Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Mbowe ahusishwa na UFISADI wa kuimaliza NSSF

Hii ni makala ya Padri Karugendo inayopatikana hapa: http://www.freemedia.co.tz/daima/2008/3/23/makala6.php
NI vizuri kwamba Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amejitokeza na kuelezea kwa ufasaha tuhuma zinazolenga kumtupa kwenye kapu la mafisadi.
Asingejitokeza, tungemshangaa kama tunavyowashangaa wanaonyoshewa vidole wakakaa kimya. Waraka wa Mbowe, aliousambaza kwenye vyombo vya habari unajitosheleza.
Walio wengi tumeelewa na kukubali kwamba yeye si fisadi na wala si mwizi, bali alikopa fedha NSSF, kitu ambacho ni cha kawaida. Hata kabla hajajieleza tulishabaini kwamba hizi ni njama za ‘wajinga’ wachache.
Tunafahamu kwamba hizi ni njama za watu wanaotumiwa kuchafua majina ya watu kwa malipo ya vijisenti vichache. Tunafahamu kwamba hizi ni njama za watu wasioheshimu taaluma zao za uandishi wa habari.
Tulishuhudia uhuni huu wakati wa kumchagua mgombea wa urais kupitia CCM. Baadhi ya wagombea walichafuliwa na kupakwa matope.
Tunawafahamu waandishi hawa wanaoandika kwa kuweka chumvi kila habari. Ni wale walioandika kwamba Edward Lowassa, alipokewa kwa magari 400 kule Arusha, wakati alipokewa kwa magari 80.
Ni aina ya waandishi walioshindwa kuandika chochote juu ya maandamano ya vijana ya kulaani vitendo vya Richmond, yaliyofanyika siku ile Lowassa alipopokewa kishujaa nyumbani kwao.
Ndio hao hao wanaosema Mbowe, anadaiwa sh milioni 1,200, wakati yeye alikopa sh milioni 15 na amelipa zaidi ya asilimia 75. Wanaandika bila utafiti, wanaandika bila kutafakari, wanaandika ili walipwe!
Kwao pesa ndizo zinabainisha uongo na ukweli. Hawa ni aina ya waandishi wasiotambua maana ya mkopo na wizi?
Mbowe alikopa NSSF, mafisadi waliiba BoT! Ina maana hawaoni tofauti?
Ni makusudi! Ni kutaka kuandika ili walipwe! Hawa ni waandishi wa hatari.
Mauaji ya kimbali nchini Rwanda, yalichochewa kwa kiasi kikubwa na waandishi wa namna hii. Ni jambo la muhimu na la haraka kwa Watanzania kuwakataa waandishi hawa hatari.
Tuyasusie magazeti yao, maana wana nia mbaya ya kutupotosha, wana nia mbaya ya kutaka kuuficha ukweli na kuutukuza uongo. Wanachuja mbu na kummeza Ngamia!
Mbowe, aligombea urais wa taifa letu Mwaka 2005. Kampeni zilikuwa nzito, alipasua anga kwa anga na kuwa tishio kwa wale waliokuwa wakipiga kampeni nyumba kwa nyumba wakigawa vitenge na chumvi.
Kama shutuma hizi anazobambikiwa leo zingekuwa na maana yoyote, basi zingejitokeza wakati wa uchaguzi mkuu.
Mbona hakuna hata chombo cha habari kilichosema juu ya deni la NSSF wakati huo? Deni hili si la leo na wala si la 2005 ni la zamani kabisa. Mbona halikujitokeza wakati ule na badala yale linakuja kujitokeza leo wakati wapinzani wakiwa katika jukwaa wakifichua wizi mkubwa unaoendelea katika taifa letu?
Mbona linajitokeza leo baada ya Mbowe kujitokeza kwa nguvu kupinga ufisadi?
Kusema kwamba mkopo wa Mbowe unaifilisi NSSF ni kichekesho. Hata aliyeandika haya kama ni msomi, mtu makini, anayefanya utafiti na kuchambua masuala mbalimbali katika jamii yetu ni lazima ajicheke mwenyewe na kujidharau.
Kila siku tunayaona mambo makubwa ya NSSF, hawa wanajenga majumba makubwa kila sehemu ya Tanzania, kama wamefilisiwa na Mbowe wasingekuwa wanafanya chochote kile.
Hata hivyo kutokana na maelezo ya Mbowe, deni analodaiwa limelipwa zaidi ya nusu. Kama si utata uliojitokeza NSSF angekuwa amemaliza kulilipa.
Kuna watu wa kusemwa juu ya NSSF na wala si Mbowe. Kuna tunaowafahamu ambao walinunua nyumba za NSSF kwa bei ya chini na baadaye kuziuza kwa bei ya juu.
Walijua kabisa kwamba wanazinunua nyumba hizo kwa bei ya chini. Walifanya hivyo kwa kushirikiana na NSSF kwa lengo la kupata chochote kama ulivyo utamaduni wetu Watanzania wa kuiuza nchi yetu kwa vijisenti vichache.
Ni kama ilivyo mikataba yote ya taifa hili, mikataba mibovu yenye lengo la kuwanufaisha wageni na kuwakandamiza wananchi. NSSF ina kashifa zake na ufisadi mwingi, deni la Mbowe ni tone dogo kwenye bahari kubwa!
