Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Kama unadaiwa ulipe ni hela za wafanyakazi wanaokatwa kodi zao kwenye mishahara kila mwezi. Uwe msafi wewe kwanza , kushindwa kutimiza masharti ya mkopo ni ufisadi kwani hizo peasa wengine wanahitaji kuzitumia si MBOWE tu.
 
kweli wahandishi wetu wa habari inabidi warudi shule ya msingi ( primary school).

Hivi tanzania wahandishi wanaspecialise?
 
yap

ukidaiwa ni vizur kulipa. tena ukiweza kulipa ontime the better
nssf wana vihela vyangu wanavikata kila mwez

lakin ni vigumu kuwa mfanyabiashara halaf ukafanikiwa sana kukaa mbali na kukopa. mbowe na familia yake nimeambiwa ni wafanyabiashara wa miaka na miaka. nssf na mabenk yanapata faida kwa kukopesha
 
Kama unadaiwa ulipe ni hela za wafanyakazi wanaokatwa kodi zao kwenye mishahara kila mwezi. Uwe msafi wewe kwanza , kushindwa kutimiza masharti ya mkopo ni ufisadi kwani hizo peasa wengine wanahitaji kuzitumia si MBOWE tu.

walipe kiasi gani Bilioni 58, milioni 230 au milioni 7?
 
Hivi kwanza niliuze swali moja....
Hii NSSF inafanya baishara ama ni shirika la kutoa huduma kwa wananchi kuwa bail out?..maanake nashindwa kuelewa inakuwaje shirika kama hili linaendeshwa huku likidai watu kiasi hicho cha fedha na kwa miaka kibao haijalipwa na hakuna final due date ya malipo..Action should have been taken kulingana na mkataba, sidhani kama kuna mkataba wowote wa hizi financial institution huwa wazi kiasi hicho..

I mean shirika kama hili likifrisika kweli bado tutalaumu uongozi wa Kikwete ati shirika limefirisika kwa sababu ya siasa zake?.. Sijawahi kuona maishani shirika la kutoa mikopo linalimbkiza madeni kufikia kiasi hicho na bado halijakamata mali zilizowekwa rehani..Na wala siwezi kuwalaumu wamiliki wa Mbowe au Mashirika mengine yaliyokopa isipokuwa shirika hili linalokopesha..

Hawa wakopeshaji wote wanafanya wanayoyafanya kwa sababu shirika hili limekosa uongozi bora na kusema kweli linapotangaza madeni yake kwa mashirika haya ni AIBU kwa utawala wa shirika hili kuona kwamba linaendeshwa kienyeji sana...
 
Swala jingine ni kwamba NSSF sio bank na sidhani kuwa ina-qualify kuitwa 'financial institution' (wataalamu mnisahihishe kwenye hili kama siko sahihi). Hivyo sidhani kama kwa nature ya shirika linatakiwa kuwa linatoa mikopo ya ki-bank ama ki-biashara. As a long shot, I could understand labda empowering schemes za members wake! Sasa nashindwa kuelewa watu (e.g. Mh. Sumaye) wanaokopa ama biashara zinazokopa NSSF huwa inakuwa on what grounds.

From what I could see kwenye NSSF Act (1997), "62. Investment of money shall be done by the Board in any viable venture as it may consider appropriate having regard to the economic and commercial viability." ama huko kukopesha ndio investment?

Pia on the same Act nasoma kuwa
"66. The funds and resources of the Board shall consist of-, Resources
(a) any income from investments of the Fund approved under this
Act.
(b) such sums as may be provided for by way of loan or grant for the purposes of the Board;
(c) any sums borrowed by the Board in accordance with the provisions of this Act;
(d) any sums which may in any manner become payable to or vested in the Board as a result of the performance by the Board of its functions under this Act or any other written law."
from section 'b' natafsiri kuwa NSSF inaweza kukopa kama resource ama fund avenue mojawapo, na board iko empowered kufanya hivyo kwenye section "68. The Board may, borrow moneys for the purposes of the Board by way of loan or overdraft, and upon such security and such terms relating to the repayment of the principal and the payment of interest as the Board may deem fit."

Sijaona mahali ikitajwa kuwa NSSF inaweza kutoa loans kibiashara (yaani ili faida iwe ni interest) kama ambavyo financial institutions zinaweza kufanya. So, if anyone has a better understanding naomba kueleweshwa NSSF inatoa mikopo kwa misingi ipi?
 
Kama 'Dr' Masau alivyokuwa anadaiwa...dawa ya deni Mbowe alipe tuuu

Mbona unang'ang'ana na Mbowe tu je hao wengine sio wadeni? Na je hujui kuwa mbowe japo anadaiwa hicho kiasi kuna kesi mahakamani ya deni hilo hilo?
 
Wanachama wa JF wakati mwingine tu wajabu sana.

Juzi ripoti imetaja double insurance katika twin towers, ilikua hatari hapa.

Leo Katajwa Fisadi Yosso Mbowe,anaelekezwa mpaka jinsi ya kujibu ili asilipe deni

Kweli tutafika jamani?

