Mbowe aligombeaje urais mwaka 2005 kama hana degree?

Mbowe aligombeaje urais mwaka 2005 kama hana degree?

Mtu kama Mbowe anakosaje Degree au ndio siasa za kuchafuana. 😁
Niliwahi wasikia madingi flan wa kichaga wanasema Baba yake Mbowe hata uhuru hujapatikana alikuwa na hela, exposure na mali hatari, kwa mujibu wa wale wazee Nyerere amewahi pewa "Support" na baba yake Mbowe eti kupambania uhuru. 😁

Maana yeke Mbowe ni wa kishua "Born to extremely rich parents".
Achana na wanaomwonea wivu,hadi kusingizia fweza za chama kuchotwa wakati hana njaa kama wao,inawezekana aliwajamata mikono waliotaka kuzichota.Hadi wanasahau kuwa chama kimepata hati safi tangu enzi za mzee Mkweli.
 
Kwa Hisani ya Martin MM

Freeman Aikael Mbowe alizaliwa tarehe 14.09.1961 katika wilaya ya Hai, mkoa wa Kilimanjaro.

Freeman Aikaeli Mbowe alisoma elimu ya msingi katika shule ya Msingi Lambo na kufanikiwa kufaulu kwenda shule ya Sekondari Kibaha mkoa wa Pwani.

Alipohitimu kidato cha 4 Kibaha Sekondari, alifanikiwa kujiunga na kidato cha 5 IHUNGO Sekondari Manispaa ya Bukoba. Baadae alielekea nchini Uingereza kwa masomo zaidi. Uingereza alisoma programu inaitwa PPE (Politics, Philosophy, and Economics).

Ni programu ambayo ilianzishwa na Uingereza kwa ajili ya watumishi serikalini. Baadaye nchi nyingine kama US na RSA zimeshaanzisha programu hiyo. Kwa UK inatolewa kama first degree tu. Mbowe akamalizia MBA in Leadership & Sustainability kutoka Chuo Kikuu cha Cumbria, UK.

Freeman Mbowe ni miongoni mwa Watu waliofanya kazi katika Bank kuu ya Tanzania kama Afisa wa Bank Kuu (BoT) huko ndipo alipofifanikiwa kukutana na Mzee Edwin Mtei, Mzee Bob Makani.

Source:
====
Vigezo gani vilikuwa vinatumika kupata hiyo scholarship ya UK?
Hakuna kigezo miaka ya kina Mbowe hata sekondari wlikuwa wanaenda watoto wa matajiri , maskini walikatwa angalia sana majina ya viongozi wengi wazee yana ubabaishaji ...Pale kibaha hata BOT watoto wa matajiri waliingizwa kimchongo .
 
Back
Top Bottom