Mbali na vyombo vya habari, kuna baadhi ya vyama vya upinzani vinamshambulia Mbowe. Mwenyekiti wa SAU, anatoa ujumbe wa wazi kwamba yeye ni kibaraka wa CCM, amekuwa akifanya hivyo siku zote.
Watanzania wanafahamu, wala hana haja ya kujificha nyuma ya wapinzani. Huyu hatusumbui hata kidogo. Ni Watanzania wachache sana wanaoweza kumsikiliza na kuamini kile anachokisema.
Nimekuwa nikimheshimu sana mchungaji Mtikila. Huyu akisema watu wanasikia. Lakini nimemshangaa jinsi alivyochanganya mambo. Badala ya kumaliza upande mmoja ambao uko wazi kabisa, upande wenye ushahidi usiopingika wa ufisadi, anamgeukia Mbowe.
Inawezekana kapitiwa, maana mtu makini kama alivyo Mchungaji Mtikila, si wa kutoona tofauti kati ya mkopo na wizi. Mbowe, alikopa na hakatai kulipa. Mafisadi wameiba na bado wanajificha, eti wanarudisha fedha walizoziiba kimyakimya.
Walio wengi wameiba na kuwekeza nje ya nchi. Mbowe, amekopa na kuwekeza hapa hapa, ametengeneza ajira kwa vijana wetu, analipa kodi, ni kati ya wafanyabiashara wanaolipa kodi kwa muda na kwa uaminifu na kutoa mchango katika ujenzi wa taifa. Haiwezekani kwamba mchungaji Mtikila halioni hili!
Sitaki kuamini kwamba hizi ni propaganda za CCM, maana chama kikongwe kama CCM, hakiwezi kufanya propaganda za ‘kijinga’ kama hizi. Mwana CCM aliye makini ni lazima afanye jitihada za ziada kukisafisha chama chake badala ya kutaka kufunika madhambi makubwa yaliyofanywa na wana CCM na maswahiba wake.
Mbinu za kutumia vyombo vya habari ili Watanzania wafumbe macho juu ya Richmond, EPA na mengine ni mbinu zilizopitwa na wakati.
Kama ufisadi uliojitokeza katika taifa letu ungekuwa ni wa mtu mmoja ama wawili, basi wapambe wangeweza kuufunika kwa kumpakazia Mbowe. Bahati mbaya ufisadi huu ni mkubwa sana. Ni ufisadi wa kutisha, ni ufisadi unaofunga wimbo wa ‘nchi yetu ni masikini.’
Ni ufisadi unaowaingiza watu wengi, viongozi wengi, makampuni mengi, chama tawala, Serikali na watu wengi kutoka nje ya nchi.
Ufisadi huu umeamsha hasira za wananchi. Watu wamegundua kwamba wakati viongozi wetu wanatulisha kasumba kwamba nchi yetu ni maskini, na kutulazimisha kuuimba wimbo huu usiokuwa na mwisho, wao walikuwa wakiogelea kwenye utajiri wa kutisha.
Wamekuwa wakitumia pesa za taifa letu kujitajirisha wao, familia zao na marafiki zao.
Wakati viongozi wetu wakituhimiza kujenga sekondari za kata, watoto wao si kwamba wanasoma nje ya nchi bali wanaishi maisha ya peponi, baadhi yao wamekuwa wakiruka kutoka London kwenda Cape Town – Afrika Kusini kwenye sherehe za ‘Birthday’, wengine wanaendesha magari ambayo hata Wazungu hawataweza kuyaendesha.
Je, kumpakazia Mbowe, kutatoa ukweli kwamba Rostam Aziz, si Mtanzania asilia? Kwamba hakuzaliwa hapa na wala hajawahi kuomba uraia? Itaondoa ukweli kwamba mbali ya kuwa mbunge, kinyume cha sheria ameshika nafasi nyeti kwenye chama tawala?
Kwamba amekuwa akikingiwa kifua na viongozi wa juu serikalini? Serikali yetu imekuwa na msimamo mkali juu ya wahamiaji haramu kiasi cha kuwafukuza hata Watanzania wenye asili ya Rwanda na Burundi, Watanzania wenye vyeti vya uraia vinavyotambuliwa na serikali, lakini serikali hiyo hiyo inawafumbia macho wageni wanaohujumu uchumi wetu!
Mbowe hakuchota pesa kutoka NSSF, hakuiba kutoka NSSF, alikopa. Hili ni jambo la kawaida. Mafisadi wa EPA, hawakukopa, waliiba! Hawa niwezi! Wanaopitisha mikataba mibovu kwa kupokea chochote ni wezi, wanapokea rushwa. Huwezi kuwaweka hawa kapu moja na Mbowe.
IGP Mwema amewafananisha mafisadi na magaidi, amesema hawakamatiki. Hawa huwezi kuwalinganisha na Mbowe. Vinginevyo ni kumdhalilisha na kumkosea haki.
Hata kama kuna njama za kumhujumu Mbowe na wapinzani, njama hizi zimefanyika ‘kijinga’. Ni bora hawa wanaoandaa njama hizi wakatambua kwamba Tanzania ya jana na juzi si sawa na ya leo.
Watu wameanza kufumbua macho, watu wameanza kuhoji. Watu wana uwezo wa kuchambua fisadi na asiye fisadi. Leo hii watu wana uwezo wa kuchambua uongo na ukweli.
Mbowe, umesema tumekusikia, tumekuelewa na kukuamini.
Usitetereke! Endeleza mapambano hadi kieleweke!
Nipigie: +255 754 633122

