Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Leo kuna Ibada ya Njia Ya Msalaba aliyopitia Bwana wetu Yesu Kristo kuelekea kwenye ukombozi wa Wana wa Mungu.

Ni imani yangu Simon wa Kirene atatuongoza!

Updates;

Nawatakia Chadema wote Ibada njema ya Njia ya Msalaba.

Mungu ni MWEMA wakati wote.

Jumaa kareem.

The End.

Umeandika kitakatifu sana: barikiwa mwaka mzima.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Dogo usiwe na hasira kiasi hiki zinazosababishwa na umasikini kwenye ukoo wako!

Kama vipi mwambie mwamba akupe hata kibarua cha kufagia pale ofisini kwake sawa?!

Sent from my SM-T295 using JamiiForums mobile app
natoa amri makomandoo watabaki chini ya kiapo kuwa walinzi wa mwamba na watiifu kwa chama
 
Ni kwanini anashukuriwa Rais wakati suala hili lilikuwa ni la kimahakama na sheria? Rais hapa anaingiaje?
Au ndio ile kusema yeye ndio ana overrule kila kitu mpaka haki?
 
Mataga Vichaa kweli. Nimeona mitandaoni wameshaanza kumpongeza Mama. Wakati FAM anatengenezewa kesi walishangilia sasa ameachiwa nao wanashangilia
 
Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Leo kuna Ibada ya Njia Ya Msalaba aliyopitia Bwana wetu Yesu Kristo kuelekea kwenye ukombozi wa Wana wa Mungu.

Ni imani yangu Simon wa Kirene atatuongoza!

Updates;

Nawatakia Chadema wote Ibada njema ya Njia ya Msalaba.

Mungu ni MWEMA wakati wote.

Jumaa kareem.

The End.
Covid 19 huko walipo mavi yanasukuma pichu
 
Yaani ni contradiction kubwa. Sijui wanasheria za jinai watasemaje?

DPP huwa anaingiza “nolle prosequi” kama hana ushahidi madhubuti dhidi ya mtuhumiwa. Sasa hapa wameacha kesi imeendelea hadi mahakama kuthibitisha kuwa ushahidi wa mwendesha mashtaka umewakuta kina Mbowe wana kesi ya kujibu. Kabla hawajaanza kujitetea DPP anajitoa! Mahakama inasimama wapi hapo?

Ni aibu juu ya aibu!
ni aibu haswaa....
ni wazi option B zote zisingeuzika
 
sasa hapo kwani nani kashinda? kesi haijamalizika mwisho utasema mbowe kashinda? kahurumiwa awashhukuru wakuu wa dini mama kawaelewa
DPP kuamua kutoendelea na case maana yake ushahidi wake ni crap!Ingekuwa vinginevyo na ni huruma basi Mbowe angepewa masharti!
Toka mwanzo anasema anaamini hana hatia hivyo hawezi kuomba msamaha!Jiulize,iweje siku anayoanza kujitetea ndiyo siku anafutiwa mashtaka bila masharti?Iweje hicho kikao Cha viongozi wa dini kikae na Rais siku Moja kabla ya Mbowe kuanza kujitetea na siku Moja baadae aachiwe huru?Kwanini WS Walitaka kujua majina na anuani za mashahidi wa upande wa utetezi?Baada ya kunyimwa taarifa hizo,unadhani hawakuogopa kuwa surprised na utetezi?

Fact:Mbowe sio gaidi Kwa mujibu wa Katiba na sheria za nchi!
Sio gaidi kwenye macho ya viongozi wa kisiasa,kidini na hata mataifa ya nje!
 
mahakama na magereza hizi issues huwa tunawasingizia tu shida iko kwetu uraiani huku tungekuwa na hofu ya Mungu haya yote yasingekuwepo kwa sababu sisi kwa sisi ndiyo tunasingiziana makosa na kupelekana huko sasa mpaka mahakama ije ijuwe huna kosa umesota sana na pengine mahakama ishindwe kujuwa kuwa huna kosakutokana na mshitaki alivyojipanga kukushitaki mahakimu siyo malaika waweze kujua moja kwa moja kuwa huyu hana kosa wao wanacheza na sheria tu
Lkn ktk polisi kusingizia rais lipo sana, na sasa hivi unawekwa ndani na wanakudai kikombozi kuachiwa, kupewa dhamana au kumpelekea mahakamani.
 
