Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ni mmoja kati ya mafisadi wazoefu hapa nchini. Alianza ufisadi huo miaka mingi iliyopita tangu alipokuwa karani wa mahesabu katika Benki Kuu akiwa chini ya baba mkwe wake, Edwin Mtei aliyekuwa Waziri wa Fedha, wakati huo, kabla hajatimuliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1979 kwa kulazimishwa ajiuzulu.

Kati ya mwaka 1993 na 1994, Mbowe alizama zaidi katika ufisadi akisaidiana na dada yake, Selina, aliyekuwa akifanya kazi Telex Room katika Benki Kuu kwa kushirikiana naye kutorosha fedha za kigeni kwenda nje ya nchi wakitumia akaunti ya Mhindi mmoja anayeitwa Shiraz aliyekuwa na akaunti yake huko London, Uingereza.

Selina ambaye baada ya kuiba sana na kaka yake na kukaribia kunaswa alikimbilia Marekani ambako amekuwa akiishi kwa miaka mingi iliyopita anahofia kurudi kutokana na dhambi aliyoitendea Tanzania.

Takwimu za ufisadi wa Mbowe zimejaa uharamia mkubwa kwa taifa, hivyo haieleweki kuona hivi leo anatumia kivuli cha Chadema kufichia uovu wake kwa Watanzania alioshiriki kwa miaka mingi kuwaibia fedha zao na kutaka aonekane kuwa ni kiongozi mwadilifu na pia mwenye uchungu mkubwa na raslimali za nchi yetu.

Kama Mbowe anabisha kuhusu ufisadi wake huo natoa changamoto kwake awaeleze wananchi undani na ukweli wa alivyokopa shilingi milioni 800 katika Benki ya Greenland, akachangia kuifilisi kinyume na maelezo aliyotoa hivi karibuni kwa waandishi wa habari akidai eti kuwa deni hilo alilipa huku akijua kwamba ni muongo.

Watu wanaelewa alivyofanya hila na mbinu chafu kuhakikisha documents zilizokuwa na kumbukumbu za mkopo wake zinaibwa kutoka benki hiyo na kupelekewa, akazichoma moto ili kupoteza kabisa ushahidi, jambo alilofanikiwa na ndiyo maana leo anaweza kusema kwa kujiamini kwamba alikopa na kulipa deni zima.

Kuiba nyaraka za mkopo na kuzichoma moto ili zisiwepo kabisa ndiko kulipa deni hilo?!

Hizi ni dalili za kichwa cha mwendawazimu. Watu wanataka kushupalia mkopo alioupata Mbowe wa shilingi 15 millioni ili kufanyia ukarabati Hotel ya Mbowe, sasa Billicana na kesi ipo mahakamani kama tulivyoambiwa na msemaji wa NSSF ambaye pia alikanusha kwamba mkopo huo haujafikia shilingi bilioni 1.2.

Wakati huo huo mafisadi waliokupua zaidi ya shilingi bilioni mia tano ambayo zaidi ya elfu thelathini na tatu ya ule mkopo wa Mbowe bado wanapeta mtaani hata majina yao kuyataja wanaogopa! lakini watu hawalioni hilo. Ama kweli kuna njemba zimeibuka from nowhere na kulipwa vijisenti vichache kama rushwa ili waharibu mjadala wa mafisadi unaoendelea kila kona ya Tanzania.

Nasema wamepokea rushwa kwa sababu haingii akilini kutaka kufananisha mkopo wa mbowe na mafisadi waliokupua karibu shilingi bilioni 500 ni vitu viwili ambavyo havina uwiano hata kidogo.
 
Umetumwa ? ama ndo unalipa fadhila ya pesa ulizopewa na Nchimbi et al? Tupe thibitisho ya haya madai yako.....hizi hadithi za alinacha hazina mbele wala nyuma....Mod ipeleke hii mahali pake, udaku

Kaka waambie ukweli wamjue huyo Mbowe wao ambaye ata wadada wote aliowapa ubunge wamepata baada ya yeye na mh Zito kuwasulubisha kwa kupokezana...mbaya zaidi mh Zito alikuwa anaanza alafu jamaa na umachame wake ndio anafatia makombo.
 
What is the connection between pesa hizi za Mbowe kukopa na matusi ya nguoni haya ? Nadhani sasa Mods anzeni kufuta hoja za kitoto za namna hii .
 