Karugendo unasema ? Haya nadhani wenye masikio na waelewa wamesha elewa .Tuendelee kuwapa wapiga kura Elimu.Jambo moja ambalo washabiki na wanachama wa CCM hawajui ni kwamba Kila chombo cha habari na watanzania kwa ujumla wameichoka CCM.Ndiyo maana unaona hata Jambo watu wanasema mawazo yao wabanakia kuitwa wana Chadema ama wapinzani .No jibu ni kwamba Watanzania wamechoka sana na CCM uozo wake dawa ni CCM kutumia Vyombo vya usalama na kukakia Katiba ya Kikoloni kuwa madarakani lakini wakiweka ngoma sawa CCM wanaujua ukweli kwamnba wamesha chokwa .
 
Mtanzania hapa HUNA HOJA KABISA, umedhalilisha akili yako mwenyewe.

Ukimsoma vizuri Karugendo utaonakwamba amefanya utafiti wa kutosha, kwani anajua hata NANI aliandika nini wakati gani, na ameshiriki vipi katika saga hili la Mbowe. Anajua nani anamtumia nani...Wewe umeingiza jaziba zako na mapenzi yako kwa mafisadi.

Kama huoni kwamba katika hili Padri Karugendo hakemei ufisadi, basi hujui kutafsiri unachokisoma. Hebu msome tena ujue anakeme nini. Hata huoni kwamba anawakemea wanaotaka kufunika hoja ya UFISADI kwa kutumia DENI la Mbowe ili naye aonekane fisadi, anyamaze, huku amekopa kihalali na analipa...? Unataka kusema wewe una akili ndogo kiasi ch akushindwa kuona SIASA katika deni la Mbowe?

Unawalaumu wakubwa kukopa, kwani ni siku gani wamewazuia wadogo kukopa? Au ni wivu tu wa kijinga? kwani unadhani kama Mbowe asingekopa hizo pesa ungekopa au ungepewa wewe? Au ni lini ulienda kukosa NSSF wakakuzuia kwamba usikope kwa sababu wewe sio kigogo? Acha utoto, jadili hoja.

Hili ni deni, sio wizi, wala Mbowe hajakataa kulipa, ila kuna ubishi wa kibiashara kuhusu riba iliyoongezeka, ambayo wanaobishana wakikubaliana atalipa. Sasa unawaambia CHADEMA waache kutetea UOZO, upi? Au umepotoshwa ukapotoka, sasa unatumia akili za balile na rostam kulifikiria hili? Sema usemalo, deni la Mbowe haliwezi kunyamazisha wananchi kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya mafisadi wa EPA na Richmond zote mbili, ya Dar na ya Mwanza....Huna hoja kabisa...

Kichwamaji,

Toa ushahidi hapa wa mapenzi yangu kwa mafisadi? Search hata JF yote na lete wapi mimi nimetetea mafisadi?

Tofauti ya mimi na wewe ni kwamba kwako ufisadi una rangi, una chama, wakati wengine tuko hapa kumkoma nyani giladi, hatuangalii sura wala chama.

Nimedhalilisha akili yangu? well I hope huna uwezo wa kupima akili za watu na laiti ungelikuwa nao basi ungekuwa na hoja za maana zaidi ya kashfa unazoandika. Matusi ni dalili ya mtu asiye na hoja na anayetaka kukuza hoja yake kwa manguvu. Kama hiyo ndio akili, basi we have a big problem here at JF.
 
Karugendo unasema ? Haya nadhani wenye masikio na waelewa wamesha elewa .Tuendelee kuwapa wapiga kura Elimu.Jambo moja ambalo washabiki na wanachama wa CCM hawajui ni kwamba Kila chombo cha habari na watanzania kwa ujumla wameichoka CCM.Ndiyo maana unaona hata Jambo watu wanasema mawazo yao wabanakia kuitwa wana Chadema ama wapinzani .No jibu ni kwamba Watanzania wamechoka sana na CCM uozo wake dawa ni CCM kutumia Vyombo vya usalama na kukakia Katiba ya Kikoloni kuwa madarakani lakini wakiweka ngoma sawa CCM wanaujua ukweli kwamnba wamesha chokwa .

Lunyungu,

Na hao wanaoita wengine ni watetezi wa mafisadi bila hata kutoa ushahidi? Au wengine wamedhalalisha akili zao bila hata kuandika why? Kumpinga Mbowe kwenye hili suala ni kudhalilisha akili yako?

Hiyo ndio JF yetu ambayo baadhi ya watu wanaona bila personal attacks, basi hakuna mijadala. KIbaya zaidi, watu akama hao wanaona eti wanajadili hoja kwa akili, kwi kwi kwi!!! kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.
 
Kichwamaji

Unaushahidi Wowote Wa Kuonyesha Kwamba Hili Suala Linasukumwa Na Lowasa Na Mwenzake Rostam ?

Kama Unao Basi Uweke Hadharani

Mimi Nakumbuka Sikuile Mbowe Anaongea Na Vyombo Vya Habari Lowasa Alikutana Na Rostam Pale Uwanja Wa Ndege , Watu Wengi Waliondolewa Katika Vip Wakabakia Wao Tu Wakaongea Kwa Dakika 30 Hivi Kisha Lowasa Akapanda Mchuma Akaishia Sijui Waliongelea Nini

Inawezekana Ni Tukio Hili

SHY,

Siku moja nikiwa Bungeni Dodoma mwaka jana, nilishuhudia Lowassa akimuita mbunge mmoja wa Chadema na kumuonya kwa maneno yanayofanana na haya(kwa sababu siwezi kuyakumbuka yote): "nyie mbona mnatushambulia sana bungeni kuhusu pesa zilizochukuliwa NSSF? Kumbuka na bosi wenu ana deni pale, tukiamua kumuumbua hatushindwi..hii ni siasa bwana, lolote linaweza kutokea..."

Na hapa katikati, rafiki yangu mmoja mwandishi wa habari aliniambia kwamba alitwa na Rostam akapewa DILI la Mbowe alilipue kwenye vyombo vya habari, mwandishi akapewa mshiko kidogo, lakini mwandishi alitaka kuifanya kitaaluma kwa kulitafiti mwenyewe kuliko kusukumwa tu na matakwa ya kisiasa na kimaslahi ya Rostam na kundi lake, akaanza kulichunguza.

