Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

hizo number nina wasiwasi nazo kama zina ukweli wowote,nina uhakika huyo mwandishi ni kilaza na hana idea anaandika nini...unakopa 12m in 2003 unaishia na deni la 5billion 2009? hakuna kitu kama hicho hata kama interest ni 100%...hawa inabidi wasome kabla ya kuandika upupu wao!
 
Kwa hilo la kuandika kama vile Mbowe Hotels inadaiwa bilioni 58 zote nakubali ni kosa. Kama kuna wengine wana daiwa zaidi yake kwanini wameandika kana kwabwa yeye ndiyo anadaiwa hizo bilioni 58 zote? Au kama vile yeye ndiyo mdaiwa deni kubwa zaidi. A lot of things in countries like ours are politically & business motivated. Ni aidha wamefanya hivyo kuuza gazeti au wana sababu zao za kisiasa.

Kuhusu hiyo riba siwezi kukubaliana na wewe. Mtu ukikopa unapewa na masharti kisha una piga sahihi. Ukisha weka wino kwenye karatasi basi inamaanisha ume kubali masharti. Kama masharti yalikua magumu kwa nini akubali? Yeye kapata walicho kubaliana basi na yeye awape walicho kubaliana simple as that. Hauwezi kusign kitu kisha baadae useme masharti magumu, ingekua hivyo basi kunge kua hamna maana ya mikataba.

Ukweli ni kwamba kama kweli ana daiwa kiasi hicho ni sharti alipe. Alikubali mkataba basi ana takiwa kuheshimu makubaliano.

A very good observation. Takriban magazeti mengi ya Tanzania huandika kwa kuweka vichwa vya habari ambavyo havibebi uzito wakutosha kwa story husika. Mara nyingi hii hutokea kwa makusudi kwa kile wengi wanachosema 'message sent' baadae wakijua kama kutakuwa na malalamiko basi wataomba omba radhi, lakini mara nyingi ni makusudi.

Pili, umebainisha kitu muhimu sana ambacho katika jamii zetu watu wengi wanapenda kuchukua excuse. Baadhi ya ndugu na jamaa zetu hufanya mambo wakiwa na akili timamu lakini baadae hutoa visingizio ambavyo katika real world hatuwezi kujichanganya. Endapo umeamua kufanya jambo basi ni vema ukawajibika kwa maamuzi na matendo yako na si vinginevyo. Kama uliamua kwenda kukopa basi ni wazi kuwa ulielewa masharti na makubaliano ambayo yalikupatia mkopo huo, vinginevyo inaonekana ni ubabaishaji.
Kusema kweli, jinsi tunavyoendesha mambo yetu hapa nyumbani, the serious people wanafuatilia wakati wote na kupima jinsi tunavyofanya mambo. Leo kama tunakuwa na ubabaishaji katika private sector ni wazi tunachimba shimo kubwa la kufukia maendeleo ya nchi hii. Private sector ndiyo inatakiwa kuwa makini kwa maana ya kulinda interest za uchumi wa nchi pamoja na kuukuza. Hatuwezi kuvutia wawekezaji wa nje katika sector ya fedha ikiwa wana taarifa zinazofanana na hizi ambazo kwao wao it's a high risk factor. Aidha, vyombo ambavyo tayari vimeshawekeza katika sector ya fedha hapa Tanzania kama vile mabenki vinaweka riba na masharti magumu kwa baadhi ya wakopaji wa kitanzania kwa kuzingatia risk factor. Wakati huo huo kuwapa masharti ya kawaida na riba nafuu wakopaji ambao kiwango chao cha risk kiko chini.
Hili jambo si la kisiasa hata kidogo japo kuna Mbunge mmoja ambaye alikuwa mkurugenzi katika bodi ya NBC aliliona kuwa ni la kisiasa, matokeo yake wakamfungulia mlango na kumwambia unaweza ukatoka.
Ni wakati muafaka tuangalie nini tunakipa kipaumbele kujenga misingi bora ya kuifanya hii nchi iwe mahala pazuri kwa mtoto aliyezaliwa leo au kuendelea kufanya mambo nje ya utaratibu ili hao watoto waje wajitafutie yao kivyao-vyao?
Let's critically think about this!!
 