Issue ni kweli anatakiwa kulipa deni hilo lote? Maana hata riba zina viwango siyo kuwa unajiwekea tu eti kwa kuwa ni makubaliano!! Mbona mama anna mkapa aliyekuwa anawalipisha walimu riba kubwa alirekebisha baada ya walimu kulalamika.

Hutakiwa kuwa mtumwa eti kwa kuwa ni mkataba basi ulipe tu lazima uhakikishe na ikigundulika kuna walakini lazima marekebisho yafanyike. Siyo swala la kulipa tu...
 
Mimi nafikiri tumeona tatizo lililopo katika heading ya gazeti na vilevile baadhi ya wachangiaji wengine kumwongelea Freeman Mbowe katika personal capacity badala ya Mbowe Hotels Ltd. Kwa hayo mawili hayana ubishi kuwa ni makosa kwa gazeti kwa heading na ni makosa kwa wachangiaji katika kumjadili Freeman Mbowe.

Sasa, kwa vile majadiliano huchukua sura tofauti kadri yanavyokwenda inafika wakati inabidi tujiulize yale ambayo ni facts,
Je, Mbowe Hotels Ltd ilikopa Shs 7.5m kutoka NSSF
Jibu hapa ni ndiyo
Je, deni hilo lilikopwa lini?
Miaka 19 iliyopita (labda hata wengine hawajazaliwa)
Je, deni hilo lilipwa?
Hapa inaonekana deni hilo lilipwa sehemu tu na bado wanadaiwa kiasi kingine cha Shs. 229m ambacho kimetokana na riba iliyosababishwa na Mbowe Hotels Ltd kutokulipa deni hilo kwa kipindi cha muda mrefu.
Je, madai ya NSSF yako nje ya mkataba?
Hapa tulitegemea Mbowe Hotels Ltd ieleze kuwa hawezi kulipa kwa sababu madai ya NSSF yapo nje ya makubaliano.

Nimejaribu kuweka assumptions ili ziweze kutufanya wachangiaji tuangalie na kuzingatia the best practice ya kufanya biashara. Endapo umeamua kufanya biashara ni wazi kuwa at certain time unaweza kukopa kwa ajili ya ku-finance biashara yako. Na unapoamua kukopa tayari unatakiwa unapoingia kwenye makubaliano ujue ni nini haki yako kama mkopaji na ni upi wajibu wako vilevile kama mkopaji.
Ni mategemeo yangu kuwa Mbowe Hotels Ltd inaelewa haki zake kwenye ule mkataba na wajibu pia. Moja kati ya haki za Mbowe Hotels Ltd ni kuona kuwa inapatiwa mkopo ule kwa masharti waliyokubaliana na wajibu wa Mbowe Hotels Ltd ni kulipa deni hilo katika kipindi walichoingia makubaliano.
Endapo deni halitalipwa kwa mujibu wa makubaliano basi NSSF wanahaki ya ku-exercise yale yaliyomo katika makubaliano.
Ninavyofahamu, commonly, parties kwenye makubaliano kama hayo zikishindwa kuafikiana basi hufikishana katika court of law huko ndiko maamuzi ya mwisho hupatikana. Na ninafikiri kesi iko mahakamani lakini sijui imefikia wapi.
 
Pundamilia, si kama unavyosema kuna kesi Mahakamani unajua inahusu nini? Maana unazungumza kana kwamba hakuna kezi zilizoko mahakamani. Kwanini tusisubiri mahakama iamue au tunataka Mbowe ilipe ili yaishe tu na ifute kesi yake mahakamani ili turidhike?

Nilidhani unatetea utawala wa sheria ambapo Mbowe Hotel imekimbilia ulinzi wake.

Mahakama ya nini basi?
 
Pundamilia, si kama unavyosema kuna kesi Mahakamani unajua inahusu nini? Maana unazungumza kana kwamba hakuna kezi zilizoko mahakamani. Kwanini tusisubiri mahakama iamue au tunataka Mbowe ilipe ili yaishe tu na ifute kesi yake mahakamani ili turidhike?

Nilidhani unatetea utawala wa sheria ambapo Mbowe Hotel imekimbilia ulinzi wake.

Mahakama ya nini basi?

Mkuu,
Hapo sijakupata vizuri, hebu soma paragraph yangu ya mwisho uone kama nimetofautiana na swali lako.
 
Mkuu,
Hapo sijakupata vizuri, hebu soma paragraph yangu ya mwisho uone kama nimetofautiana na swali lako.

Nimekuelewa ulivyosema... kimsingi ni kuwa kwa vile kesi hii iko mahakamani ambapo Mbowe Hotel inabishania kiasi cha riba basi tusubiri mahakama iamue; vile vile kwa vile mikataba siyo vitu vilivyoandikwa mbinguni hata ikishaingiwa inaweza bado kupitiwa upya ili pande zote mbili zinufaike au kuondoa utata wowote. Hadi hivi sasa NSSF hawataki kupitia huo mkataba na hiyo ndiyo sababu nyingine ya kesi mahakamani.