Alipochunguza suala lenyewe akakuta ni DENI ambalo katika misingi ya biashara nijambo la kawaida, na kwamba stori ilishindwa kuandikika kwa sababu ilionekana mdaiwa ANALIPA siyo kwamba halipi bali hajakamilisha deni, na zaidi ya hayo NSSF walimwambia suala hilo liko mahakamani kwa kuwa kuna ubishi wa kipi kilipwe...wakati bado anaendelea na uchunguzi wake, akasoma stori hiyo hiyo katika gazeti la RAI linalomilikiwa na Rostam na Azizi. Na inasemekana sasa ile stori imeandikwa na balile, yule mwandishi (kipenzi cha lowassa), ambaye amekuwa anaandika habari za kumsafisha lowassa.

Hapo hapo usisahau wameanza jitihada za kujisafisha kwa kuelekeza macho ya umma kwingine, ndiyo maana unaona stori nyingi zinazonadikwa na Mtanzania zinahusu zaidi EPA ili ionekane ishu ya RICHMOND ni cha mtoto, zipo kubwa za Mkapa na EPA....

Lakini hapo hapo wanatafutwa kasoro za wapinzani ili wawapake nao wafunge mdomo, nchi iliwe vizuri. DENI la Mbowe likafanywa lionekane WIZI!!! haikubaliki. Hili ni deni, nadhani hata wewe shy kuna watu wanakudai sasa..au unawadai...kukopa kwa haki na kulipa pole pole hakuwezi kufanywa ufisadi.

SHY, hapo nimekupa dodoso tu...nawe tumia akili yako kutafuna, kutafakari nan kuchambua dodoso hizo, fanya judgement ya kiutu uzima ulete hoja yako
 
Lunyungu,

Na hao wanaoita wengine ni watetezi wa mafisadi bila hata kutoa ushahidi? Au wengine wamedhalalisha akili zao bila hata kuandika why? Kumpinga Mbowe kwenye hili suala ni kudhalilisha akili yako?

Hiyo ndio JF yetu ambayo baadhi ya watu wanaona bila personal attacks, basi hakuna mijadala. KIbaya zaidi, watu akama hao wanaona eti wanajadili hoja kwa akili, kwi kwi kwi!!! kweli akili ni nywele na kila mtu ana zake.

Mkuu Mtanzania
Salaam toka Comoro , mimi nimeandika haya baada ya kuona kila mara tunarushiana maneno hapa mara Chadema , mara CCM mara mpinzin mara mtetea mafisadi .JF ina watu makini na badala ya watu kulia lia kama Makamba kila saa ni vyema wakajua kwamba CCM ni kweli haipendwi kabisa nainatumia mabavu nandiyo maana kila mahali watu wanaiponda na wachache sasa wana acha maana na kuja naunazi hapa namatusi lakini nadhani ni vyema kubakia huru na kukata issues bila kuwashutumu watu .Jenga hoja kama msomi na si kukurupuka kulinda maslahi kwa uwazi na kila mmoja anakuona na kukudharau .Tabia hii imeibuka hapa ya watu kuacha kujadili issues wanachanganya habari na kuua maana ya mada ndiyo sababu kila mahali nawaomba warudi kwenye mada na kuacha udaku ama kuchanganya mambo .
 
Kichwamaji,

Toa ushahidi hapa wa mapenzi yangu kwa mafisadi? Search hata JF yote na lete wapi mimi nimetetea mafisadi?

Tofauti ya mimi na wewe ni kwamba kwako ufisadi una rangi, una chama, wakati wengine tuko hapa kumkoma nyani giladi, hatuangalii sura wala chama.

Nimedhalilisha akili yangu? well I hope huna uwezo wa kupima akili za watu na laiti ungelikuwa nao basi ungekuwa na hoja za maana zaidi ya kashfa unazoandika. Matusi ni dalili ya mtu asiye na hoja na anayetaka kukuza hoja yake kwa manguvu. Kama hiyo ndio akili, basi we have a big problem here at JF.

Kwikwwikwikwikwi!

Mtanzania, inawezekana wewe hufanyi hivyi makusudi, lakini maandishi yako yananyesha kwamba yameathiriwa na njama zile zile za akina RA ambao ndio walipanga mkakati huu kuwachota waganganyika...labda hukujua, umesubiri kulikuta hapa JF.. ila tayari wamefanikiwa kwa mbinu yao, na kwa wewe kujadili deni hili kwa msisitizo huu unatetea azima ya mafisadi wenyewe. Ushahidi utajileta wenyewe kwenye maandishi yaetu hapa...

Pole naona umeguswa, lakini ndo hivyo sisi wengine tunakerwa na mbinu chafu zinazotumiwa na mafisadi kunyamazisha hoja kwa vijistori kama hivi hapa...na tunakerwa na mashabiki wao (hata kama wanafanya hivyo kwa kuchotwa tu).

Nasema hivyo kwa kuwa najua asili ya hoja hizi, na diyo maana hata akina Karamagi na Lowassa nao sasa wamejiingiza katika uwekezaji wa vyombo vya habari na mmojawapo wa consultants wao ni balile huyo huyo wanayemtumia, katika gazeti litakalosimiwa na Prince Bagenda. Jipe muda, mtajua mengi mwaka huu, lakini msikubali kupotoshwa na kina RA na EL
 
Sumaye hakuwa mwanachama, why? Wakati alikuwa mfanyakazi wa serikali kwa muda mrefu kabla ya kuwa mwanasiasa? Pia alikuwa kwenye shirika la umma kabla ya kuwa mwanasiasa. Ni nani huyo aliyesema Sumaye hakufuata sheria?