Ndio maana kuna post moja nimesema umefika wakati watanzania tukajua jinsi ya kupata pesa za bure, hapa Mbowe anaweza kuvuta kutoka CCM kwa kuwambia

Please don't go to personality. The issue here is not Freeman Mbowe, it is Mbowe Hotels Ltd. Kwa sheria zetu hili deni lina mipaka kwa vile Mbowe Hotels Ltd is limited liability company. Tusitake kuingiza jina lake katika hili kwani Mbowe Hotels Ltd inaweza kushitaki na kushitakiwa kama entity. Let's be fair.
 
hizo number nina wasiwasi nazo kama zina ukweli wowote,nina uhakika huyo mwandishi ni kilaza na hana idea anaandika nini...unakopa 12m in 2003 unaishia na deni la 5billion 2009? hakuna kitu kama hicho hata kama interest ni 100%...hawa inabidi wasome kabla ya kuandika upupu wao!

Mkuu Koba,
Wewe ni mmoja katika ya wachangiaji mahiri katika forum hii. Ni kweli unaposoma taarifa iliyowekwa hapa hupati picha halisi au ni jinsi gani hilo limefikia katika kiwango hicho kikubwa. Sasa, ilikuondoka katika kufanya conclusion based on single source of information, tungeomba yeyote, kati ya wale ambao walikuwepo katika mkutano huo na CAG watuwekee ripoti hiyo na kuweza kuona chanzo kinasemaje. Hii itasaidia kupata kujua ukweli ni upi. Endpao report ya CAG itaonesha hivyo basi CAG anaweza kutueleza hizi hesabu za riba zimefanyika kwa namna gani.
Nadhani kwa kufanya hivyo tutakuwa tumeiweka JF mahala pazuri pa kutimiza malengo yake.
Natoa wito kwa yeyote aliyekuwepo katika mkutano na CAG ana anayo report ile atuwekee ili tuweze kuona mambo katika 3D.
 
Please don't go to personality. The issue here is not Freeman Mbowe, it is Mbowe Hotels Ltd. Kwa sheria zetu hili deni lina mipaka kwa vile Mbowe Hotels Ltd is limited liability company. Tusitake kuingiza jina lake katika hili kwani Mbowe Hotels Ltd inaweza kushitaki na kushitakiwa kama entity. Let's be fair.

That is true. tusichanganye kampuni na mtu binafsi kwa maana hiyo Mbowe Hotel LTD inaweza kuwa na shareholders wengine zaidi ya huyo Mbowe hata kama jina lake ndiyo lipo kwenye kampuni. Huu si mkopo binafsi bali ni kampuni imekopeshwa. It is likely Mbowe ana husika after all it is his company or a majority shareholder at least but ina wezekana maamuzi yote siyo yake peke yake. Could be yuko kwenye ubia na wengine wakaamua kukopa ikawa ishu lakini kwa vile jina lake lipo pale na yeye ni public figure basi ndiyo maana ana chukua moto wote. Lets not be to personal in our judgements, swala ni MBOWE HOTELS LTD THE COMPANY SIYO MBOWE THE PERSON.
NOT TO SAY THAT MR. MBOWE IS INNOCENT OR NOT, I'M NOT THE ONE TO SAY BUT IJULIKANE MDAIWA NI KAMPUNI SIYO MTU BINAFSI
 
Making judgement after hearing one side only is biased & unfair. Hata mahakamani husikilizwa pande zote mbili. Although i say yes the company should pay because whether the interest is too high or not ni walikubali wenyewe na wakaona wanaweza but i think we should also try to find out why they haven't made payments in the first place. Its possible hawana kisingizio cha kuto kulipa but just to be unbiased we should hear the other side of the strory & look at botth sides of the shillings.
 
Making judgement after hearing one side only is biased & unfair. Hata mahakamani husikilizwa pande zote mbili. Although i say yes the company should pay because whether the interest is too high or not ni walikubali wenyewe na wakaona wanaweza but i think we should also try to find out why they haven't made payments in the first place. Its possible hawana kisingizio cha kuto kulipa but just to be unbiased we should hear the other side of the strory & look at botth sides of the shillings.

