Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Tanzania ni shamba la bibi viongozi wa kisiasa wanajilimia tu.

duuuuh kuna siku unaongea mambo ya msingi sana.....hasa ukiangalia Richmond mpaka sa hv huku tegeta wiki ya 3 mgao unaendelea kimya kimya
 
Tundu Lissu hakuyajua haya au alikuwa anamlengeshea Mbowe kijanja achukue uenyekiti?
 
Jamani muacheni mbowe,anakopa kuendesha chama.gharama zimezidi,msisahau hivi sasa amejiongezea mzigo wa kina lipumba.
 
Hawa Ghasia alimtaka Lisu kama kweli anaushaidi, aweke vithibitisho mezani kama sheria ya bunge inavyotaka, cha ajabu yeye akamtaja Mbowe bila kuweka ushaidi mezani.
 
Sabubu ya ujinga wako tuuu, unamtaja mbowe freeman. lakini aliyekopa MBOWE HOTEL, YENYE WAKURUGENZI WATATU WENGINE UWATAJI. NA NDO MAAANA NAPITA TUUU
 
Ukijua kitu kinachoitwa separate entity wala hupati shida
 
CD ishachuja,
Tunataka 200bil za escrow account!
 
Heshima Mbele,

Mbowe aifilisi NSSF

*Adaiwa milioni 1,200, hataki kulipa
*Atumia sheria kukwepa asifungwe
*Adai iliyokopa ni kampuni si yeye


na mwandishi wetu

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anakalia kiasi kikubwa cha fedha za Mfuko wa Hifadhi ya Jamii (NSSF), kwa kukataa kulipa deni alilokopa.

Mbowe anadaiwa wastani wa sh milioni 1200 (sh bilioni 1.2), kutokana na deni alilochukua mwaka 1990 kwa nia ya kufanya upanuzi wa Mbowe Hotel ya jijini Dar es Salaam, maarufu kama Bilcanas.

Kwa kutumia mamilioni aliyokopa kutoka NSSF Machi 10, mwaka 1990, Mbowe aliweza kupanua Mbowe Hotel kwa kujenga mgahawa wa Hard Rock, kumbi za Bilcanas, Much More na Sugar Mama, ambazo amekuwa azitumia kwa ajili ya biashara tangu wakati huo.

Kumbukumbu zilizopo zinaonyesha kuwa deni la mkopo huo aliouchukua kwa kutiliana saini kati yake na Shirika la Hifadhi ya Jamii (NPF), ambalo baadaye lilibadilishwa jina na kuwa NSSF, sasa limekua na kufikia zaidi ya sh milioni 1200. Deni hili linatokana na mkopo aliouchukua na riba inayotokana na deni hilo.

Wakati wa kuchukua mkopo huo NPF (wakati huo) iliwakilishwa na Mustafa Mkulo, aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, huku Mbowe Hotel ikiwakilishwa Mbowe mwenyewe aliyetia saini. Pande zote mbili zilikuwa na mwakilishi mmoja. Mkulo kwa sasa ndiye Waziri wa Fedha.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo kati ya Mbowe na NSSF, ambayo ilichukua majukumu ya NPF, Mbowe Hotel ilikopeshwa sh milioni 15, mwaka 1990. Ibara ya 5, ya Mkataba wa Mkopo kati ya Mbowe Hotel na NSSF yenye vifungu 5.01, 5.02 na 5.03, iliweka bayana kuwa riba ya mkopo huo ilikuwa asilimia 31, na kwamba kila mwaka iwapo riba isingelipwa kwa wakati nayo ingetozwa riba ya asilimia 31.

Kifungu cha 6.01 na 6.02 cha mkataba wa mkopo huo kati ya Mbowe na NSSF vinaeleza kuwa Mbowe Hotel ilitakiwa kulipa deni hilo kwa mikupuo sawa mitano katika kipindi cha miaka sita. Mwaka wa kwanza wa mkopo Mbowe Hotel haikutakiwa kulipa kitu kwa nia ya kuipa fursa ya kujiimarisha katika biashara kwa mwaka wa kwanza.