NSSF walisema amekopa kwa kufuata sheria.
hapa ishu siyo sumaye wala nini, ishu hapa ni mbowe, hata kama sumaye alipatia au kukosea hii haina mantiki yoyote mintaarafu ishu hii ya Mbowe.

Kwa mimi wote wawili wana makosa yanayofanana, kosa la wanasiasa na matajiri
kukopa kule ambako mwananchi wa kawaida hawezi kukopa
. Niambie Machinga gani ambaye ni mwanachama wa NSSF amewahi hata kukopa laki moja huko NSSF?

Mkuu hapa nadhani hapa hakuna hoja, kama ukopaji NSSF ni ruhusa kisheria basi hapa laumu sera usilaumu Mbowe.by the way kuna baadhi ya mikopo inalenga project kubwa kubwa zenye uwezo wa kuleta impact katika uchumi, siyo mtu anataka kufungua genge la nyanya basi naye aende NSSF akakope

Kosa la pili la Mbowe ni kushindwa kulipa deni lake kwa muda waliokubaliana mpaka kuanza kuburuzwa mahakamani.

Yeye mwenyewe amedai anadaiwa na NSSF ila anapinga kwamba sio hizo 1.2 bilion. Sasa si alipe anazodaiwa? Kweli deni la miaka 6 linachukua miaka 18, watu hamuoni kosa hapo?
wewe Mtanzania umekuwaje?. ndiyo mbowe anapinga hizo milioni 1200 lakini hawezi kujiamulia kulipa anazozitaka yeye, ndio maana kuna kesi inunguruma mahakamani ili iamuliwe alipe kiasi gani,kwa sbabu inaonekana ugomvi mkuu hapa siyo Mbowe hataki kulipa,bali hajaridhika na kiwango anachoambiwa alipe,nio maana shauri lipo mahakamani, au kwa mtizamo wako mtu kushitakiwa mahakamani tayari mtu huyo keshakuwa mhalifu?

Kosa la tatu ni kwamba NSSF ni mfuko wa Watanzania wa kawaida, wengi wao wakiwa maskini. Failure yoyote ya hiyo NSSF kukusanya madeni, madhara yake ni kwa wananchi wa kipato cha chini. Mbowe kushindwa kulipa hizo pesa, anaongeza taabu hizo wanazopata wanachama wa NSSF
Kosa la nne ni kwamba Mbowe ni mwanasiasa, sio tu kwamba anakuwa judged kiuchumi lakini anakuwa judged pia kisiasa. Kama mwanasiasa, kwa maoni yangu hakutakiwa kukopa NSSF.
wewe sijui unazungumzia mbowe yupi, Mbowe aliyekopa mwaka 1990 au Mbowe aliyegombea uraisi mwaka 2005, labda nikumbushe kidogo tu Mwaka 1990 Chadema haikuwepo wala CUF haikuwepo,wakati huo kulikuwa kuna chama kimoja tu enzi hizo kikiitwa "nambari wani"
yaani CCM. get your facts correct bro[/QUOTE]

Unataka sababu zingine
Kabisa kabisa, kosa la Mbowe ni nini?
 
wewe sijui unazungumzia mbowe yupi, Mbowe aliyekopa mwaka 1990 au Mbowe aliyegombea uraisi mwaka 2005, labda nikumbushe kidogo tu Mwaka 1990 Chadema haikuwepo wala CUF haikuwepo,wakati huo kulikuwa kuna chama kimoja tu enzi hizo kikiitwa "nambari wani"
yaani CCM. get your facts correct bro

Gamba la Nyoka,

Wala hata huhitaji kunikumbusha ninajua vizuri kabisa Mbowe alikopa lini
na lini alianza siasa.

Soma maandishi yangu mengine hapo nimeandika wazi, Mbowe alivyoamua kuingia siasa, hili deni ilitakiwa alifikirie na labda kulilipa.

Kwa mtu binafsi, kwa mawazo yangu, huwezi kukopa NSSF bila kuwa na mazingira ya rushwa. Unaweza usikubali lakini ndio ukwerli wenyewe.

Ndio maana hata alivyokopa Sumaye, watu tulimlaani hivyo hivyo japo yeye wala hakuchelewa kumaliza deni lake.
 
hapa ishu siyo sumaye wala nini, ishu hapa ni mbowe, hata kama sumaye alipatia au kukosea hii haina mantiki yoyote mintaarafu ishu hii ya Mbowe.

Kabisa kabisa, kosa la Mbowe ni nini?[/QUOTE]

GAMBA LA NYOKA,
Unajua watu hapa wameshahau au basi tudhani kwamba hawajui kwamba hata ishu ya Sumaye iliibuliwa a hao hao akina RA, EL na JK kwa malengo ya kisiasa.

Walilenga cheo chake kama waziri mkuu nan tetesi kwamba anautaka urais...lakini hawakusema kwamba SHERIA inamruhusu kukopa NSSF. Walilotaka limekuwa na ndilo hilo wanalotakakutumia kwa Mbowe. Usishangae wanaleta hoja ya Sumaye katika suala la Mbowe, kana kwamba Watz hatuna kumbukumbu za ujasusi wa wanamtandao dhidi ya Sumaye...na kwamba NSSF haina mandate ya kukopesha wajasiriamali, tena walio wanachama wake.

Wanataka tujadili ufisadi katika gunia bila kujua nini kimefungwa mle...wamepotoka. hapa kila hoja itaelezwa chanzo na kusudio lake.

Umefanya vema kumjulisha kwamba mwaka 1990 chadema haikuwapo...
 