Ukiangalia hii stori nzima ya gazeti la UHURU ni biased na imeandikwa kiitikadi zaidi ya kitaalamu. Practically, mtu akikopa kuna kuwa na makubaliano ya jinsi ya kulipa lakini ukiona upande mmoja unaamua kwenda kivyake vyake kwa maagizo ya wanasiasa basi hapo kuna walakini. Hizi ni mbinu za kuelekea kufilisi watu, leo hii tukiangalia katika daftari halisi la NSSF utakuta wanasiasa wengi wanadaiwa na hasa wale wa CCM ila kwa kuwa wao ni wenye nchi wanalindana.

How come in 19 years 7m izalishe interest ya 230M that isn't practical unless "kuna upishi wa data", Ina maana katika miaka hiyo yote inaonesha kuwa Mbowe Hotel iliisha default siku nyingi na kwa nini hawakukamata mali kipindi kile? kwa nini wanaacha active accounts?, It's finacially impracticle kwa interest hiyo

Na hao UHURU waache siasa kwenye uandishi siku wakikosa Ruzuku za kendeshea gazeti lao utakuwa ndiyo mwisho wao. Mtu makini akinunua gazeti lenye kichwa kama hiki halafu akute kilichoandikwa next time hata fikiria kununua tena upuuzi.
 
Hiyo hoteli watakuwa na wazimu kulipa deni riba ya 223 milioni kutoka deni la milioni sijui 7! As a matter of fact, I would have sued NSSF kwa kuvunja katiba!
 
Hiyo hoteli watakuwa na wazimu kulipa deni riba ya 223 milioni kutoka deni la milioni sijui 7! As a matter of fact, I would have sued NSSF kwa kuvunja katiba!

I agree with you mwanakijiji but kama hiyo riba ipo kwenye mkataba then hoteli haina kesi. Hapa mkombozi wa matatizo yote haya ni nini kilichopo ndani ya mkataba. The only case the hotel has ni kama NSSF wamevunja makubaliano ya mkataba otherwise......Hapo kilicho baki ni huo mkataba kati yao uangaliwe mwenye makosa awajibike whether its one of them or both the parties involved. Tatizo nchi yetu ni sheria na mikataba. Sheria na mikataba ikifuatwa matatizo yote haya yange kwepeka.
 
I agree with you mwanakijiji but kama hiyo riba ipo kwenye mkataba then hoteli haina kesi. Hapa mkombozi wa matatizo yote haya ni nini kilichopo ndani ya mkataba. The only case the hotel has ni kama NSSF wamevunja makubaliano ya mkataba otherwise......Hapo kilicho baki ni huo mkataba kati yao uangaliwe mwenye makosa awajibike whether its one of them or both the parties involved. Tatizo nchi yetu ni sheria na mikataba. Sheria na mikataba ikifuatwa matatizo yote haya yange kwepekwa.

It's a good point.
kitu muhimu hapo ni kurudi kwenye mkataba na kuangalia makubaliano yalikuwa ni yapi. Suala la kusema kuwa Hotel isilipe ni unethical haiendena na best practices za kibiashara. Pia kitu kingine cha kuangalia hapa ni kwani principal imeachwa kulipwa kwa kipindi kirefu cha miaka 19? nadhani hivi ni vitu muhimu pia kujiuliza na kupata clues kama vile ambavyo tunajaribu kuangalia calculations za riba zimekwendaje?
 
I agree with you mwanakijiji but kama hiyo riba ipo kwenye mkataba then hoteli haina kesi. Hapa mkombozi wa matatizo yote haya ni nini kilichopo ndani ya mkataba. The only case the hotel has ni kama NSSF wamevunja makubaliano ya mkataba otherwise......Hapo kilicho baki ni huo mkataba kati yao uangaliwe mwenye makosa awajibike whether its one of them or both the parties involved. Tatizo nchi yetu ni sheria na mikataba. Sheria na mikataba ikifuatwa matatizo yote haya yange kwepeka.

Ndiyo hivyo, hata mkataba ukiwa na vipengele ambavyo kimsingi ni vya kukandamiza, mahakama inawezakutupilia mbali. Huwezi kuandika mkataba wa kuhakikisha unapata riba ya kiasi gani sijui! Huu upuuuzi. Yaani, mimi leo ninunue gari kwa dola 9000 halafu ni default na baada ya miaka 19 tu riba ifikiee lakini 230,000!? Majaji wa hapa mbona wanaweza kuwa na field day.

