kuukata na kuubuza barabarani ufunge njia.
I mean mti ukatwe na watu wanne, Kisha wauburuze mpaka ufunge barabara halafu kuwe na chaos.
Child's day pipe dream.
Rama tell us another one.
 
Wale polisi mashahidi washitakiwa kwa mateso waliyoyafanya kwa watuhumiwa.
 
Hii si sawa kabisa! Kuwaumiza watu kipindi chote kisha simply eti hana haja ya kuendelea na kesi.

Sheria hii ni kandamizi na haiwatendei haki watihumiwa kama hawatalipwa fidia.
 
Waliofurahi wana haki ya kufanya hivyo. Walioachiwa huru hongera zao. Kutokana na kesi hii kuna maswali najiyliza naomba mtu anisaidie kuniweka sawa.

Je ilikuwa ni sahihi kufungua kesi kama hii iliyochukua muda na pesa na mwisho kuiachia njiani?

Je DPP ameshtuka nini mpaka akaamua kubwaga manyanga?

Je kuna shinikizo lililosababisha ku drop mashtaka? Na kama ni ndiyo, hii ni nzuri kwa mfumo wa sheria?

Na mwisho wahanga wa kesi hii wana haki ya madai ya fidia?
 
Azingatie ushauri wa Mufti mzee wa Bakwata mzee wa hekima alioyeomba Raisi kuwa amsamehe Mbowe ila amkanye asirudie tena

Hawa wazee huyo Mufti na Pengo wakiongea kitu kauli zao huchukuliwa kwa uzito mkubwa mno sababu wanatambua kazi zao kama viongozi wa dini wako Cool na self disciplined

Nafikiri Mbowe mtu mzima ataelewa kwa nini katoka asirudie tena kupanga ugaidi.

Somo kalipata na kajua hii nchi sio ya kuchezea asirudie tena.

Huo ndio ujumbe anaotakiwa kuondoka nao
 
Serikali ilikuwa inaenda kuaibika sasa...wangeitwa kina DCI wa zamani, Samia, Zerro nk... walikuwa wanaenda kuvuliwa nguo.

Haki imeshinda. Kina Mbowe wafungue kesi ya kudai fidia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…