Pre GE2025 Mbowe ampinga Profesa Kabudi mbele ya halaiki; 'hatuwezi jadili mambo yale yale kwa miaka 30'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Baadhi ya hawa watu hata hawana aibu mbele za watu. Profesa mzima unatetea vipi hayo ya Ujerumani ndiyo yawe ya hapa, sisi hatuna akili ya kutengeneza tunachotaka kutokana na mazingira yetu?
Kwa nini tutazame ya Ujerumani?

Wasomi wetu hawana maana wanashindwa kutumia usomi wa nadharia kutatua matatizo ya nchi yao kama Tanzania, kazi yao kubwa kutema nadharia walizosoma bila kutoa ufumbuzi wa tatizo liwe la kisiasa, kikatiba, kiuchumi na kijamii wasomi hawana mchango.
 
Wasomi wetu hawana maana wanashindwa kutumia usomi wa nadharia kutatua matatizo ya nchi yao kama Tanzania, kazi yao kubwa kutema nadharia walizosoma bila kutoa ufumbuzi wa tatizo liwe la kisiasa, kikatiba, kiuchumi na kijamii wasomi hawana mchango.
Wasomi wako hivyo kwa sababu ya CCM ndivyo inavyotaka wawe.

Leo hii akitokea kiongozi mzalendo wa kweli, na kuwaunga mkono wasomi watumie taaluma zao kuliendeleza taifa hili, utaona mabadiliko makubwa. Badala yake, wasomi hawa sasa wanajidhalilisha kabisa bila ya aibu, kama huyu Kabudi!
 
09 May 2024
SUSAN KIWANGA AWAWAKIA CCM :NYIE MUNGU ANAWAONA / BORA MNINYANGANYE MAIKI ILA UKWELI NITAONGEA"


View: https://m.youtube.com/watch?v=2OGOvOkKJYU

SIKU YA PILI MKUTANO WA KITAIFA KUTAFAKARI NA KUJENGA UELEWA JUU YA SHERIA ZA UCHAGUZI ZILIZOPITISHWA

Susan Kiwanga hiki chama dola kongwe kilipora mchakato mzima wa uchaguzi 2020 bila aibu yoyote hii haijapata kutokea tangu CCM waanze wizi wa kura ....

Hivi muda huu wakurugenzi wote wamejifungia mjini Kibaha mkoa wa Pwani wakipanga nini wafanye 2025 .. kwa maana nyingine wanatusanifu na kutuona sisi wapumbavu tuliopo katika kongamano hili tukijadili Tume Huru na Uchaguzi wa Haki anasema kwa uchungu kamanda Susan Kiwanga aliyekuwa mbunge wa CHADEMA

Anaongeza kuwa muda huu wameanza kuboresha daftari na wasimamizi wa zoezi hilo ni makatibu tarafa ambao wote ni CCM na vijana wanaoomba kazi ya zoezi hilo wanaambiwa kama siyo CCM huwezi kuruhusiwa kupewa kazi bila kiongozi wa CCM kukubeba .... anabainisha yanayoendelea sasa huko katika ngazi za tarafa nchi nzima kamanda Susan Kiwanga

Vituo vya kupiga kura sasa kitakuwa kituo kimoja tu katika kila kijiji chenye vitongoji kadhaa sasa kwa mfano kule kwetu Mlimba Morogoro itabidi wapiga kura kusafiri hadi umbali wa kilometa 20 kupiga kura ndani ya kijiji kwani vitongoji viko mbalimbali anasema Susan Kiwanga na kuongeza hizi zote ni dalili ya CCM kuvuruga uchaguzi wa 2024 / 2025 kama ilivyo mazoea ya chama dola kongwe CCM ...Na hali ya vitongoji katika vijiji nchini kote Tanzania inafanana na ya kwetu Mlimba Morogoro na kwa hali hii CCM tayari inafanya ukatili kwa raia wake....
 
Gorge Bush senior wa Republican Aliangushwa na Bill Clinton wa Republican. Usitake kuleta upotoshaji wa kijinga wakati huna ujualo.
 
Hii dhambi ya mauti alafu kuna wanaojiita viongozi wa dini wanawaombea , sijui wanasema ni wateule wa mungu sijui takataka gani, Mungu afanye yake !
 
Hii dhambi ya mauti alafu kuna wanaojiita viongozi wa dini wanawaombea , sijui wanasema ni wateule wa mungu sijui takataka gani, Mungu afanye yake !

Hakika chama dola kongwe kimeishiwa mbinu hatujui baada ya kuvuruga mchakato na mfumo mzima wa uchaguzi nini watafanya 2024 / 2025 hawa CCM siyo wa kuaminiwa kabisa
 
Joseph Selasini - Tayari tumepigwa chenga ya mwili sheria hizi haziwezi kutumika 2024 / 2025


View: https://m.youtube.com/watch?v=banPfKHj3cE
Selasini kiongozi wa NCCR Mageuzi amesema hayo huku Profesa Palamagamba Kabudi kada wa CCM akitikisa kichwa kuafiki mchakato wa sheria mpya za uchaguzi kutumika 2024 / 2025 haiwezekani .....
 
Ukimsikiliza Mbowe unaelewa kwa kina namna ambavyo Tanzania yetu imemezwa na jinamizi la watawala ndani ya CCM

Ni busara sana kudai Katiba Mpya la sivyo hakutakuwa na maana ya kufanya chaguzi
 
Mh Mbowe, kaongea vitu vya MSINGI sana, ila CCM hawana AIBU wala HAYA, wataendelea kufanya maupuuzi yale yale, ili yabaki MADARAKANi..bila Wapinzani kubadili MBINU na kuwa BOLD, CCM hawatatoka madarakani...
Ongezeni nguvu CDM, maandamano, fikeni huku kwenye msingi lakini msisahsu TV na Radioya Chama
 
Unaposema bila wapinzani kubadili mbinu unafikiri nchi ni ya wapinzani peke yao?
WATANGANYIKA wote wabadilike, wache kutumiwa kama pedi na kondom, unanyingwa , unaporwa na bado unamkumbatua mtesi wako?
Hakuna mkono wa chuma unao ondoka hivi hivi!
 

SIKU YA PILI MKUTANO WA KITAIFA KUTAFAKARI NA KUJENGA UELEWA JUU YA SHERIA ZA UCHAGUZI ZILIZOPITISHWA

Prof. Palamagamba Kabudi atafuta uhalali wa hali iliyopo kwa kujibanza nyuma ya katiba, kuwa siyo sisi chama kongwe dola tunaitaka hali hii ila ni hii katiba niliyonayo mkononi ndiyo inatuchelewesha siyo sisi CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=xyn2C1c5McY
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…