Nilinunua gari zamani (kama 20,000 USD) baada ya kukaa nalo like for 5 years malipo yakawa magumu nikawapigia waje walichukue gari lao nikaanda kununua used car for abt 3000; jamaa wakanitumia deni langu ati natakiwa kulipa karibu 12,000, nikawazungusha mahakamani hadi mwisho wakakubali kusettle for 1500!

Shoot, I ain't paying 229 millioni kwa deni la 9 millioni!

sasa ninaelewa kwanini GT ameng'ang'ania walipe deni; dawa ya deni ni kulipa!?
 

Pia kitu kingine cha kuangalia hapa ni kwani principal imeachwa kulipwa kwa kipindi kirefu cha miaka 19? nadhani hivi ni vitu muhimu pia kujiuliza na kupata clues kama vile ambavyo tunajaribu kuangalia calculations za riba zimekwendaje?

Principal ilishalipwa mbona muda mrefu tu.. wanachogombana mahakamani ni hiyo riba.
 
Philemon Michael yu wapi in the wake of all this? Nadhani input yake inahitajika humu jama
 
Making judgement after hearing one side only is biased & unfair. Hata mahakamani husikilizwa pande zote mbili. Although i say yes the company should pay because whether the interest is too high or not ni walikubali wenyewe na wakaona wanaweza but i think we should also try to find out why they haven't made payments in the first place. Its possible hawana kisingizio cha kuto kulipa but just to be unbiased we should hear the other side of the strory & look at botth sides of the shillings.
Great minds think alike
 
Hehehehe,

Kwanza niungane na wengine kusema Mbowe hakutendewa haki kwenye kichwa hiki cha habari.

Pili kuhusu, interest no doubt ni sahihi kabisa 230m. Kwa kawaida bank zote ukilaza interest inakuwa principle so mwezi unaofuatia nayo inachargiwa interest ... mwaka hadi mwaka.

Hivyo ukifanya assumption kwamba Mbowe Hotel haikulipa hata shillingi moja baada ya kuchukua mkopo, na mkopo ulikua unachargiwa interest 20% p.a then kwa miaka 19 atakuwa anadaiwa Ths 239,610,000 hivyo kama kuna wakati walinegotiate interest aama alilipa 10m then utaishia na hiyo 229m. Hivyo hiyo habari inaweza kuwa sahihi (for detail analysis see the attached file)
 

Attachments

Principal ilishalipwa mbona muda mrefu tu.. wanachogombana mahakamani ni hiyo riba.

That's perfect.

Njia nzuri ni ku-argue mbele ya sheria kwa maana mahakama. Nina hakika sheria itajadiliwa na uamuzi kupatikana. hii ndiyo njia nzuri ya kuimarisha utawala bora kwani matokeo ya kesi hiyo yatasaidia sana kutatua matatizo mengine mbalimbali. Kwa mfano ruling ikiwa against NSSF basi wengi wanaodaiwa wanaweza kuamuliwa mashauri yao kufuatana na hukumu hiyo. Vilevile, endapo shauri litaamuliwa in favor of NSSF basi pia itaisaidia NSSF kurecover madeni yake mengi ya muda mrefu.
 
Siasa za bongo zinawadanganya wananchi. Ni kweli Mbowe hotel ilikopa mil hizo 7.5. Mbowe hotel ilisha lipa principal amount yote shida ni hiyo riba. Hiyo kampuni ya Kagera Sugar ilikopa 12 billion sio (12 million) na haijalipa chochote. Ikumbukwe hiyo kampuni ilikopa jumla ya Tshs. 72 billion (syndicate loan) wakopeshaji wakiwa ni pamoja na NSSF, CRDB Bank, Barclays Bank, Stanbic Bank, PSPF, etc. Kama mtakumbuka siasa zilijaribu kuingilia swala hili zikiongozwa na Lowasa lakini hii kampuni haikulipa deni na sijui ni vigezo gani vilitumika kutoifilisi or receivership. Hivyo tuwe realistic tusiwe kama wanasiasa na sisi tuchambue vizuri
 