Malipo hayo yalipaswa kufanyika kila ifikapo Desemba 31, kuanzia mwaka 1991, ambapo kila mwezi alistahili kulipa sh 3,000,000 kama deni la msingi na riba ya asilimia 31 kama ilivyokubaliwa kwenye mkataba.

Wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Manase A. Mbowe, Freeman Aikaeli Mbowe na Dk. Lilian Mtei Mbowe, kwa sababu wanazozijua wao waliamua kuacha kulipa deni hilo bila mawasiliano ya aina yoyote na NSSF wala juhudi za wazi za kuonyesha nia ya kulipa hadi mwaka 1993, walipoamua kulipa sh 3,000,000 kati ya deni lote.

Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo, hadi mwaka 1993, wakurugenzi hao walistahili kuwa wamelipa wastani wa sh milioni 9,000,000 katika deni la msingi, lakini walikaa kimya hali iliyolitia wasiwasi shirika la NSSF.

Baada ya kutoa malipo ya sh 3,000,000, wakurugenzi hao walikaa kimya na ilipofika Septemba 1996, NSSF iliamua kufungua kesi Mahakama Kuu. Kesi hiyo ya madai No. 277 ya mwaka 1996, ilikuwa ikidai Mkopaji alipe deni la msingi sh milioni 12 zilizokuwa zimesalia pamoja na riba.

Hatua hii iliwafanya wakurugenzi wa Mbowe Hotel kuomba suala hilo walimalize nje ya Mahakama. Hata hivyo, hawakuendelea kulipa hadi mwaka 1998, walipopewa tishio la kufungwa jela ndipo waliamua kulipa kwa mkupuo sh milioni 12.

Hadi wanatoa malipo hayo, deni lilikwishakuwa na kufikia wastani wa sh milioni 145.38, na kimsingi makubaliano ilikuwa ni kwamba deni hilo lingelipwa katika muda wa miezi 24 tangua tarehe ya makubaliano.

Hata hivyo, Mbowe na wakurugenzi wenzake waliamua kutoendelea kulipa deni hilo badala yake wakaamua nao kuchukua mkondo wa kisheria kwa kutumia wahasibu kukokotoa tena hesabu za riba, bila mawasilianao na NSSF, na kisha wakachagua kiasi wanachotaka kulipa wao.

Mbowe Hotel ikitumia kampuni ya uwakili ya Nyange, Ringia & Co., walifanya kazi ya kuwasiliana na wahasibu mbalimbali kisha kuwasiliana moja kwa moja na wakili wa NSSF, Ademba Gomba, kutaka deni la riba lipunguzwe.

Mgogoro na mvutano kati ya Mbowe Hotel uliendelea, huku riba ya deni nayo ikizidi kuongezeka na ilipofika Oktoba 11, 2002 Meneja wa Fedha wa Bilcanas Group Inc, Godbless Naftal, kupitia barua yake yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL02/02/01, alikokotoa hesabu na kutaka wakurugenzi wa Mbowe Hotel walipe wastani wa sh 31,959,369.86, kwa maelezo kuwa kanuni iliyotumiwa kukokotoa riba ilikosewa.

Januari 16, 2003 NSSF kupitia kwa Mussa S. A. kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu, alimjibu Naftal kwa barua yenye Kumb. No. NSSF/LA/F.131/10/89/135, akimweleza kuwa NSSF imekataa mapendekezo yake (Naftal) na hivyo wanapaswa kulipa deni lote kwa mujibu wa hukumu ya za Mahakama Kuu za mwaka 1999 na 2001.

NSSF na Mbowe Hotel waliendelea kupigana ngwala mahakamani na kwenye bodi za usuluhishi hadi ilipofika Oktoba, 2006 ambapo Jaji Manento alihukumu wakurugenzi wa Mbowe Hotel watiwe mbaroni na kufungwa jela kwa kushindwa kutekeleza amri ya mahakama ya kulipa deni lao.