Duh! Hebu waoneni hawa. Wana tofauti gani na wale wafuasi wa yule mfalme Zumaridi?


Kwani hujui wafuasi wa Chadema ndio wafuasi wa zumaridi ndio maana staili za kugaragara zinafana na hizo za Leo mahakamani hao nao ni makerubi na Maserafi wa Zumaridi Leo walikuwa mahakamani kesi ya Mbowe ni waumini wa Mfalme Zumaridi hao
 
Baada ya upande wa Mashtaka kufunga ushahidi wao na kuialika Mahakama kutoa hukumu ndogo na kisha mahakama kuwakuta watuhumiwa na kesi ya kujibu mnamo Februari 18 2022. Leo 04, Machi 2022 ni siku ya watuhumiwa kuanza kujitetea kutokana na tuhuma wanazotuhumiwa nazo.

Awali Mahakama iliwakuta na kesi ya kujibu katika mashtaka 5 kati ya 6 katika kesi ya uhujumu uchumi inayowakabili.

Kujua kesi ilipoishia fungua kiunganishi hiki:Mbowe na Wenzake 3 wakutwa na kesi ya kujibu. Kesi imeahirishwa hadi Machi 04, 2022 watuhumiwa kuanza kujitetea


=========

UPDATES

Jaji anaingia Mahakamani Muda huu Saa 4 na Dakika 52

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Jamuhuri Dhidi ya Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa hapa Mahakamani Muda huu

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Ikupendeze naitwa Robert Kidando Wakili wa Serikali Mwandamizi nipo na

Pius Hilla
Abdallah Chavula
Jenitreza Kitali
Nassoro Katuga
Esther Martin
Ignasi Mwinuka
Mawakili Wa Serikali Waandamizi Tulimanywa Majige
Wakili wa Serikali

Wakili Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Ikupendeza naitwa Peter Kibatala nipo Pamoja na

Paul Kisabo
Sisty Aloyce
Gaston Garubindi
Iddi Msawanga
Evaresta Kisanga
Maria Mushi
Nashon Nkungu
John Mallya
Jeremiah Mtobesya
Fredrick Kihwelo
Dickson Matata Ni hayo tu mh Jaji.

Jaji: Shauri lilikuwa lina kuja kwa Utetezi, Je Mnazo habari zozote za Wateja wenu?

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji ni kweli Kwamba Shauri lilikuwa limepangwa kwa ajili ya Utetezi Kwa Upande wangu tulifanya Maandalizi Mazuri Mimi John Malya, Dickson Matata, Fredrick Kihwelo na

Kibatala: wengine Juzi na Jana tulikuwa Ukonga na Segerea. Tulionana nao wakiwa na Bashasha kabisa, Kwamba Leo tunaendelea na Utetezi Lakini Leo Asubuhi tumepata Taarifa Kutoka Kwa Askari Magereza Kwamba Mbowe amepata Matatizo ya Ki Afya. Kwa hiyo hatuwezi Kuendelea,

Hivyo, Tunaweza Kupanga Kuendelea Jumatatu

Jaji: Jumatatu itakuwa Tarehe ngapi

Wakili Peter Kibatala: Tarehe 07 March 2022

Wakili wa Serikali Robert Kidando: Mheshimiwa Jaji Shauri limekuja kwa ajili ya Utetezi, na tumewasikia Wenzetu Maombi Waliyo Wasilisha Sasa tusingependa Kujibu Hoja hiyo, Kwa sababu na sisi tuna Maombi Mengine Kwa hiyo Kujibu Hoja hiyo haitokuwa na Maana sana

Mheshimiwa Jaji tunaomba Moja la Kufanya Mbele ya Mahakama yako Na Ombi hili Mheshimiwa Jaji ni kwamba Mkurugenzi Wa Mashitaka (DPP) kwa niaba ya Jamhuri anaomba Kuwasilisha Taarifa ya Kutokuwa na Nia na Kuendelea na Shauri hili

Na Taarifa hiyo tunaitoa Chini ya Kifungu cha 91(1) kwa Sheria ya Mwenendo Wa Makosa ya Jinai

Jeremiah Mtobesya: Tumesikia Taarifa ya Notes hiyo kutoka kwa Mkurugenzi Wa Mashtaka, na Kwa Bahati Mbaya hatuwezi Kusema lolote zaidi ya Kusema tunaichia Mahakama, sababu Kifungu Kinatoa Maelezo Yote Kwamba Baada ya Kusema hivyo tunaichia Mahakama dhidi ya Amri zake za Mwisho

