Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Mbowe aachiwa huru na wenzake watatu baada ya DPP kuwasilisha hati ya kutotaka kuendelea na kesi

Jamaa kamasi zilimtoka sana akaomba suluhu......🤣
Leo watabwatuka sana humu maana halkua wanamsemo wao mvua thelathini, sasa hamna mvua hata moja wakapambane na kingai huko
 
Sasa hii imeletwa na people's power au religious leaders' power? Au people's power kupitia religious leaders' power? Je, sio kutokana na external influence/ pressure wakati wa safari ya Rais huko ughaibuni na kuja kudanganyia viongozi wa dini ambao waliwapanga wenyewe!? Yaweza kuwa pia serikali iliona ingeshindwa kesi, hivyo kuwapanga viongozi wa dini!
 
Mnajisumbua tu hakuna katiba mpya hapa! Fanyeni kazi tujenge nchi! Acheni bla bla mtapigwa na vitu vizito kichwani

Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
Pole sana bwana naona mmepata pigo la kufa mtu lakini msijali ndio dunia ilivyo, haki waga haipotei ila inaweza kucheleweshwa tu.

Tunaendelea na mapambano ya kudai katiba mpya baada ya njama zenu kugonga mwamba.
 
Mchungaji Erasto anasema kama kuna watu wa kupongezwa katika ushindi wa Freeman Mbowe basi ni Wakili msomi Peter Kibatala na jopo lake lote.
Wengine ni Viongozi wawili wa Kiroho Shehe Ponda na Askofu Mwamakula.

Pia mh Tundu Lisu Mungu wa mbinguni ambariki sana kwa kufanya kila awezalo hadi akaonana " Ana kwa Ana" na Rais Samia

Hapa duniani ni vigumu sana kuruhusiwa kukutana na Rais wa nchi kwenye kikao cha Watu Wawili lakini Tundu Lisu ameweza, anasema mchungaji Erasto.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mungu wa mbinguni awabariki nyote.

Leo kuna Ibada ya Njia Ya Msalaba aliyopitia Bwana wetu Yesu Kristo kuelekea kwenye ukombozi wa Wana wa Mungu.

Ni imani yangu Simon wa Kirene atatuongoza!

Updates;

Nawatakia Chadema wote Ibada njema ya Njia ya Msalaba.

Mungu ni MWEMA wakati wote.

Jumaa kareem.

The End.
Sina cha kushangili maana alikuwa ameonewa kwa kubambikiwa kesi! kama angelikuwa kweli katenda kosa, basi ningelishangilia. Labda nishangilie HAKI IMESHINDA! Erythrocyte
 
Uzee wako ni uzee kweli au ni uzee wa kuchezea matope?

Mbowe hajakutwa na hatia bali KESI YA KUJIBU.
Maana yake wajitetee katika hayo wanayotuhumiwa...kwasababu yaliyosemwa yalisemwa na upande mmoja...kujitetea kwao ni kuipa mahakama kupima pande zote ndipo itoe hukumu.
Ndo ameshasamehewa sasa! Andamaneni kupinga huo msamaha! Aache vitendo vya kigaidi atakuja afungwe!!
 

ZITTO KABWE ATOA NENO KUACHIWA KWA MBOWE " NIMEFARIJIKA"​

 
Vipi Dr.Slaa atajisikiaje baada ya Mbowe kuachiwa pale aliposema anakerwa na watu wanaosema "Mbowe si Gaidi"?
 
Ivi kina mbowe na wenzake wata jisikiaje wakikutana na kingai, good luck, J4 malangahe, swila, homeboy Urio & other.....

Sisi binadamu tumeumbiwa Revenge ila Revenge nzuri ni kumwachia Mwenyezi Mungu....

Serikali Huwa zina siri nyingi....Ina wezekana hata kina mbowe na makomandoo wakawa poisoned...ili kuwadhohofisha afya Zao Taratibu hata kwa Miaka kadhaa.....

Wengi tulipaza sauti humu ndani.....Mpk mawe yaliandikwa mbowe sio Gaidi.....

Tulishauri humu ndani KUA Hii kesi ya ugaid ingemalizwa mapema.....pesa Bora zinge tumika kupambana na maadui wa taifa ambao tumeaninishwa Tangu UHURU ambao ni UJINGA, UMASKINI NA MARADHI

Natamani kuandika mengi nimefurah sanaa...Asante nying kwa team nzima ya mawakili wa utetezi kwa kumuaibisha Shetani.....

Asante nying sana kwa wadau wa Jf walio simamia ku post hatua kwa hatua katika kesi hii....

Asantee sanaa kwa wadau tulio kua team mbowe na makomandoo kwenye hii kesi ya UGAIDI.
 
Imekaa Njema Sana ,Chuki za kisiasa hazina tija,Mama SSH na DPP mmefanya jambo jema,hii kesi ilikuwa inawaharibia kimataifa.

Ugaidi wa laki 6 then ugaidi wa kumtumia mtu elfu 80??? seriously ,ugaidi wa kutaka kulipua vituo vya mafuta wakati hakuna hata kituo kilicholipuliwa.

Marekani ndiyo wanajua hasa ugaidi ni nini maana 9/11 hawatoisahau kamwe.
 
Chief Hangaya amesanda. Mbowe hataki ujinga wa kumpigia mtu magoti.

Salamu zimfikie Kingai🤣
 
Golikipa ni Fredrick Kihwelo, Mbavu ya kulia Sisty Aloyce, Mbavu ya kushoto Gaston Garubindi,
Halfback four yupo Iddi Msawanga
Center half kasimama Brigadia Generali Nashon Nkungu, Halfback six Evaresta Kisanga
Right wing ni Maria Mushi, Inside Eight ni Luteni Generali
John Mallya, Center forward ni Generali Peter Kibatala,
Inside Ten ni Luteni Kanali Jeremiah Mtobesya na Left wing ni
Meja Jenerali Dickson Matata...

Kwa kikosi hiki lazima uweke mpira kwapani...šŸ¤£šŸ˜‚šŸ¤£šŸ˜‚
Weraaaaa irudiwe waisikie...
 
Naomba kuuliza kutoka kwa wanasheria mbowe kakutwa na kesi ya kujibu lakn kabla hajajibu DPP Hana Nia ya kuendelea na kesi . Kuna mtego wowote hapa?
 
Huo ndio ukweli ila naweka angalizo tu kuwa Uyu mama raisi hajahusika kwa dhati kt kuachiwa kwa mwenyekiti.

...na kama kahusika basi wenzake wamemwambia Aibu kubwa wewe na serikali yako ingewahusu sana akaona itakuwa soo akawashauri majambazi wenzake waweke mpira kwapani.
Mchungaji Erasto anasema kama kuna watu wa kupongezwa katika ushindi wa Freeman Mbowe basi ni Wakili msomi Peter Kibatala na jopo lake lote.
Wengine ni Viongozi wawili wa Kiroho Shehe Ponda na Askofu Mwamakula.

Pia mh Tundu Lisu Mungu wa mbinguni ambariki sana kwa kufanya kila awezalo hadi akaonana " Ana kwa Ana" na Rais Samia

Hapa duniani ni vigumu sana kuruhusiwa kukutana na Rais wa nchi kwenye kikao cha Watu Wawili lakini Tundu Lisu ameweza, anasema mchungaji Erasto.

Maendeleo hayana vyama!
 
Back
Top Bottom