Wakili wa Mbowe Hotel, Herbert Nyange, aliwasilisha katika Mahakama ya Rufaa hati ya kiapo ambayo muhuri wake umegonjwa Oktoba 30, 2006 akipinga wakurugenzi wa Mbowe Hotel kukamatwa kwa maelezo kuwa Mahakama Kuu ilikwenda nje ya mipaka kisheria kwa kutaka wakurugenzi wakamatwe.

"Uamuzi wa amri ya kukamatwa kwa walalamikaji (wakurugenzi wa Mbowe Hotel) ulifikiwa kwa misingi ya wazi ya uvunjaji wa kanuni juu ya wajibu wa wakurugenzi dhidi ya deni au uamuzi dhidi ya shirika, hivyo ni kinyume na sheria," alisema Nyange katika barua hiyo ya kupingwa kukamatwa kwa akina Mbowe.

Hata hivyo, kutokana na Mbowe kuona mambo yanaendelea kuchacha, Desemba 14, mwaka 2006, mmoja wa wakurugenzi wa Mbowe Hotel, Dk. Lilian Mtei Mbowe, aliamua kutoa malipo ya wastani wa sh milioni 50 kwa NSSF kwa hundi mba 298492, iliyoambatana na barua yenye Kumb. No. BGI/NSSF/MHL06/01, huku akitaka warejee kwenye meza ya majadiliano badala ya kufungwa jela.

Barua hiyo pia iliomba NSSF irejee barua ya Kampuni ya Ushauri wa Fedha ya Morgan cKlien Associates iliyoteuliwa na Mbowe mwaka 2004 kushiriki majadiliano na usuluhishi juu ya jinsi ya kulipa deni hilo.

Kampuni hiyo iliyokuwa chini ya Afisa Mtendaji Mkuu, Hubert Mengi, ilitoa maelezo mengi yenye kuonyesha kwa nini Mbowe Hotel ilishindwa kulipa deni lake kwa wakati. Anasema katiak moja ya vielelezo kuwa fedha zilipotolewa na NSSF mwaka 1990, nchini Tanzania hakukuwapo vifaa vya ujenzi.Mengi anaeleza kuwa Mbowe Hotel walilazimika kuagiza vifaa vya ujenzi kutoka nje ya nchi, na lilijitokeza tatizo lingine kwamba benki nchini hazikuwa na fedha za kigeni, hivyo Mbowe Hotel ililazimika kusubiri kwa muda mrefu kupatiwa fedha hizo za kigeni.

Kwa maelezo hayo, anasema Mbowe Hotel walichelewa kupata vifaa na mradi ukashindwa kukamilika kwa wakati hali iliyosababisha wakurugenzi wake washindwe kulipa deni hilo kwani walikuwa hawafanyi biashara.

Baada ya mivutano yote hiyo, Mbowe Hotel wamealikwa kwenye NSSF kujadili jinsi ya kulipa deni hilo linaloendelea kukua lakini hadi jana vyanzo vyetu kutoka NSSF vilionyesha kuwa wakurugenzi wa Mbowe Hotel wameamua kukaa kimya.

Kutokana na hali hiyo, ni wazi NSSF inaendelea kupoteza mapato yake yanayokaliwa na wakopaji wa aina hiyo, ambapo mwenendo usipodhibitiwa shirika linaweza kufilisika sawa na ilivyotokea kwa mashirika mengi nchini


======
makinda ya CCM Someni hapa ........​
 
Wadau, baada ya kipindi cha Maswali na Majibu, kulikuwa na miongozi ya Wabunge kwa Naibu Spika. Moja ya hoja zilizojitokeza ni madai ya Lissu kuwa Wabunge wa CCM wanachukua fedha kutoka kwenye mifuko ya jamii.

Hata hivyo, waziri Gaudensia Kabaka alisema kuwa si kweli kuwa wabunge wanaenda kuchukua fedha kwenye mifuko ya kijamii na kuweka mfukoni mwao bali wanaomba fedha kwenye mifuko hiyo kwa ajili ya maendeleo kwenye majimbo yao.

