Mbowe amepoteza sifa za kuendelea kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA

mleta uzi alikuwa na mawazo constructive lakn watu wamekuwa washabiki zaid na ndio ninpoona ccm itaendelea kutawala.sis tuko bize kujibu hoja mitandaoni wao wanaenda vijjn kwa wapiga kura

Kwa CDM yamepita sasa imebaki kwa maccm,EL.Cta,Mkyembe,ZZK(atakaribishwa kundini tu muda si mrefu)M'Kamba na kila anayebalehe huko anaona anafaa.Hapo ndipo CDM atakaponyakua nchi kama Tai anyakuavyo mzoga.
 

Mi nadhani hoja ya kung'ang'ania ingekuja kama, Muda wa Uchaguzi ungefike, halafu watu wakanyimwa wazi wazi fursa ya kuchukua form za Kugombea Uenyekiti.
Au Mwenyekiti aliyepo angeshindwa uchaguzi halali halafu akafanya hila kubaki madarakani.

Mi sidhani kama kuna mtu yeyote mwenye akili timamu anaweza akaangalia tu na kucheka huku anaona wazi wazi kuwa kuna mtu anatengeneza personal mechanism nje ya utaratibu wa Katiba wa kutaka Madaraka.

"Civilization starts at home"
Je, wewe ungekuwa ni Mwenyekiti uliyepigiwa kura wa Kikundi chochote halali, ungependa kufanyiwa hila za kuondolewa madarakani bila sababu za msingi, na huku uliapa kuitetea katiba ya kikundi hicho? Ask yourself before you judge others!
 
Zitto aanika 'siri' za Mbowe: - Adai mwaka 2010 Mbowe alipewa
Milioni 200 na Mkono kwa ajili ya
Kampeni ya Dr. Slaa na Rostam
Aziz alimpa Milioni 100
- Mbowe asema "Kupewa pesa na
Kikwete au CCM si tatizo lakini unapewa pesa kwa sababu zipi,
kwa malengo gani?"
 

Wakati mwingine kunakuwa na hoja ambazo kumradhi zinakosa nguvu ya ushawishi, Kama Dr Slaa alimtaja "Mr Hand" a.k.a "Mr Arm" katika List Of Shame ya Mafisadi 11, leo iweje tena "Mr hand" anatoa Millions kumkampenia Dr Slaa? This is only possible in the country where people cant differentiate black and white!!!!
 
W. J. Malecela
Mkuu hapa umeonyesha kukomaa kisiasa; hiki ulichoandika ni mistari michache yenye kubeba ujumbe mzito!
 
Last edited by a moderator:
Wajinga wenzako watakuunga mkono lakini kwa hakika hata mamako hakubaliani na upumbavu wako,achilia mbali mkeo/mmeo.

asieelewa akajihisi anajua humuona anayejua ni mjinga.
Saikolojia yangu inasema ata ukimsikiliza kichaa akiongea kunabaadhi ya vitu vitakua vya msingi. Vipi kuhusu Zitto? Mbowe ajipime na akubali kutafuta mwaminifu ampe chama
 
Kuna tuhuma nyingi sana zimeelekezwa kwa mwenyekiti wetu. Kwa haraka haraka tu ni hizi zifuatazo:

1. Anatumia madaraka yake vibaya ikiwa ni pamoja na kujivinjari na "vidosho"
2. Dikteta (Mbabe)
3. Inasemekana mkataba wa nyumba anayotumia kwa shughuli zake za kibiashara una utata.
4. Aliwahi kupokea fedha zisizoeleweka eleweka dhumuni na matumizi yake kutoka kwa makada wa chama kingine
5. Kuna tetesi kuwa anampango wakutaka kuwa mwenyekiti wa chama chetu wa maisha
6. Fedha ambazo zingezanzisha chombo cha habari cha chama alizitumia kuanzishia chombo binafsi cha habari nk nk nk.

Mpaka naandika ujumbe huu hakuna maelezo yanayojitosheleza" kutoka kwa mwenyekiti au kurugenzi yetu ya habari kuhusu hizi tuhuma. Kama kuna maelezo ya "kutosha", naomba radhi kwa kutokuwanayo.

