BAK
JF-Expert Member
- Feb 11, 2007
- 124,790
- 288,165
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ni mmoja kati ya mafisadi wazoefu hapa nchini. Alianza ufisadi huo miaka mingi iliyopita tangu alipokuwa karani wa mahesabu katika Benki Kuu akiwa chini ya baba mkwe wake, Edwin Mtei aliyekuwa Waziri wa Fedha, wakati huo, kabla hajatimuliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1979 kwa kulazimishwa ajiuzulu.
Kati ya mwaka 1993 na 1994, Mbowe alizama zaidi katika ufisadi akisaidiana na dada yake, Selina, aliyekuwa akifanya kazi Telex Room katika Benki Kuu kwa kushirikiana naye kutorosha fedha za kigeni kwenda nje ya nchi wakitumia akaunti ya Mhindi mmoja anayeitwa Shiraz aliyekuwa na akaunti yake huko London, Uingereza.
Selina ambaye baada ya kuiba sana na kaka yake na kukaribia kunaswa alikimbilia Marekani ambako amekuwa akiishi kwa miaka mingi iliyopita anahofia kurudi kutokana na dhambi aliyoitendea Tanzania.
Takwimu za ufisadi wa Mbowe zimejaa uharamia mkubwa kwa taifa, hivyo haieleweki kuona hivi leo anatumia kivuli cha Chadema kufichia uovu wake kwa Watanzania alioshiriki kwa miaka mingi kuwaibia fedha zao na kutaka aonekane kuwa ni kiongozi mwadilifu na pia mwenye uchungu mkubwa na raslimali za nchi yetu.
Kama Mbowe anabisha kuhusu ufisadi wake huo natoa changamoto kwake awaeleze wananchi undani na ukweli wa alivyokopa shilingi milioni 800 katika Benki ya Greenland, akachangia kuifilisi kinyume na maelezo aliyotoa hivi karibuni kwa waandishi wa habari akidai eti kuwa deni hilo alilipa huku akijua kwamba ni muongo.
Watu wanaelewa alivyofanya hila na mbinu chafu kuhakikisha documents zilizokuwa na kumbukumbu za mkopo wake zinaibwa kutoka benki hiyo na kupelekewa, akazichoma moto ili kupoteza kabisa ushahidi, jambo alilofanikiwa na ndiyo maana leo anaweza kusema kwa kujiamini kwamba alikopa na kulipa deni zima.
Kuiba nyaraka za mkopo na kuzichoma moto ili zisiwepo kabisa ndiko kulipa deni hilo?!
Hizi ni dalili za kichwa cha mwendawazimu. Watu wanataka kushupalia mkopo alioupata Mbowe wa shilingi 15 millioni ili kufanyia ukarabati Hotel ya Mbowe, sasa Billicana na kesi ipo mahakamani kama tulivyoambiwa na msemaji wa NSSF ambaye pia alikanusha kwamba mkopo huo haujafikia shilingi bilioni 1.2.
Wakati huo huo mafisadi waliokupua zaidi ya shilingi bilioni mia tano ambayo zaidi ya elfu thelathini na tatu ya ule mkopo wa Mbowe bado wanapeta mtaani hata majina yao kuyataja wanaogopa! lakini watu hawalioni hilo. Ama kweli kuna njemba zimeibuka from nowhere na kulipwa vijisenti vichache kama rushwa ili waharibu mjadala wa mafisadi unaoendelea kila kona ya Tanzania.
Nasema wamepokea rushwa kwa sababu haingii akilini kutaka kufananisha mkopo wa mbowe na mafisadi waliokupua karibu shilingi bilioni 500 ni vitu viwili ambavyo havina uwiano hata kidogo.