Siasa za bongo zinawadanganya wananchi. Ni kweli Mbowe hotel ilikopa mil hizo 7.5. Mbowe hotel ilisha lipa principal amount yote shida ni hiyo riba. Hiyo kampuni ya Kagera Sugar ilikopa 12 billion sio (12 million) na haijalipa chochote. Ikumbukwe hiyo kampuni ilikopa jumla ya Tshs. 72 billion (syndicate loan) wakopeshaji wakiwa ni pamoja na NSSF, CRDB Bank, Barclays Bank, Stanbic Bank, PSPF, etc. Kama mtakumbuka siasa zilijaribu kuingilia swala hili zikiongozwa na Lowasa lakini hii kampuni haikulipa deni na sijui ni vigezo gani vilitumika kutoifilisi or receivership. Hivyo tuwe realistic tusiwe kama wanasiasa na sisi tuchambue vizuri

Mkuu naomba utusaidie kama unazo detail:

Alilipa lini hiyo principle??? Je wakati analipa hiyo principle kulikuwa na any cummulative interest? If yes ni kiasi gani?

Note: Bank zote bongo any Accrued interest kwa first period inakuwa principle period inayofuatia. Kwa maana ingine kama ulipaswa kulipa instalment moja kwa mwaka (yaani all interest + part ya principle) then usipolipa interest yote mwaka unaofuatia inakuwa principle, (hii ndio wanaita Compound interest).

Ukiweza kutupa hizo figure mkuu tutatatua hicho kitendawili cha interest mkuu
 
Mengi anaweza kumsaidia kulipa hili deni

nadhani mnajua Mbowe hapendi kuonekana kama anadaiwa hivyo mwenyewe akija ingia humu baadae atauwasha huu moto mpaka basi

hii thread bora iendelee kisha mtajua huyu Freeman ni mtu wa namna gani...na nadhani mnajua kule mahakamani alifanya nini ili hii kesi iishe

nadhani mna close contacts nae hivyo muulizeni alifanya nini alipokaliwa kooni kuhusu hili deni?
 
Making judgement after hearing one side only is biased & unfair. Hata mahakamani husikilizwa pande zote mbili. Although i say yes the company should pay because whether the interest is too high or not ni walikubali wenyewe na wakaona wanaweza but i think we should also try to find out why they haven't made payments in the first place. Its possible hawana kisingizio cha kuto kulipa but just to be unbiased we should hear the other side of the strory & look at botth sides of the shillings.

mwanafalsafa hili la deni la mbowe hotel na NSSF siyo geni na upande wa pili umeshatolewa mara kadhaa..

