Ulichotoa hapo, na walichotoa wana ccm (kadogoo na Anfaal) vina tofauti gani? nimetumia neno spin za wanaccm, kama hii inakufanya wewe mwanaccm so be it.
Ngoja nikukumbushe jambo moja, miaka fulani iliyopita wakati mkapa akiwa preziii. CUF walifanya mkutano kigamboni (au temeke) kama sikosei. Polisi kama ilivyokuwa kawaida yao wakati wa uongozi wa mkapa, wakaenda wakatoa kipigo cha nguvu sana. Watu wengi sana waliumizwa na kupelekwa polisi. I know this kwa sababu nilikuwepo kwenye mkutano huo.
Mkutano uliofuatia, CUF wakampeleka Lipumba akasaidie kwenye kampeni. Polisi kama kawaida yao, wakatoa dozi kwa wafuasi wa CUF (this time wakampiga Lipumba). Lipumba akaumizwa mkono kutokana na kipigo. Kwa kuonesha solidarity kwa wanachama wake, Lipumba "akalizimisha" kukamatwa pia na polisi. Vyombo vya habari vikachukua picha... the next thing we know, picha zinaoneshwa kwenye TV na kwenye magazeti Lipumba akiwa kafungwa bandage akielekea kwenye tinga tinga la polisi.
Hiyo publicity ilikuwa too much for Mkapa to handle. Since then, polisi walianza kuwa na adabu kwenye mikutano ya CUF. Kama Lipumba angeingia mtini na kuacha wanachama wake, nadhani risasi za moto zingetumika kuwafagilia mbali.
Katika kampeni za upinzani, polisi wanatoa "heshima kidogo" kwa viongozi wa kitaifa. Wanachama wengine ni sisimizi tu wasio na thamani yoyote ile.