Nasema hivyo kwa kuwa najua asili ya hoja hizi, na diyo maana hata akina Karamagi na Lowassa nao sasa wamejiingiza katika uwekezaji wa vyombo vya habari na mmojawapo wa consultants wao ni balile huyo huyo wanayemtumia, katika gazeti litakalosimiwa na Prince Bagenda. Jipe muda, mtajua mengi mwaka huu, lakini msikubali kupotoshwa na kina RA na EL

Mimi najua CCM wanahusika na kutoa hii habari ya Mbowe. Lakini kwangu mimi that is not an issue. Tatizo ni yule mwenye kosa na wala sio aliyesaidia kumuumbua.

Siasa ni mchezo mchafu na kila mtu anajua hilo, sasa ulitegemea CCM wafanye nini? Waandike kumpongeza Mbowe kwa kukopa NSSF?

Kwa mimi sijali nani katoboa siri, ninachojali ni kama hiyo habari ni kweli. Hata kama 90% ni uwongo lakini imesaidia kutufanya tujue ukweli ambao ni 10% kwa mimi ni sawa.

Njia ya kupambana na madhambi kwenye jamii ni pamoja na vita ya panzi furaha kwa kunguru. Wao wenyewe kwa wenyewe wakiumbuana sisi ndivyo tutakavyojua ukweli.

Ni kupoteza muda kuhangaika kujua habari imeanzia wapi au nani anahusika. Hangaikeni kujua ukweli ukoje na kwanini Mbowe ameshindwa kulipa hilo deni miaka 18 baada ya kukopa.
 
Umefanya vema kumjulisha kwamba mwaka 1990 chadema haikuwapo...

Kichwamaji,

Kwa taarifa tu nilikuwa kwenye harakati za kudai haki zetu miaka ya mwisho wa 80. Tulikuwa tunaandamana na akina Marando na wengine wakati huo wanataka vyama vingi viruhusiwe.

Ni kichekesho kwa mtu wa namna hiyo kwamba hajui CHADEMA ilianza lini, au Mbowe alikuwa mwanasiasa lini.

Ninajua siasa hata kama sio mwanasiasa kuliko unavyoweza kudhani.

Jadili mengine maana huko unapoteza muda wako bure!
 
Mkuu Mtanzania
Salaam toka Comoro , mimi nimeandika haya baada ya kuona kila mara tunarushiana maneno hapa mara Chadema , mara CCM mara mpinzin mara mtetea mafisadi .JF ina watu makini na badala ya watu kulia lia kama Makamba kila saa ni vyema wakajua kwamba CCM ni kweli haipendwi kabisa nainatumia mabavu nandiyo maana kila mahali watu wanaiponda na wachache sasa wana acha maana na kuja naunazi hapa namatusi lakini nadhani ni vyema kubakia huru na kukata issues bila kuwashutumu watu .Jenga hoja kama msomi na si kukurupuka kulinda maslahi kwa uwazi na kila mmoja anakuona na kukudharau .Tabia hii imeibuka hapa ya watu kuacha kujadili issues wanachanganya habari na kuua maana ya mada ndiyo sababu kila mahali nawaomba warudi kwenye mada na kuacha udaku ama kuchanganya mambo .

Mkuu Lunyungu,

Huko Comoro unafanya nini? Angalia na wewe usije ukaingizwa kwenye mafisadi wa Comoro!

Vipi wanaujeshi wetu wanapigana huko Comoro?

Hili la NSSF, wakati umefika kwa NSSF kutoa majina ya wanasiasa wote ambao wamekopa huko.

Wanakimbilia kuliko nafuu na kuwaacha Watanzania wengine wakisumbuliwa na
mabank.
 
Mimi najua CCM wanahusika na kutoa hii habari ya Mbowe. Lakini kwangu mimi that is not an issue. Tatizo ni yule mwenye kosa na wala sio aliyesaidia kumuumbua.

Siasa ni mchezo mchafu na kila mtu anajua hilo, sasa ulitegemea CCM wafanye nini? Waandike kumpongeza Mbowe kwa kukopa NSSF?

Kwa mimi sijali nani katoboa siri, ninachojali ni kama hiyo habari ni kweli. Hata kama 90% ni uwongo lakini imesaidia kutufanya tujue ukweli ambao ni 10% kwa mimi ni sawa.

Njia ya kupambana na madhambi kwenye jamii ni pamoja na vita ya panzi furaha kwa kunguru. Wao wenyewe kwa wenyewe wakiumbuana sisi ndivyo tutakavyojua ukweli.

Ni kupoteza muda kuhangaika kujua habari imeanzia wapi au nani anahusika. Hangaikeni kujua ukweli ukoje na kwanini Mbowe ameshindwa kulipa hilo deni miaka 18 baada ya kukopa.

Mtanzania,

Pole pole, hapa sasa umeanza kujadili hoja. Wengi wetu tusioendekeza ushabiki hapa ndipo tulipo. Hata hivyo, kwa umakini wa kawaida, ni vigumu kwa mtu yeyote kijadili hoja vizuri bila kujua vema mazingira yaliyoisababisha. Tunapotaka ku-contextualize stori hii ya mbowe na deni la NSSF tunataka ku-counter mbine ile ile inayotumiwa na wanaoitumia, ili kufunika madhambo yao, hasa pale tunapofanya ulinganifu wa makosa ya wahusika. Hawa ni wezi na huyu ni mdeni. Hatuwezi kuwaweka katika mizani ile ile kama ambavyo watu wengi wamekuwa wakijaribu kufanya hapa katika JF, na hasa kwa vile nia ya awali ilikuwa kumwingiza Mbowe katika kundi la MAFISADI na kumfunga mdomo.