Mbowe ajitetea kuhusu ufisadi Tuesday, 18 March 2008 Mwandishi Wa Habari Leo

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe, amesema anaamini habari za yeye kudaiwa mamilioni na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) na amri ya kukamatwa kwake, zinakuzwa na wapinzani wake katika siasa aonekane fisadi na apunguze kasi ya kutaka kuchukuliwa hatua kwa waliozoa mabilioni Benki Kuu (BoT) kupitia Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA).
Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mbowe alikiri kuwa kampuni yake ya Mbowe Hotels Ltd ilikopa Sh milioni 15 kutoka NSSF mwanzoni mwa miaka ya 1990, lakini ameshindwa kumalizia kulipa mkopo huo kutokana na utata uliopo kwenye riba, licha ya kuwapo kwa amri ya Mahakama Kuu tangu mwaka 2004 ya kutaka akamatwe kwa kushindwa kulipa.
“Habari hizi zinazojaribu kunipaka matope leo hii zikigeuza kesi ya Mbowe Hotels ambayo kimsingi ni ya biashara ili ichukue sura ya siasa na ufisadi…zinalenga kuniharibia heshima yangu kwa jamii na kunichonganisha na wanachama wa Mfuko (NSSF),” alisema Mbowe huku akitamba kwamba ataendelea kupigania haki.
Alisema kutokana na vuta nikuvute hiyo ya deni la NSSF, mkewe, Dk. Lillian Mbowe, alikamatwa mwaka jana na kupelekwa Mahakama Kuu mbele ya aliyekuwa Jaji Kiongozi Amiri Manento, ajieleze kwa nini asifungwe kwa kushindwa kuheshimu amri ya kulipa deni.
Wakati huo Freeman alikuwa masomoni Uingereza. Habari za mkopo unaolalamikiwa na Mbowe na riba juu yake ziliripotiwa kwa mara ya kwanza magazetini wiki iliyopita, huku ikielezwa kuwa deni hilo limefikia Sh bilioni 1,200 na kwamba Mahakama Kuu imetoa amri ya kukamatwa kwa wakurugenzi wa Mbowe Hotels.
Akijitetea jana, Mbowe alisema kampuni yake ilipewa mkopo huo kwa ajili ya upanuzi na uboreshaji wa hoteli yake Dar es Salaam na wakati anakopa riba iliyokuwa inatolewa na NSSF, ilikuwa asilimia 31 na hadi kufikia Juni mwaka jana, kampuni yake ilikwisha kulipa Sh milioni 75.5, kiasi ambacho alisema ni mara tano ya kiwango kilichokopwa.
Alisema ugomvi wake na NSSF ni riba, kwani kampuni yake imekuwa inaiandikia NSSF ipitie upya mkataba wa mkopo huo, jambo alilodai ni la kawaida kwa kila taasisi ya fedha inayojua wajibu wake na yenye nia njema kwa wateja wake. “Mchanganuo wa kitaalamu wa deni la sasa la Mbowe Hotels Ltd pamoja na riba ni Sh milioni 43.2.
Hili mimi ndilo ninalojua kwamba bado wanatudai na tumekuwa tunawaomba tukae nao turejee mkataba juu ya mchanganuo huu, lakini hawataki,” alisema. Alisema kama mfanyabiashara, amekuwa anakopa katika benki mbalimbali kwa ajili ya uwekezaji katika miradi mbalimbali na amekuwa analipa bila matatizo.
“Iweje hawa NSSF wagome kufanya hivyo…na wao ndiyo wamekuwa chanzo cha kuchelewesha kulipwa kwa deni hilo, kwani hawataki kukaa na sisi kurejea mkataba huo,” alisema Mbowe anayemiliki baadhi ya biashara nchini, zikiwamo za hoteli. Mbowe alisema mkataba na NSSF ulioingiwa mwaka 1990 uligubikwa na mizengwe mwaka mmoja tu tangu kuingiwa.
Alisema kampuni yake iliomba kuongezewa mkopo kukamilisha mradi uliokusudiwa, lakini ilichukua mwaka mmoja kutoa jibu la kukataa kwa madai kuwa kutoa fedha za ziada siyo sera yao. Mfanyabiashara huyo alisema baada ya kukataliwa alianza upya mchakato wa kutafuta mkopo na akaenda benki ya CRDB ikakubali kumkopesha.
“Wakati hali hii ikiendelea, NSSF ilianza kudai marejesho ya riba kwa mkopo waliotoa kwa mradi walioufadhili na kuutekeleza.” Alisema mwaka 1996 ukiwa mwaka mmoja baada ya Uchaguzi Mkuu wa kwanza wa mfumo wa vyama vingi ambao alishiriki kama mgombea wa upinzani katika Jimbo la Hai, wadhamini wa NSSF walifungua kesi ya madai katika Mahakama Kuu wakidai malipo ya Sh milioni 80.1 ikijumuisha salio la deni mama la Sh milioni 12 na riba ya Sh milioni 68.1.
Alisema tangu mwaka 2003 walikubaliana na NSSF wakae wazungumze, lakini baadaye shirika hilo likawa kimya. Alisema mwaka jana, kampuni yake iliiandikia tena NSSF kuomba wakubali mapendekezo ya kumaliza deni hilo na barua nyingine; lakini hawajajibu barua hizo hadi leo, ikiwa ni miezi minane tangu waandikiwe barua hizo.
Juhudi za kuwapata maofisa wa NSSF kuzungumzia suala hilo hadi jana jioni hazikufanikiwa. Mbowe alisema anaamini baadhi ya watu wanavitumia vyombo vya habari kumchafua yeye ili Watanzania wageuzie mawazo yao kwenye habari zake na NSSF na wasahau habari za ufisadi wa EPA na Richmond zinazowagusa baadhi ya viongozi.

