Elimu ni muhimu lakini kuweka kigezo cha elimu cha degree sio tu si muhimu, lakini pia ni kigezo cha kibaguzi. Hususan kwenye nchi ambayo watu wengi sana wana uwezo mzuri tu lakini hawana elimu rasmi ya degree.
Inatupasa tuelewe unaweza kuwa na elimu bila degree na unaweza kuwa na degree bila elimu.
Rais wa sasa wa Brazil Luiz Inacio Lula da Silva hana degree, lakini watu wamemkubali sana hawakujali hilo.
Zaidi, kitu muhimu kuliko kukosa degree, ni sababu ya kukosa degree.
Mtu kama Lula hana degree, lakini hakuwa na uwezo wa kusoma,alianza kufanya kazi akiwa mdogo, akafanya kazi sana na kupanda ngazi katika Labor Unions za Brazil, akafika juu kabisa.
Hiyo kazi aliyoifanya huko katika vyama vya wafanyakazi, ni jubwa kuliko degree.
Sasa mtu kama huyo naye utasema huyu hafai kuwa rais kwa sababu hana degree?
Elimu yake practical aliyoipata kwenye siasa za vyama vya wafanyakazi imepita kikwazo chochote cha degree yoyote mtakachoweka.
Sasa hatuoni tukiendeleza kigezo cha degree tutawanyima kina Lula wetu nafasi ya kutuongoza?