Kudaiwa si ufisadi, na biashara si ufisadi. Ieleweke hapa kwamba sote (naamini hivyo) tunajua kwamba Mbowe ni mfanyabiashara, nakama kawaida wafanyabiashara ni watu wa madeni, maana huendesha shughuli zao kwa mikopo kutoka taasisi zinazotoa mikopo.

Hoja hapa ingekuwa na nguvu kama alikopa KIFISADI au alikomb pesa kama walivyofanya EPA, na jinsi alivyozitumia. Na kwa kuwa lmezuka, yao engi tutayafuatilia kwa karibu, lakini watu makini watakataa KUFUNGWA katika gunia la kina RA, Edo na vibaraka wao. walau si katika hili la kufunika wizi wa mafisadi kwa DENI la Mbowe. Nasisitiza, deni ni kitu cha kawaida sana, hasa katika biashara. Mtanzania, hudaiwi popote? Au humdai mtu? Au hujawahi kudaiwa, tena mazingira yakafanya deni kuwa gumu kulipika kwa muda halisi? Hata kama kuna mazingira ya kisiasa, si wizi huo.
 
Siku moja nikiwa Bungeni Dodoma mwaka jana,

Hakuna tatizo kukopa benki yoyote bongo au duniani, na hakuna tatizo kwa mfanyabisahara kuwa deni lakini ni upinzani ndio unahusika zaidi na kuifanya benki hiyo ionekane kuwa inahusika sana na ufisadi mbele ya jamii, ukweli hata mimi I was shocked kusikia kuwa Freeman, anahusika na kukopa huko kwenye hiyo benki, kama nilivyomuomba majuzi ni kwmaba kama analo deni kweli alilipe turudi kwenye focus ya ishu muhimu kwa taifa, kwa sababu yeye as a politician hana anything to gain na hii ishu, ingawa anazo all the rights kuendelea ku-argue nao on the legal matters of the ishu,

Halafu siamini kuwa hii ishu inakuwa trumpeted na CCM peke yao, hayo mawazo ni very politically naive, as long as you are a politician unakuwa na maadui hata kwenye chama chako sometimes hata ndugu zako, the ishu ni kama wewe mwenyewe unawapa something to attack to you, wanaom-attack could be anybody na wala sio CCM peke yao.
 
chadema ni chagga party why??sina details za kutosha ila kama kuna mtu ambaye atakuwa ameisoma hii taarifa atakubali.
kuna kipindi chadema walifanya maandamano Dr Peter Mziray wa PPT-MAENDELEO aliwaomba aungane nao wakamtosa sasa sijui mziray ni kabila gani ila walimtosa hata kwenye helkopta yao ya wachagga..

Siku nyingine uone aibu ya kuandika mambo yanayofunua udhaifu wako wa ndani. Sentensi yako ya kwanza na ya mwisho zinaonyesha wewe ni mtu muovu katika nafsi yako, na hapa unataka kumwaga uchafu kuchafua nafsi zetu. Viwango hivyo tumevipita, kajitukane mwenyewe! Huna sababu ya kuandika kama huna cha kuandika.
 
Hakuna tatizo kukopa benki yoyote bongo au duniani, na hakuna tatizo kwa mfanyabisahara kuwa deni lakini ni upinzani ndio unahusika zaidi na kuifanya benki hiyo ionekane kuwa inahusika sana na ufisadi mbele ya jamii, ukweli hata mimi I was shocked kusikia kuwa Freeman, anahusika na kukopa huko kwenye hiyo benki, kama nilivyomuomba majuzi ni kwmaba kama analo deni kweli alilipe turudi kwenye focus ya ishu muhimu kwa taifa, kwa sababu yeye as a politician hana anything to gain na hii ishu, ingawa anazo all the rights kuendelea ku-argue nao on the legal matters of the ishu,

Halafu siamini kuwa hii ishu inakuwa trumpeted na CCM peke yao, hayo mawazo ni very politically naive, as long as you are a politician unakuwa na maadui hata kwenye chama chako sometimes hata ndugu zako, the ishu ni kama wewe mwenyewe unawapa something to attack to you, wanaom-attack could be anybody na wala sio CCM peke yao.

Isome vizuri tena hii. Unachozungumza ni hoja, lakini ukweli wa hili asili yake inafahamika, haihitaji kufikirika.

Siku moja nikiwa Bungeni Dodoma mwaka jana, nilishuhudia Lowassa akimuita mbunge mmoja wa Chadema na kumuonya kwa maneno yanayofanana na haya(kwa sababu siwezi kuyakumbuka yote): "nyie mbona mnatushambulia sana bungeni kuhusu pesa zilizochukuliwa NSSF? Kumbuka na bosi wenu ana deni pale, tukiamua kumuumbua hatushindwi..hii ni siasa bwana, lolote linaweza kutokea..."

Na hapa katikati, rafiki yangu mmoja mwandishi wa habari aliniambia kwamba alitwa na Rostam akapewa DILI la Mbowe alilipue kwenye vyombo vya habari, mwandishi akapewa mshiko kidogo, lakini mwandishi alitaka kuifanya kitaaluma kwa kulitafiti mwenyewe kuliko kusukumwa tu na matakwa ya kisiasa na kimaslahi ya Rostam na kundi lake, akaanza kulichunguza.

Alipochunguza suala lenyewe akakuta ni DENI ambalo katika misingi ya biashara nijambo la kawaida, na kwamba stori ilishindwa kuandikika kwa sababu ilionekana mdaiwa ANALIPA siyo kwamba halipi bali hajakamilisha deni, na zaidi ya hayo NSSF walimwambia suala hilo liko mahakamani kwa kuwa kuna ubishi wa kipi kilipwe...wakati bado anaendelea na uchunguzi wake, akasoma stori hiyo hiyo katika gazeti la RAI linalomilikiwa na Rostam na Azizi. Na inasemekana sasa ile stori imeandikwa na balile, yule mwandishi (kipenzi cha lowassa), ambaye amekuwa anaandika habari za kumsafisha lowassa.