Habari hiyo hiyo iliripotiwa hivi na IPP

Wananizulia kufifisha vita dhidi ya ufisadi - Mbowe

2008-03-18 10:18:16
Na Mashaka Mgeta

Mkurugenzi wa Kampuni ya Mbowe Hotels Limited, Bw. Freeman Mbowe, amesema tuhuma zinazomkabili kuhusu kinachoitwa `hujuma` dhidi ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), zina lengo la kufifisha vita dhidi ya ufisadi nchini.

Bw. Mbowe, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), aliyasema hayo akiwa na Mkurugenzi Mwenza wa kampuni hiyo, Dk. Lilian Mbowe, ambaye ni mke wake, walipozungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

Wiki iliyopita, baadhi ya vyombo vya habari, viliripoti kuhusu kampuni hiyo kukopa Sh. bilioni 1.2 za NSSF, lakini Bw. Mbowe, alisema deni halisi lilikuwa Sh milioni 15 zilizokopwa mwaka 1990.

Alisema fedha hizo zilikopwa wakati huo NSSF ikijulikana kama Mfuko wa Taifa wa Pensheni (NPF), kwa makubaliano ya kulipa riba ya asilimia 31, ili itumike katika mradi wa kupanua na uboreshaji wa hoteli yake jijini hapa.

Bw. Mbowe, alisema mwaka mmoja baada ya mkopo huo kusainiwa, hali ya kutoelewana ilijitokeza kati ya pande mbili hizo, baada ya kampuni yake kuomba ongezeko la mkopo ili kukamilisha mradi wake.

Alisema ombi hilo lilikubaliwa, lakini NSSF ilitumia kigezo cha sera zake kutoruhusu ongezeko la mkopo na kuishauri (kampuni ya Mbowe), kukopa katika taasisi nyingine ya fedha.

Bw. Mbowe, alisema ilibidi kampuni yake kukopa fedha katika Benki ya CRDB, ikiwa ni kiasi kikubwa kuliko kilichokopwa NSSF.

``Ni dhahiri kuwa mradi huu uliathiriwa kwa kiasi kikubwa, na ninaamini umakini na utaalamu wa kibenki haukutumika katika maamuzi haya� Inanilazimu kuhoji uwezo wa kitaaluma wa Mfuko kujishughulisha na biashara za ukopeshaji,`` alisema.

Bw. Mbowe, alikiri kuwapo kesi namba 277 iliyofunguliwa Septemba, 1996 na Bodi ya NSSF dhidi ya kampuni yake, ikidai malipo ya Sh. milioni 80.1, ikiwa ni jumla ya salio la deni mama la Sh. milioni 12 na riba ya Sh. milioni 68.1.

Alisema ombi hilo lilikubaliwa na Mahakama Kuu bila upande wa walalamikiwa ama wakili wao, kuwapo mahakamani hapo.

Bw. Mbowe, alisema hadi kufikia Juni 30, mwaka jana, kampuni yake ilishalipa Sh. milioni 75.5 na kwa mujibu wa mchanganuo wa kitaalamu, deni la sasa linapaswa kuwa Sh. 43,169,727.

Hata hivyo, alisema kampuni yake iliwasilisha ombi namba 151 na 152 la mwaka juzi, kutaka amri ya kukamatwa kwa Wakurugenzi wake (akiwamo Mbowe) isitekelezwe, na Mahakama ya Rufaa ilikubali.

Bw. Mbowe, alisema kesi ya kusikiliza dai la kampuni yake, kuhusu shauri la msingi kuwa na hukumu mbili, itasikilizwa Aprili 29, mwaka huu, Mahakama Kuu.

Hivyo, Bw. Mbowe, alisema taarifa zinazomhusisha na ufisadi katika NSSF, zina lengo la kuipotosha jamii, na kuondoa fikra za umma kutoka kwa watu waliohujumu uchumi na mali za umma, kwenda kwa `Mbowe na NSSF`.

Kwenye mkutano huo, Bw. Mbowe alifuatana pia na wabunge Bw. Chacha Wangwe (Tarime), Bw. Kabwe Zito (Kigoma Kaskazini), Bw. Said Arfi (Mpanda Kaskazini) na Mkurugenzi wa Vijana wa CHADEMA, Bw. John Mnyika.
 
Back
Top Bottom