Madela wa Madilu,
Mkuu wangu kuhusiana na riba wala tusitake kuitazama kwa vigezo mnavyotoa kwani yawezekana kabisa miaka 19 ya mkopo ikafika kiwango hicho maadam tufahamu ni asilimia ngapi ya riba huweka kwa kila mwezi..
Nitakupa mfano mdogo sana jinsi riba inavyojiongeza.. Ukiwa Umekopa Tsh.100 na riba ni asilimia 20 unatakiwa kulipa 120 by the end of the month mara nyingi wenye riba wanakuandikia unatakiwa kulipa Tsh. 20, pamoja na service charge na kadhalika tuseme Total Tsh 30..
Usipolipa mwezi wa kwanza, mwezi unaofuata deni linaseama (Previous Balance) unadaiwa 130 na riba yake ni asilimia ile ile 20 ya amount hiyo Tsh.130,..hivyo utatakiwa kulipa Tsh 26 kama riba plus services na late fees na kadhalika, Total amount ya deni linaweza kuwa Tsh. 160 mwezi wa pili tu.. Hivyo hivyo ukiendelea kutolipa deni linakuwa ni pamoja na riba unayodaiwa kila mwezi kuongezwa ktk principal, services pamoja na fine zake pia zinaweza kuwa in %..Kwa mwaka mzima deni hilo linaweza kabisa fikia 1,000.. mara tisa ya mkopo uliotolewa..
Mimi kinachonipa shida kuelewa ni sababu zipi zilizoifanya Mbowe Hotels na wadaiwa wengine wasilipe deni hilo hata iwe kiwango kidogo cha ile riba inayotakiwa kila mwezi kuhakikisha deni halipandi zaidi ya mkopo wenyewe..Na kati yetu hatuelewi riba ilikuwa kiasi gani ktk mikopo na navyojua Ukopeshaji wa Bongo inaweza kabisa kuwa ni asilimia 30 au zaidi..
Pili, sielewi kwa nini NSSF walisubiri hadi miaka 19 - Jamani 19yrs!.. ipite hivi hivi wakiandikiana barua na wakopeshwaji wakati sii jambo la kawaida kabisa na matokeo yake wanapelekana mahakamani kama vile huu ni upatu!..Hapa ndipo napoona kwamba tatizo sio Mbowe Hotels ama wadaiwa wengine isipokuwa ni uongozi wa NSSF na nina hakika kabisa yapo mashirika mengi, pengine hata majina ya watu binafsi waliokopeshwa fedha hizo na hazijarudishwa..Mbowe ni Banmgusilo tu anayetumiwa kisiasa kwani hata mtoto mdogo anaweza kuona kinachofanyika hapa.
Kisha kwa wale wanaotaka kujua kwa nini NSSF inakopesha watu nafikiri hapa tutakuwa tunapotosha. NSSF haikumkopesha Mbowe bali imekopesha shirika la Mbowe Hotels na mashirika mengine ikiwa ni non risk ninvestment inayotegemea riba..
Kwa vyovyote vile fedha zinategemewa kurudi na wametengeneza faida ambayo inaendesha shirika zima badala ya kutegemea bajeti ya serikali kulipia matumizi ya shirika ambalo linatakiwa kujiendesha..