kasyabone tall
JF-Expert Member
- Sep 13, 2009
- 254
- 63
Daniel Mjema, Hai
MGOMBEA Ubunge Jimbo la Hai mkoani Kilimanjaro, kwa tiketi ya Chadema, Freeman Mbowe ambaye pia ni Mwenyekiti wa chama hicho, anatuhumiwa kumpiga vibao viwili mwangalizi wa ndani wa Baraza la Waislamu Tanzania (Bakwata), Nassir Othman (20).
Kamanda wa Polisi mkoa Kilimanjaro, Lucas Nghoboko alilithibitishia kupokea taarifa za tukio hilo lakini akasema asingeweza kulizungumzia kwa undani kwa kuwa maofisa wake aliowatuma walikuwa hawajarejea.
Hata hivyo mkuu wa wilaya ya Hai, Dk Norman Sigalla ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na Usalama wilaya ya Hai, alidai kuwa tukio hilo lilitokea saa 8:45 mchana katika kituo cha Zahanati ya Kambo eneo la Msufini.