Kuna udhaifu mmoja hapa JF akiguswa Mbowe tu!Uta majeshi yanakuja humu Mafisadi hao wanamchafua!wanalipwa na mafisadi kumchafua Mbowe!Sasa na wengine(wanasiasa)wakituhumiwa hapa JF wanalipwa na nani?
Mafisadi wamejadaliwa sana sana tu humu!kama kuna mada inayohusu Mbowe ijadaliwe kama kuna ukweli uanikwe!Kama majungu itajulikana!
Sasa Oooh Mbona wengine wameiba Mabilioni hawakamatwi Mbowe tu !Mjadala wa hao mafisadi kuiba Mabiloini na kutoguswa ni mjadala mwingine na zipo thread kibao zilizojadili hoja hiyo,Hapa hoja iliyopo JE MBOWE NAYE NI FISADI?HIZI TUHUMA NI ZA KWELI?
sasa kuja na hoja mmetumwa na mnlipwa kuja kumchafua Mbowe!kwani mbowe ni nabii au malaika hajadiliki,hazungumzwi?
 
Kweli bwana Salim,

Inabidi kweli kuwe na balance hapa JF, ccm lazima nao wapate utetezi hapa maana ufisadi haukuanza leo. Inabidi sasa wewe na wanachama wengine wengi wa ccm tuje hapa kwa wingi ili na sisi tuwachafue viongozi wa upinzani maana hii sasa imezidi.
 
Kaka waambie ukweli wamjue huyo Mbowe wao ambaye ata wadada wote aliowapa ubunge wamepata baada ya yeye na mh Zito kuwasulubisha kwa kupokezana...mbaya zaidi mh Zito alikuwa anaanza alafu jamaa na umachame wake ndio anafatia makombo.

Hivi na ile skendo ya Mbowe kutembea na mama Mkapa na pia kuwa anamfuatilia mke wa Kikwete kwani imeishia wapi? Watu wanadhani hapa ni mchezo, wao chadema wakileta ya Buzwagi na BoT basi wategemee na sisi CCM kuleta ufisadi wao wa ngono hapa JF!
 
Kuna udhaifu mmoja hapa JF akiguswa Mbowe tu!Uta majeshi yanakuja humu Mafisadi hao wanamchafua!wanalipwa na mafisadi kumchafua Mbowe!Sasa na wengine(wanasiasa)wakituhumiwa hapa JF wanalipwa na nani?
Mafisadi wamejadaliwa sana sana tu humu!kama kuna mada inayohusu Mbowe ijadaliwe kama kuna ukweli uanikwe!Kama majungu itajulikana!
Sasa Oooh Mbona wengine wameiba Mabilioni hawakamatwi Mbowe tu !Mjadala wa hao mafisadi kuiba Mabiloini na kutoguswa ni mjadala mwingine na zipo thread kibao zilizojadili hoja hiyo,Hapa hoja iliyopo JE MBOWE NAYE NI FISADI?HIZI TUHUMA NI ZA KWELI?
sasa kuja na hoja mmetumwa na mnlipwa kuja kumchafua Mbowe!kwani mbowe ni nabii au malaika hajadiliki,hazungumzwi?

Hakuna udhaifu wowote! Hebu linganisha tofauti kati ya mkopo wa shilingi milioni 15 ambayo kesi yako iko mahakamani na mafisadi waliokupuwa shilingi bilioni 500 ambao hata kutajwa majina wanaogopwa! Tofauti ni kama usiku na mchana kama hutaki kuiona hili ni lako wewe. Tusifananishe ndimu na machungwa kuna tofauti tena kubwa sana!
 
Naona wachangiaji wengi wanajitahidi kuleta hoja kisiasa zaidi, kunatofauti kubwa sana kati ya Mkopo na wizi, anayechukua mkopo anatakiwa kulipa kulingana na masharti ukikopa huwezi itwa FISADI, yule anayeiba kisheria anatakiwa akamatwe na afunguliwe mashitaka, kuna tofauti kubwa sana kulaghai kwa kutumia kampuni zisizokuwepo kuiba keki ya taifa mfano EPA, Richmonduli kila muhusika anakataa hata kusikia Richmonduli...haya ni mawazo yangu na mchango wangu katika kujaribu kuendelea na vita zidi ya mafisadi. Wale waliojikopesha EPA mbona hata majina inakuwa ngumu kuyataja?

Sitetei mtu,mimi na sinufaiki zaidi ya kujifunza zaidi hapa JF nini kipo behind the scene, Kuna watu waniPM kunikashfu na kunitishia, nawaomba waache wakiendelea nitazipost PM zao kwangu hapa jamvini...kwanini unitukane kama sikubaliani na wewe? ama wenzangu mnamshiko ? tuambiane basi I am just putting my thought hapa kama hukubaliani basi nijibu kwa hoja, usinitishie eboooooo

Ushi wa Rombo
 
Hivi na ile skendo ya Mbowe kutembea na mama Mkapa na pia kuwa anamfuatilia mke wa Kikwete kwani imeishia wapi? Watu wanadhani hapa ni mchezo, wao chadema wakileta ya Buzwagi na BoT basi wategemee na sisi CCM kuleta ufisadi wao wa ngono hapa JF!

kwa hiyo nyie huko ccm mambo ya mbowe na mama mkapa au mbowe na mama Kikwete (hata kama ni yakweli) yana manufaa gani kwa taifa?Mambo mengine hata yanatia aibu kabisa..... grrrrrrrrr
 
hawa jamaa wana ajenda ya siri, lengo lao ni kudilute mijadala yetu hapa Jf, ili baadae ionekane hapa ni genge la wahuni wenye habari za kizushi.

