Making judgement after hearing one side only is biased & unfair. Hata mahakamani husikilizwa pande zote mbili. Although i say yes the company should pay because whether the interest is too high or not ni walikubali wenyewe na wakaona wanaweza but i think we should also try to find out why they haven't made payments in the first place. Its possible hawana kisingizio cha kuto kulipa but just to be unbiased we should hear the other side of the strory & look at botth sides of the shillings.
mwanafalsafa hili la deni la mbowe hotel na NSSF siyo geni na upande wa pili umeshatolewa mara kadhaa..
Mbowe ajitetea kuhusu ufisadi

Tuesday, 18 March 2008 Mwandishi Wa Habari Leo
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema anaamini habari za yeye kudaiwa mamilioni na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na amri ya kukamatwa kwake, zinakuzwa na wapinzani wake katika siasa aonekane fisadi na apunguze kasi ya kutaka kuchukuliwa hatua kwa waliozoa mabilioni Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alikiri kuwa kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd ilikopa Sh milioni 15 kutoka NSSF mwanzoni mwa miaka ya 1990, lakini ameshindwa kumalizia kulipa mkopo huo kutokana na utata uliopo kwenye riba, licha ya kuwapo kwa amri ya Mahakama Kuu tangu mwaka 2004 ya kutaka akamatwe kwa kushindwa kulipa.
Habari hizi zinazojaribu kunipaka matope leo hii zikigeuza kesi ya Mbowe Hotels ambayo kimsingi ni ya biashara ili ichukue sura ya siasa na ufisadi
zinalenga kuniharibia heshima yangu kwa jamii na kunichonganisha na wanachama wa Mfuko (NSSF), alisema Mbowe huku akitamba kwamba ataendelea kupigania haki.
Alisema kutokana na vuta nikuvute hiyo ya deni la NSSF, mkewe, Dk. Lillian Mbowe, alikamatwa mwaka jana na kupelekwa Mahakama Kuu mbele ya aliyekuwa Jaji Kiongozi Amiri Manento, ajieleze kwa nini asifungwe kwa kushindwa kuheshimu amri ya kulipa deni.
Wakati huo Freeman alikuwa masomoni Uingereza. Habari za mkopo unaolalamikiwa na Mbowe na riba juu yake ziliripotiwa kwa mara ya kwanza magazetini wiki iliyopita, huku ikielezwa kuwa deni hilo limefikia Sh bilioni 1,200 na kwamba Mahakama Kuu imetoa amri ya kukamatwa kwa wakurugenzi wa Mbowe Hotels.
Akijitetea jana, Mbowe alisema kampuni yake ilipewa mkopo huo kwa ajili ya upanuzi na uboreshaji wa hoteli yake Dar es Salaam na
wakati anakopa riba iliyokuwa inatolewa na NSSF, ilikuwa asilimia 31 na hadi kufikia Juni mwaka jana, kampuni yake ilikwisha kulipa Sh milioni 75.5, kiasi ambacho alisema ni mara tano ya kiwango kilichokopwa.
Alisema ugomvi wake na NSSF ni riba, kwani kampuni yake imekuwa inaiandikia NSSF ipitie upya mkataba wa mkopo huo, jambo alilodai ni la kawaida kwa kila taasisi ya fedha inayojua wajibu wake na yenye nia njema kwa wateja wake.
Mchanganuo wa kitaalamu wa deni la sasa la Mbowe Hotels Ltd pamoja na riba ni Sh milioni 43.2.
Hili mimi ndilo ninalojua kwamba bado wanatudai na tumekuwa tunawaomba tukae nao turejee mkataba juu ya mchanganuo huu, lakini hawataki, alisema. Alisema kama mfanyabiashara, amekuwa anakopa katika benki mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji katika miradi mbalimbali na amekuwa analipa bila matatizo.
Iweje hawa NSSF wagome kufanya hivyo
na wao ndiyo wamekuwa chanzo cha kuchelewesha kulipwa kwa deni hilo, kwani hawataki kukaa na sisi kurejea mkataba huo, alisema Mbowe anayemiliki baadhi ya biashara nchini, zikiwamo za hoteli. Mbowe alisema mkataba na NSSF ulioingiwa mwaka 1990 uligubikwa na mizengwe mwaka mmoja tu tangu kuingiwa.
Alisema kampuni yake iliomba kuongezewa mkopo kukamilisha mradi uliokusudiwa, lakini ilichukua mwaka mmoja kutoa jibu la kukataa kwa madai kuwa kutoa fedha za ziada siyo sera yao. Mfanyabiashara huyo alisema baada ya kukataliwa alianza upya mchakato wa kutafuta mkopo na akaenda benki ya CRDB ikakubali kumkopesha.
Wakati hali hii ikiendelea, NSSF ilianza kudai marejesho ya riba kwa mkopo waliotoa kwa mradi walioufadhili na kuutekeleza. Alisema mwaka 1996 ukiwa mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi ambao alishiriki kama mgombea wa upinzani katika Jimbo la Hai, wadhamini wa NSSF walifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu wakidai malipo ya Sh milioni 80.1 ikijumuisha salio la deni mama la Sh milioni 12 na riba ya Sh milioni 68.1.