Sasa kama tukiakua kweli kufuata sheria utaona basi kuwa mahakamani ndiko mambo haya yataamuliwa na siyo kwa shinikizo la kusema "alipe alipe" kwa sababu tu ni deni!

Nimekupata.
 
7.5m mpaka kufikia 229m

7.5m mara miaka 19 = 142.5m

12m mara miaka 19 = 228m


jamani ni riba ya aina gani hiyo hata kama ame default pamoja na faini haiwezi kufika hiii
mboe usilipe nenda maakamani inaonekana hizi ni hila za kisiasa
 
Dawa ya deni ni kulipa.Kigazeti cha CCM ni cha Wazushi wachovu wa akili.SUUNI O LETA UHURU NWIZI PEPA WILI BE REDUZIDI TO E TABLOIDI.Ukope 7 M ulipe karibu 300M???Hii hapa USA wanaiita predatory landing.Mbowe alipe deni NCCF ni wezi Kigazeti cha Uhuru nacho watueleze nani kawatomasa waandike habari hiyo?
 
Madela wa Madilu,
Mkuu wangu kuhusiana na riba wala tusitake kuitazama kwa vigezo mnavyotoa kwani yawezekana kabisa miaka 19 ya mkopo ikafika kiwango hicho maadam tufahamu ni asilimia ngapi ya riba huweka kwa kila mwezi..

Nitakupa mfano mdogo sana jinsi riba inavyojiongeza.. Ukiwa Umekopa Tsh.100 na riba ni asilimia 20 unatakiwa kulipa 120 by the end of the month mara nyingi wenye riba wanakuandikia unatakiwa kulipa Tsh. 20, pamoja na service charge na kadhalika tuseme Total Tsh 30..
Usipolipa mwezi wa kwanza, mwezi unaofuata deni linaseama (Previous Balance) unadaiwa 130 na riba yake ni asilimia ile ile 20 ya amount hiyo Tsh.130,..hivyo utatakiwa kulipa Tsh 26 kama riba plus services na late fees na kadhalika, Total amount ya deni linaweza kuwa Tsh. 160 mwezi wa pili tu.. Hivyo hivyo ukiendelea kutolipa deni linakuwa ni pamoja na riba unayodaiwa kila mwezi kuongezwa ktk principal, services pamoja na fine zake pia zinaweza kuwa in %..Kwa mwaka mzima deni hilo linaweza kabisa fikia 1,000.. mara tisa ya mkopo uliotolewa..

Mimi kinachonipa shida kuelewa ni sababu zipi zilizoifanya Mbowe Hotels na wadaiwa wengine wasilipe deni hilo hata iwe kiwango kidogo cha ile riba inayotakiwa kila mwezi kuhakikisha deni halipandi zaidi ya mkopo wenyewe..Na kati yetu hatuelewi riba ilikuwa kiasi gani ktk mikopo na navyojua Ukopeshaji wa Bongo inaweza kabisa kuwa ni asilimia 30 au zaidi..

Pili, sielewi kwa nini NSSF walisubiri hadi miaka 19 - Jamani 19yrs!.. ipite hivi hivi wakiandikiana barua na wakopeshwaji wakati sii jambo la kawaida kabisa na matokeo yake wanapelekana mahakamani kama vile huu ni upatu!..Hapa ndipo napoona kwamba tatizo sio Mbowe Hotels ama wadaiwa wengine isipokuwa ni uongozi wa NSSF na nina hakika kabisa yapo mashirika mengi, pengine hata majina ya watu binafsi waliokopeshwa fedha hizo na hazijarudishwa..Mbowe ni Banmgusilo tu anayetumiwa kisiasa kwani hata mtoto mdogo anaweza kuona kinachofanyika hapa.

Kisha kwa wale wanaotaka kujua kwa nini NSSF inakopesha watu nafikiri hapa tutakuwa tunapotosha. NSSF haikumkopesha Mbowe bali imekopesha shirika la Mbowe Hotels na mashirika mengine ikiwa ni non risk ninvestment inayotegemea riba..
Kwa vyovyote vile fedha zinategemewa kurudi na wametengeneza faida ambayo inaendesha shirika zima badala ya kutegemea bajeti ya serikali kulipia matumizi ya shirika ambalo linatakiwa kujiendesha..
 
Nimekuelewa ulivyosema... kimsingi ni kuwa kwa vile kesi hii iko mahakamani ambapo Mbowe Hotel inabishania kiasi cha riba basi tusubiri mahakama iamue; vile vile kwa vile mikataba siyo vitu vilivyoandikwa mbinguni hata ikishaingiwa inaweza bado kupitiwa upya ili pande zote mbili zinufaike au kuondoa utata wowote. Hadi hivi sasa NSSF hawataki kupitia huo mkataba na hiyo ndiyo sababu nyingine ya kesi mahakamani.

Sasa kama tukiakua kweli kufuata sheria utaona basi kuwa mahakamani ndiko mambo haya yataamuliwa na siyo kwa shinikizo la kusema "alipe alipe" kwa sababu tu ni deni!

Nimekupata.

Tuko pamodzi
 
Back
Top Bottom