Alisema kuwa ni wabunge wa CCM ndio wanaojitokeza kuomba kwa ajili ya majimbo yao jambo ambalo amesema kuwa ni jema. Anawashangaa wabunge wa upinzani kulalamika kuwa wabunge wa CCM wanaomba fedha kwenye mifuko yao ilhali wao hakuna anayewazuia kuomba.

Kibaya zaidi waziri Kabaka alisema ni pale Mbunge ambaye anajitokeza kukopa fedha kwenye mifuko hiyo na akakaa na deni kwa muda mrefu hali inayomfanya awe kwenye risk ya kukamatwa na kufunguliwa mashtaka. Alisema kuwa kuna kiongozi mmoja wa upinzani ambaye amekopa fedha nyingi NSSF na mpaka sasa anakwepa kulipa.

Katika majibu ya nyongeza, Waziri wa TAMISEMI, HAWA GHASIA alimtaja mtu huyo kuwa ni Freeman Mbowe, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ambaye alitumia mamlaka yake kama KUB kukopa kiasi kikubwa cha fedha (kiwango hakikubainishwa) na mpaka sasa hajalipa na haoneshi nia ya kulipa hivyo kujiweka kwenye uwezekano mkubwa wa kukamatwa
Hivi unafikiri kwa makini kweli,Hawa Ghasia( waziri ), ndio msemaji wa shirika la NSsF?, pili kwani Mh.Mbowe alipokuwa anakopa Ghasia( fujo), alikuwa mdhamini?,
Kama ndio hivyo sasa tueleza waliouza benki yetu ya NBC ni Mh.Mbowe?, ukichanganya zaidi tueleze wazee wetu wastaafu hadi sasa hawajalipwa mafao yao ,tatizo ni mkopo wa Mh.Mbowe?, fanya hesabu hela alizokopa mbowe ndizo zimesababisha wale wazee wasilipwe?
Kama haitoshi ,tueleze aliyeiba fedha za EPA na kurudisha usiku bila watu kuwaona unavielelezo toka benki yoyote kuwa nani,wapina wangapi walirudisha?
Pesa ml2000 zidadavue ziko wapi?, hati chafu za halmashauri zinasababishwa na Mbowe?, wizi wa tembo,miradi hewa ,na hata balali yuko wapi?, zungumza kwa nini madawati hatuna wakati miti ikiuzwa nje?, mwisho tuambie waliokopa fedha za kampeni toka nssf wataje harafu tukuumbue zaidi fisadi wewe
 
Huyu Mbowe kaifilisi NSSF mkuu, mbwembwe kibao kumbe madeni..

Hazidi mbwembwe za Tanzania! Uliona siku ile mavifaa ya kivita? Yote yale yamenunuliwa kwa pesa ya kukopa. Kila mtanzania ana deni lisilopungua 500,000/=! Halafu ho uchumi umepanda!
 
Ukijua kitu kinachoitwa separate entity wala hupati shida

Shida ya watu walio wengi, kuanzia mwandishi wa hiyo stori, aliyeileta hapa JF na wachangiaji, kwa kweli ni uelewa wao mdogo katika masuala ya sheria.

Mkataba walioingia Mbowe Hotels na NPF (then, kabla ya sheria namba 28 ya mwaka 1997 haijaifanya kuitwa NSSF) uko governed, pamoja na mambo mengine na Sheria ya Mkataba Law of Contract Act (RE 2002), huo Law of Contract Ordinance).

Pamoja na mambo mengine, sheria tajwa, inaweka miongozo ya namna ya kuingia mikataba na inapotokea upande mmoja umefanya "breach" basi kuna remedy ya upande mwingine inapata.

Kimsingi, sheria pia imeweka mazingira ambayo, utekelezaji wa mkataba ukishindikana, upande husika hutoa utetezi wake,na hapo tumeona Mbowe Hotel wameelezea 'Commercial Sterility" kama miongoni kwa mambo yaliyosababisha kushindwa kutekelezwa kwa mkataba.

Tusimame kwenye mantiki na sheria. Tuache mahaba niue..
 
akichangia hoja mh.wenje mh.mbowe alisema moja ya makampuni yake yanaidai actl dola laki mbili....hata yeye anadai.
 
Back
Top Bottom