Mamods sijui wanakuwa wapi sometimes, mfano thread kama hii ilibidi iwe merged na ile inayozungumzia ufisadi wa mbowe,
 
Gamba la nyoka,

wanachotaka hapa kina purpose nyingi zaidi, pamoja na kudilute mijadala, wanaanzisha pia mambo ambayo yako below standard ili thread zao zihamishwe na waanze kulialia kuwa kuna upendeleo hapa JF?! All is done ili kuhafifisha JF lakini kumbuka kuwa sio kwamba wameanza leo na hawatakwisha leo.

Kitu kimoja lazima wajue ni kuwa kila wakileta udaku wao (kama huo hapo juu kuwa Mbowe alifanya mapenzi na mama mkapa au ule wa kuwa Mbowe anamfukuzia mama Kikwete) basi wataaibishwa bila kukopeshwa. Meanwhile, wana JF wengine wataendelea na mapambano bila kutingishwa hata kidogo!
 
Ndio maana Rev Kishoka akaanzisha topic ya "Tumevamiwa?", nafikiri aliona mbali huyu mwenzetu!
 
Kuna mada ya kuingiliwa hapa .Mengi yamesha sema lakini hapo juu jamaa anasema sasa wanaleta mada ya kufitinisha .Lakini wajue kwamba Watanzania are not foolish people .Wanaujua ukweli na mbinu chafu zimeanzia Dodoma hadi leo kwenye makundi ndani ya CCM.Mtaleta hoja zitakufa kama ni kulipiza kisasim lakini nashangaa pia kwamba Upinzani Nchi nzima sasa ni Mbowe kama vile wengine hawapo.Hili jambo zuri kwa angalau CCM kujua kwamba Chadema ni Chama Mbadala no matter what .Wajanja wote wamesha jua la kufanya a kinacho endelea. Siku za nyuma kabisa niliwahi kusoma hapa mpango wa kuwachafua Mbowe na Chadema.Yale ya zamani ndiyo haya sasa .Leo mtu ana akili anaweza kusema Mbowe anatembea an Mke wa JK ama Mkapa ? This is A Curse .
 
Tatizo lao wengine wanadhani kuwa wasomaji wa JK wana elimu kama wasomaji wa magazeti ya Shigongo (mlokole anayechochea uzinifu kuliko hata shetani mwenyewe). Katika hili la Mbowe kutembea na mama mkapa na mama kikwete nadhani wameenda below hata uchemfu wa kawaida.
 
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe ni mmoja kati ya mafisadi wazoefu hapa nchini. Alianza ufisadi huo miaka mingi iliyopita tangu alipokuwa karani wa mahesabu katika Benki Kuu akiwa chini ya baba mkwe wake, Edwin Mtei aliyekuwa Waziri wa Fedha, wakati huo, kabla hajatimuliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, mwaka 1979 kwa kulazimishwa ajiuzulu.

Kati ya mwaka 1993 na 1994, Mbowe alizama zaidi katika ufisadi akisaidiana na dada yake, Selina, aliyekuwa akifanya kazi Telex Room katika Benki Kuu kwa kushirikiana naye kutorosha fedha za kigeni kwenda nje ya nchi wakitumia akaunti ya Mhindi mmoja anayeitwa Shiraz aliyekuwa na akaunti yake huko London, Uingereza.

Selina ambaye baada ya kuiba sana na kaka yake na kukaribia kunaswa alikimbilia Marekani ambako amekuwa akiishi kwa miaka mingi iliyopita anahofia kurudi kutokana na dhambi aliyoitendea Tanzania.

Takwimu za ufisadi wa Mbowe zimejaa uharamia mkubwa kwa taifa, hivyo haieleweki kuona hivi leo anatumia kivuli cha Chadema kufichia uovu wake kwa Watanzania alioshiriki kwa miaka mingi kuwaibia fedha zao na kutaka aonekane kuwa ni kiongozi mwadilifu na pia mwenye uchungu mkubwa na raslimali za nchi yetu.

Kama Mbowe anabisha kuhusu ufisadi wake huo natoa changamoto kwake awaeleze wananchi undani na ukweli wa alivyokopa shilingi milioni 800 katika Benki ya Greenland, akachangia kuifilisi kinyume na maelezo aliyotoa hivi karibuni kwa waandishi wa habari akidai eti kuwa deni hilo alilipa huku akijua kwamba ni muongo.