Alisema tangu mwaka 2003 walikubaliana na NSSF wakae wazungumze, lakini baadaye shirika hilo likawa kimya. Alisema mwaka jana, kampuni yake iliiandikia tena NSSF kuomba wakubali mapendekezo ya kumaliza deni hilo na barua nyingine; lakini hawajajibu barua hizo hadi leo, ikiwa ni miezi minane tangu waandikiwe barua hizo.
Juhudi za kuwapata maofisa wa NSSF kuzungumzia suala hilo hadi jana jioni hazikufanikiwa. Mbowe alisema anaamini baadhi ya watu wanavitumia vyombo vya habari kumchafua yeye ili Watanzania wageuzie mawazo yao kwenye habari zake na NSSF na wasahau habari za ufisadi wa EPA na Richmond zinazowagusa baadhi ya viongozi.
Habari hiyo hiyo iliripotiwa hivi na IPP
Wananizulia kufifisha vita dhidi ya ufisadi - Mbowe
2008-03-18 10:18:16
Na Mashaka Mgeta
Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbowe Hotels Limited, Bw. Freeman Mbowe, amesema tuhuma zinazomkabili kuhusu kinachoitwa `hujuma` dhidi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), zina lengo la kufifisha vita dhidi ya ufisadi nchini.
Bw. Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliyasema hayo akiwa na Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo, Dk. Lilian Mbowe, ambaye ni mke wake, walipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.
Wiki iliyopita, baadhi ya vyombo vya habari, viliripoti kuhusu kampuni hiyo kukopa Sh. bilioni 1.2 za NSSF, lakini Bw. Mbowe, alisema deni halisi lilikuwa Sh milioni 15 zilizokopwa mwaka 1990.
Alisema fedha hizo zilikopwa wakati huo NSSF ikijulikana kama Mfuko wa Taifa wa Pensheni (NPF), kwa makubaliano ya kulipa riba ya asilimia 31, ili itumike katika mradi wa kupanua na uboreshaji wa hoteli yake jijini hapa.
Bw. Mbowe, alisema mwaka mmoja baada ya mkopo huo kusainiwa, hali ya kutoelewana ilijitokeza kati ya pande mbili hizo, baada ya kampuni yake kuomba ongezeko la mkopo ili kukamilisha mradi wake.
Alisema ombi hilo lilikubaliwa, lakini NSSF ilitumia kigezo cha sera zake kutoruhusu ongezeko la mkopo na kuishauri (kampuni ya Mbowe), kukopa katika taasisi nyingine ya fedha.
Bw. Mbowe, alisema ilibidi kampuni yake kukopa fedha katika Benki ya CRDB, ikiwa ni kiasi kikubwa kuliko kilichokopwa NSSF.
``Ni dhahiri kuwa mradi huu uliathiriwa kwa kiasi kikubwa, na ninaamini umakini na utaalamu wa kibenki haukutumika katika maamuzi haya� Inanilazimu kuhoji uwezo wa kitaaluma wa Mfuko kujishughulisha na biashara za ukopeshaji,`` alisema.
Bw. Mbowe, alikiri kuwapo kesi namba 277 iliyofunguliwa Septemba, 1996 na Bodi ya NSSF dhidi ya kampuni yake, ikidai malipo ya Sh. milioni 80.1, ikiwa ni jumla ya salio la deni mama la Sh. milioni 12 na riba ya Sh. milioni 68.1.
Alisema ombi hilo lilikubaliwa na Mahakama Kuu bila upande wa walalamikiwa ama wakili wao, kuwapo mahakamani hapo.
Bw. Mbowe, alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka jana, kampuni yake ilishalipa Sh. milioni 75.5 na kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaalamu, deni la sasa linapaswa kuwa Sh. 43,169,727.
Hata hivyo, alisema kampuni yake iliwasilisha ombi namba 151 na 152 la mwaka juzi, kutaka amri ya kukamatwa kwa Wakurugenzi wake (akiwamo Mbowe) isitekelezwe, na Mahakama ya Rufaa ilikubali.
Bw. Mbowe, alisema kesi ya kusikiliza dai la kampuni yake, kuhusu shauri la msingi kuwa na hukumu mbili, itasikilizwa Aprili 29, mwaka huu, Mahakama Kuu.
Hivyo, Bw. Mbowe, alisema taarifa zinazomhusisha na ufisadi katika NSSF, zina lengo la kuipotosha jamii, na kuondoa fikra za umma kutoka kwa watu waliohujumu uchumi na mali za umma, kwenda kwa `Mbowe na NSSF`.
Kwenye mkutano huo, Bw. Mbowe alifuatana pia na wabunge Bw. Chacha Wangwe (Tarime), Bw. Kabwe Zito (Kigoma Kaskazini), Bw. Said Arfi (Mpanda Kaskazini) na Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, Bw. John Mnyika.