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji Taarifa Hii tunaiwasilisha kwa Njia ya Maandishi, Kwa Maombi hayo ya Kifungu cha 91(1) tunaomba Kuondoa Mashitaka Yote dhidi ya Washitakiwa Wote Sababu zote zipo katika Noel Prosecui ambayo tumeiwasilisha

Wakili wa Serikali Robert Kidando: anapeleka Nyaraka Mbele ya Karani wa Jaji, na Karani anampatia Jaji

Jaji: Je umezungumza kwa niaba ya Defense Wote..?

Jeremiah Mtobesya: Mheshimiwa Jaji naomba kila Mmoja aseme

John Malya: Mheshimiwa Jaji notes iliyotolewa inayushuka Mikono wote, pamoja na Kujiandaa kwa ajili ya Kujitetea, Mikono yetu imefungwa na hatuwezi Kusema lolote, Tulitaka sana Warudishe Gharama zetu na Mengine lakini wacha Tusubiri Maamuzi ya Mahakama

Fredrick Kihwelo: Kwa niaba ya Mshtakiwa wa tatu Tumesikia Taarifa iliyotolewa, Tunaichia Mahakama iweze Kutoa Amri

Peter Kibatala: Mheshimiwa Jaji Na sisi tunaichia Mahakama, Sheria inajielezea wazi.. Mahakama ipo Kimya Kidogo na Jaji Bado anaandika

Kule Nje ni Kelele za Shangwe na Fifijo watu Wanaimba, Imebidi Mahakama Kufunga Vioo Vya Madirisha ili Kuzuia Kelele Kuingia Mahakamani, Wewe furaha yako ni Kiwango gani? Onyesha emoji ya furaha hapa Chini.. Au picha yako ukiwa na furaha kubwa..

Jaji: Baada ya Mahakama Kusikiliza Hoja iliyoletwa na Wakili Mwandamizi wa Serikali Kwamba Mkurugenzi wa Mashtaka hana nia ya Kuendelea na Kesi, na Upande wa Pili wakaridhia

Mahakama inasema Shauri hili lililo kuwa linawakabili Washitakiwa Khalfani Bwire, Adam Kasekwa, Mohammed Ling'wenya na Freeman Mbowe inatajwa nakiondosha Mahakamani na Washitakiwa Wanaachiwa huru bila Masharti, sababu Kuna Vielelezo vililetwa Mahakamani, naandaa Amri ya Kuviachia

Jaji: Na hivyo naelekeza Mkuu wa Magereza Kuwaachiwa Mara Moja, Leo na si Vinginevyo Natoa Amri Jaji anatoka Mahakamani Mahakama inaridima Kwa Shangwe.

=======
Freeman Aikael Mbowe na wenzake watatu, wameaachiwa huru leo, na Mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Baada ya DPP Kuwasilisha hati ya kutokuwa na nia ya kuendelea na shauri hilo, leo 4.3.2022. Hivyo, Freeman Aikaeli Mbowe

Viongozi wa dini waache kutumiwa na ccm

Wanatumika vibaya
 
Asante Rais wangu Mpendwa Mh. SSH. Mwenyenzi Mungu akupe hekima na ufahamu zaidi. Akupe kujawa na upendo na haki katika utendaji wako.

Mungu akupe kuisimamia nchi ktk haki pasipo kubebwa na nasty cabals zisizojali maslahi ya nchi. Kwa mwendo huu naamini Mungu atakupa nguvu ya kuwashinda wenye chama chao na kutuletea katiba na kuisimika mihimili inayosimamia haki bila kupepesa macho.

Asante sana nyote mliosimama Mwenyekiti Mbowe, naomba CCM wenzangu tuwe watulivu huku tukataka haki isimame imara ktk kila kitu hata katika chaguzi zote.
 
Ni kwanini anashukuriwa Rais wakati suala hili lilikuwa ni la kimahakama na sheria? Rais hapa anaingiaje?
Au ndio ile kusema yeye ndio ana overrule kila kitu mpaka haki?
Aliyeondoa kesi ni DPP siyo mahakana kwa hiyo upande wa serikali ndio wenye mamlaka ya kuondoa kesi za jinai mahakamani.
 
Back
Top Bottom