MBOWE ALIONGEA JAMBO ZITO KUHUSU VIJANA

MBOWE ALIONGEA JAMBO ZITO KUHUSU VIJANA

senzighe

JF-Expert Member
Joined
Jan 1, 2012
Posts
2,108
Reaction score
1,666
Wakati Mhe. Mbowe anatia nia ya kugombea nafasi ya Uenyekiti Chadema alitamka jambo zito sana linalowahusu vijana wa sasa.Naungana na Mhe. Mbowe katika jambo hili kwa sababu ni kweli kabisa vijana hawa na hasa wa kizazi hiki wamekuwa na mawazo vichwani mwao kuwaona wazee hawana akili. Vijana hawa ni wale wanaojiona wasomi wametoka vyuoni juzijuzi tu lakini kila kitu wanajiona wanajua wao.Na hili hatuongelei kwenye siasa tu ni katika kila fani ya maisha .Ukija kwenye demokrasia wao ndio wanaoijua zaidi wazee ni mbumbu tu,Ukienda kwenye fani nyingine huko utasikia wanasema wazee wanaharibu tu na wameshakaa sana watuachie nafasi.Na unapofanya kazi nao vijana hawa utagundua kuwa wengi wao zaidi ya asilimia 95 hawajui lolote zaidi ya kuchezacheza na Computer tu,huko ndio wamebobea.Wakiachiwa kazi bila ya usimamizi wa wakongwe matokeo yake ni madudu matupu.
Kizazi hiki cha SHISHA na BANGI kielewe kuwa bila uwepo wa wazee waliosimama barabara na kuhakikisha kuwa mambo yanaenda sawa, wasingeipata hata hiyo nafai ya kupanua midomo yao kwa sasa.
Kwa hiyo niwaambie vijana kuwa Wazee wapo na wataendelea kuwepo na wataondoka kwa taratibu zinazoeleweka na vilevile muwe na adabu na heshima kwa wazee wenu.
 
Back
Top Bottom