Hapo hapo usisahau wameanza jitihada za kujisafisha kwa kuelekeza macho ya umma kwingine, ndiyo maana unaona stori nyingi zinazonadikwa na gazeti la Mtanzania na RAI zinahusu zaidi EPA ili ionekane ishu ya RICHMOND ni cha mtoto, zipo kubwa za Mkapa na EPA....

Lakini hapo hapo wanatafutwa kasoro za wapinzani ili wawapake nao wafunge mdomo, nchi iliwe vizuri. DENI la Mbowe likafanywa lionekane WIZI!!! haikubaliki. Hili ni deni, nadhani hata wewe shy kuna watu wanakudai sasa..au unawadai...kukopa kwa haki na kulipa pole pole hakuwezi kufanywa ufisadi.

SHY, hapo nimekupa dodoso tu...nawe tumia akili yako kutafuna, kutafakari nan kuchambua dodoso hizo, fanya judgement ya kiutu uzima ulete hoja yako
 
Na inasemekana sasa ile stori imeandikwa na balile, yule mwandishi (kipenzi cha lowassa), ambaye amekuwa anaandika habari za kumsafisha lowassa.

Wakuu wanaomjua vizuri huyu mkuu, naomba watufunue macho, huyu si kuna wakati alikuwa London anasoma, na siku alipomaliza shule tuliambiwa hapa JF kuwa ni mwanamapinduzi hodari na tukamtumia ujumbe wa heshima kwa kuwa pia alikuwa ni mwana-JF, sasa since then vipi what happened?
 
Fieldmasrashal kumbe wewe hata magazeti husomi? Huyu jamaa alianikwa na vyombo vya habari vya hapa Bongo, mwaka jana, hata kabla hajamaliza shule huko London, kwamba EL na RA walikuwa wanamtumia kumshughulikia Mbowe kupitia magazeti, huku yeye akiwa ndiye msimamizi wa magazeti ya Mbowe. Alikuwa amepewa assignment hiyo na EL ili watumie gazeti la Rai kuandika makala chafu dhidi ya Mbowe na wapambanaji wengine 'wanaomsamakama' lowassa, katika kipindi kile kile ambacho pia lowassa na jk waliwaomba akina Prince bagenda, Hizza Tambwe na Charles Charles nao wajibu mapigo kwa kuwashambulia washabuliaji wa wakubwa.

Baadhi ya waliokuwa wanalengwa na mkakati huo ni Mbowe mwenyewe, Absalom Kibanda (aliyechukua nafasi ya balile) na Ngurumo (aliyekuwa mhariri Tz daima). balile alipewa kazi hiyo, naye akaomba ushirikiano wa Manyerere (ambaye walitumiwa pamoja pale Tz Daima wakati wa kampeni, sasa yupo Mtanzania) ili kupitisha makala na kzifikisha kwa mhariri wa Rai, na kwamba balile angetumia jina bandia, sijui mwakyembe (la pili nimesahau).

Kumbe bahati mbaya yake, mawasiliano yao na manyerere yalidakwa na wataalamu wa mtandao (nadhani kwa udhaifu wa Manyerere). Balile akaanza mashambulizi, akapeleka makala kwa Manyerere (akimchanachana Mbowe kwa mambo mengi ya kutunga), ilipofika kwa mhariri wa RAI akaisoma akaona UTOTO, akasema: "siwezi kuwajibika kwa utoto hu..kama mwandishi anaamini alichoandika, mwambie atumie jina lake..." akamrudishia Manyerere. Wakati huo huo, Bagenda naye alikuwa amendika makala dhidi ya Mbowe na kuipeleka RAI,..baadaye machale yakamcheza, akampigia simu mhariri wa RAi kumuomba aondoe jina lake. Mhariri (Muhingo Rweyemamu) akasema kama hutaki jina lako liandikwe, makala sitaitumia, akaitupa.

Baada ya hapo yaliyofuata ni aibu ya balile na manyerere, maana mambo yaliibuka na kuwachafua sana, tena ssi wengine tukasema mbona walishatumika hata wakati wa kampeni hadi Tz daima likaonekana ni la mtandano kuliko la Mbowe. Katika mazingira hayo, balile alipoamaliza shule akaamua mwenyewe kukimbilia kwa watu wake na kuwafanyia kazi rasmi...ndivyo alivyojiunga na RA na kuanza kazi ya kumshughulikia Mbowe. upo hapo? Yapo mengi, uliza utaambiwa.
 
Fieldmasrashal kumbe wewe hata magazeti husomi?

You got it right, unataka nisome magazeti gani haya yanayomilikiwa na wanasiasa wa bongo? Nimeuliza swali dogo sana as opposed na hayo majibu yako mengi ambayo hayahusiani na swali langu, kwamba at onetime Balile alikuwa very dear friend wa watu wengi hapa JF, na mpaka alipomaliza shule kule London, hapa kulikuwa na special thread ya kumpongeza, na tuliambiwa kuwa alikuwa karibu sana na Freeman kule London, sasa swali langu ni kwamba alibadilika lini?

Mimi ninasoma JF sisomi magazeti uchwara.
 
wakati tuanaendelea na hii hoja nadhani ni vyema kuwekana sawa kwamba sumaye hakukopa nssf bali ppf. nadhani ni vyema hili likaeleweka hususan kwa wale wanaolinganisha deni la sumaye na mbowe.
 
Back
Top Bottom