Watu wanaelewa alivyofanya hila na mbinu chafu kuhakikisha documents zilizokuwa na kumbukumbu za mkopo wake zinaibwa kutoka benki hiyo na kupelekewa, akazichoma moto ili kupoteza kabisa ushahidi, jambo alilofanikiwa na ndiyo maana leo anaweza kusema kwa kujiamini kwamba alikopa na kulipa deni zima.

Kuiba nyaraka za mkopo na kuzichoma moto ili zisiwepo kabisa ndiko kulipa deni hilo?!

Watu gani hao wanaoelewa zaidi yako wewe uloleta hii hadithi ya enzi za Deborah Mwenda - hadithi yenyewe uliianza vizuri - hongera unaweza kuandika udaku ukauza mitaani, lakini uliharibu ulipotaja uchomaji wa nyaraka - kama hili ni kweli tupatie ushahidi alizichomea wapi na ni kina nani hao waliziiba na kumpelekea - bila hivyo unampa sifa Mbowe kuwa ana uwezo wa kupata nyaraka za siri katika nchi hii - Mbona hatujamuona kutuletea majina ya wanaodaiwa kurejesha pesa za BOT na najua hilo linamkera na litamuongezea umaarufu - jamani wacheni hizi hapa JF huwa tunataka Ushahidi, Kweli aliyosema Rev. Kishoka - TUMEINGILIWA.
 
[/COLOR][/SIZE]

Hii issue ya kuiba na kuchoma benki wamewekewa watu wengi sana hapo Tanzania - kwenye ile thread ya mabaya ya Nyerere, kuna mtu alisema kuwa pesa za BoT zilichukuliwa na Nyerere kupitia kwa Nyirabu (wote ni watu wa musoma) na baadaye ikabidi nyerere achome benki ili kuficha ushahidi naona sasa wameanza kusema kuwa ni MBowe alifanya haya...

Naona ccm wanatapatapa sana hapa JF!
 
hawa jamaa wana ajenda ya siri, lengo lao ni kudilute mijadala yetu hapa Jf, ili baadae ionekane hapa ni genge la wahuni wenye habari za kizushi.

Mamods sijui wanakuwa wapi sometimes, mfano thread kama hii ilibidi iwe merged na ile inayozungumzia ufisadi wa mbowe,

Nakubaliana na wewe Mwafrika wa Kike kuna mengi ya muhimu ya kuyajadili lakini kuna watu wanazungumzia mambo ya uhusiano wa watu binafsi( kama ni kweli)- la kulijadili kwe nchi yetu ilipofikia ni lini mwananchi wa kawaigda atajiona yuko huru katika nchi yake na kufaidi rasilimali tulizopewa na Muumba ambaye kusema kweli katupendelea kaw kutupa hizo rasiloimali ukilinganisha na nchi nyingi duniani.
 
mimi nasubiri kuona kuwa kama ikithibitishwa kuwa Mbowe katembea na mama mkapa au mama kikwete sijui nani atapata aibu kubwa kwa kulingana na tamaduni na fikra za watanzania wengi, aliyechukua au aliyechukuliwa mke?

Otherwise, endeleza mapambano kule kwingine maana mafisadi wanajua kuwa kamati ya madini imekaribia kutoa report yake kwa hiyo wameanza kuchachawa ukichukulia kuwa miezi ya EPA nayo imekaribia kuisha!
 
[/COLOR][/SIZE]

Watu gani hao wanaoelewa zaidi yako wewe uloleta hii hadithi ya enzi za Deborah Mwenda - hadithi yenyewe uliianza vizuri - hongera unaweza kuandika udaku ukauza mitaani, lakini uliharibu ulipotaja uchomaji wa nyaraka - kama hili ni kweli tupatie ushahidi alizichomea wapi na ni kina nani hao waliziiba na kumpelekea - bila hivyo unampa sifa Mbowe kuwa ana uwezo wa kupata nyaraka za siri katika nchi hii - Mbona hatujamuona kutuletea majina ya wanaodaiwa kurejesha pesa za BOT na najua hilo linamkera na litamuongezea umaarufu - jamani wacheni hizi hapa JF huwa tunataka Ushahidi, Kweli aliyosema Rev. Kishoka - TUMEINGILIWA.

Hizi ni shutuma nzito sana .Kazito Mtikila na leo someone is doing the same hapa JF.Ni kesi mbaya sana ya kuiba na kuchoma document za serikali . Je yeye mleta mada alikuwa wapi wakati haya yanatokea ? Kwa nini sasa asifungue kesi atoe ushahidi wa hili Mbowe achukuliwe hatua ?
 
Back
Top Bottom