Hizi tuhuma zote ni tofauti kabisa na misingi ya chama chetu na yale tunayoyasema majukwaani au bungeni kwa kupitia viongozi wetu. Ni mambo ambayo tumekuwa tukiyalalamikia dhidi ya viongozi waliopo madarakani. Wakati mwingine tumewataka wahusika wawajibike kwa tuhuma zinazofanana na hizo ili kutekeleza dhana ya utawala bora. Na tumediriki kuwaita mizigo kwa sababu ya tabia na mambo yao ambayo hayana tija kwa taifa. Kama mwenyekiti wetu anatuhumiwa kwa yale yale ambayo tunayapinga na ni kinyume na misingi ya chama chama. Na yanaashiria kutokuwa na tija kwa chama. Kwangu mimi huu ni USALITI na UHUJUMU wa chama chetu na ni mzigo mzito pengine kuliko ule wa mnyamwezi ambao inabidi tuutue. Ni muhujumu kwa sababu hayo ni mambo yanayotishia ustawi wa chama.

Nashauri, kama ambavyo chama chetu kimekuwa kikishauri mizigo iliyopo madarakani:

1. Kwa uungwana mwenyekiti akae pembeni kwa hiari yake japo kwa muda kupisha uchunguzi huru wa tuhuma dhidi yake

2. Itakuwa ni mfano wa kuigwa na vyama vingine endapo mwenyekiti atajiudhuru kabisa kwa sababu hizi tayari ni kishfa nzito kwa kiongozi.

3. Kama la kwanza na la pili yatamshinda mwenyekiti, chombo husika ndani ya chama kimsimamishe mwenyekiti ili kupisha uchunguzi.

4. Matokeo ya uchunguzi yawekwe bayana

5. Ikithibitika, mwenyekiti achukuliwe hatua stahiki

Ni matumaini yangu haya yakifanyika yatadhihirisha kweli chama chetu kina mpango wa kujitofautisha na vyama vingine na tutaaminika kwa umma kweli tumekuesudia kuleta mabadiliko. Na kama hayatafanyika watu hawatatuamini juu ya yale tuyasemayo na yaliyopo kwenye makablasha ya chama. Matokeo yake watatuadhibu kwenye kura.

Wasalaam
 
Wanasema Chadema haisiti kufanya maamuzi magumu kwa kuwashughulikia makada mizigo huku wakitoa mifano ya akina Zitto,Mwigamba na Kitila haya sasa na Mwenyekiti huyooo naye ndani ya nyumba ningependa kuona kama Chama kitafanya maamuzi magumu dhidi ya huyu GAMBA,NOT!
 

Jipe moyo,chadema ndio kivuli mkiti ameingia deal na viongozi wa ccm kapewa mihela na mikataba ya n.h.c na nssf,nyie hamjui, labda kaiuza chadema,kazi yenu ni matusi na maneno ya laana.Mtegemeeni Mungu sio binadamu kwa sababu binadamu ni dhaifu
 
sio huyu huyu mbowe ndie alietoa kipengele cha uongozi bila kikomo kisirisiri ili asing'atuke?
 
Hujasema Kwanini Mbowe amepoteza uhalali wa kuwa mwenyekiti wa Chadema

Mbowe uwezo wake wakufikiri umefikia mwisho hawezi kuwa new ideas and innovations za kuikabili CCM. Pia hivi sasa ukiacha kukailiana na Zitto anatakiwa kushughulikia matatizo ya ndoa yake ikiwa ni pamoja na kuandaa uhalali wa motto aliyezaa na Joyce Mukya.
 

wenye akili wanamuelewa mbowe ndani na nje ya Chama. Tabia ya CCM kushika wenyeviti wa nyama vya Wafanyakazi kama CWT, TUGE NA TUCTA ni hivyohivyo hadi kwa vyama vya siasa vyenye nguvu.
LEMA alikiri kukaa kikao na Jk Ili aamie CCM na agombee ubunge arusha kupitia CCM ila akawaruka.
Kama ni kweli ajiulize mbowe ameshakaa vikao vingapi vya siri na Mbowe au Simu za siri.
 
Muruke,mupe,muruke,mupe kafwanta kabaridi,wewe unaitwa nani? Massawe huyo muruke na wewe Rwe....mupe kasafwari kabaridi,nalabuk
 

Labda kwa kuwa Chama ni cha mkwewe kapewa akikiacha ataambiwa aache na Mke wake.
 
unaju nilianzisha hoja nyingi kuwafungua watu juu ya mbowe name zit to name walivyogeuza siasa mitaji zikafutwa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…