Pre GE2025 Mbowe ampinga Profesa Kabudi mbele ya halaiki; 'hatuwezi jadili mambo yale yale kwa miaka 30'

Pre GE2025 Mbowe ampinga Profesa Kabudi mbele ya halaiki; 'hatuwezi jadili mambo yale yale kwa miaka 30'

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

SIKU YA PILI MKUTANO WA KITAIFA KUTAFAKARI NA KUJENGA UELEWA JUU YA SHERIA ZA UCHAGUZI ZILIZOPITISHWA


Andrew Chenge akiri kuwa Uchaguzi wa 2019 / 2020 walihusika ktk uchafuzi , hivyo naelewa mkiona kamba ya katani mnaona nyoka hata leo 2024 / 2025 ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=tYSTG-AWM6c

Amesema hayo Mwanasheria Mkuu wa Serikali mstaafu Andrew Chenge kwenye Mkutano wa Kitaifa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za Uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa wa Mwaka 2024 na uchaguzi mkuu wa Mwaka 2025 ulioandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania tarehe 9 Mei 2024.
 

MKUTANO WA KITAIFA KUTAFAKARI NA KUJENGA UELEWA JUU YA SHERIA ZA UCHAGUZI ZILIZOPITISHWA​

Wadau mbalimbali wa masuala ya kisiasa hapa nchini wameoneshwa kutoridhishwa na mabadiliko yaliyofanyika kwenye sheria za uchaguzi, kwa kile walichodai kuwa bado hazitoi mwanga kamili wa kuwa na chaguzi huru na za haki.

Sheria hizo ni Sheria ya Uchaguzi wa Rais, Wabunge na Madiwani namba moja ya mwaka 2024, Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi namba mbili ya mwaka 2024, Sheria ya Marekebisho ya Sheria za Vyama vya Siasa namba tatu ya mwaka 2024 na Sheria ya marekebisho ya sheria mbalimbali namba nne ya mwaka 2024.

Madai hayo yametokana na kile kilichoelezwa kuwa Serikali imetupilia mbali baadhi ya mambo ambayo wadau hao waliyapendekeza yawepo kwenye sheria hizo, lakini pia kitendo cha maandalizi ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa kushikiliwa na Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) pekee pasipo kuwashirikisha wadau wengine.

Haya yote yamebainishwa jana Mei 8, 2024, wakati wa mkutano wa kitaifa wa kutafakari na kujenga uelewa wa pamoja juu ya sheria za uchaguzi zilizopitishwa kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa baadaye mwaka huu na uchaguzi mkuu wa hapo mwakani.

Mkutano huo wa siku mbili ambao umeendelea pia leo hii umeandaliwa na Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) na kufanyika katika ukumbi wa mikutano wa maktaba ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ukiwakutanishwa wadau mbalimbali kutoka kwenye vyama vya siasa, asasi za kiraia, mabalozi pamoja na waandishi wa habari.

Baadhi ya mambo ambayo wadau hao wameyataja kuwa yametupiliwa mbali ni pamoja na pendekezo la kufanyika kwa marekebisho madogo kwenye katiba ya mwaka 1997, kuruhusiwa kwa mgombea binafsi, matokeo ya Urais kupingwa mahakamani pamoja na viongozi wa umma wanaoteuliwa na Rais kutokuwa sehemu ya tume ya uchaguzi.

Wadau wanakosoa uchaguzi Serikali za mitaa kuendelea kusimamiwa na Wizara ya Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), licha ya Sheria ya Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi iliyopitishwa kueleza kuwa kuwa tume hiy ndiyo ambayo itakuwa na wajibu kusimamia uchaguzi.

“Serikali haikuona umuhimu wa kufanya mabadiliko madogo [ya katiba] kwa hivi sasa,” anasema Profesa Ibrahim Lipumba ambaye ni Mwenyekiti wa TCD. “Ilipeleka miswada mitatu bungeni ambayo baada ya mijadala na marekebisho ilipitishwa na kuwa sheria.”

“Sheria ambayo imepitishwa inasema kwamba jukumu la Tume Huru ya Uchaguzi ni kusimamia uchaguzi wa Serikali za mitaa, sasa hili likoje kwamba sheria tayari imepitishiwa lakini uchaguzi wa Serikali za Mitaa utasimamiwa na TAMISEMI? Labda pana maelezo ya namna gani katika kipindi hiki cha mpito?” Alihoji Profesa Lipumba.

Anna Henga ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Haki za Binadamu na Demokrasia (LHRC). Akitoa mada kwenye mjadala huo ameeleza kwamba kwa mujibu wa uchambuzi wao walioufanya sheria za uchaguzi zilizopitishwa zimebeba asilimia 30 tu ya walichukuwa wakikitaka.

“Kwa hiyo kama [sheria za uchaguzi] zingeweza kuleta mabadiliko ya 15 ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, kubadilisha kidogo na kubadilisha baadhi ya vitu kwenye Katiba tungeweza kupata matokeo makubwa zaidi.”

“Sisi kule ofisini kwetu tulikuwa tunasema hapa tumepata kama asilimia 30 tu ya tulichokuwa tunakitaka asilimia 70 bado. Kwa hiyo kama tungeweza kutaka kufikia hiyo [asilimia] 70 angalau tungeweza kuibadilisha katiba ingeweza kutusaidia sana.”

Madai haya ya Henga yametokana na kile alichoeleza kuwa Serikali haijapeleka bungeni muswada wa Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, kitu ambacho walikuwa wamekipendekeza lakini pia Serikali haijatekeleza baadhi ya maamuzi ya mahakama kwenye kesi mbalimbali za kimkakati.

Baadhi ya maamuzi hayo ni pamoja na wafungwa kupiga kura, kuwepo kwa mgombea binafsi na kutokutumia wakurugenzi wa halmashauri kwenye uchaguzi.

Mifumo haiakisi

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, yeye ameeleza kuwa mabadiliko kwenye sheria hizo yaliyofanyika kwenye sheria za uchaguzi hayaakisi mifumo ya uchaguzi iliyopo kutokana na madai yake ya kuwa kila kitu bado kipo chini ya Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Mbowe anadai kuwa ikiwa imesalia miezi minne hivi sasa kuelekea uchaguzi wa Serikali za Mitaa, bado wao kama vyama vya upinzani hawajui kanuni zitakazotumika kwenye uchaguzi huo, kwani licha ya kuwa wao ni washiriki lakini wamekuwa hawashirikishwi kwenye hatua zozote.

“Tunakwenda kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa miezi minne ijayo hatujui kanuni, sisi ni washiriki, wanaojua ni Serikali na CCM, wanahodhi kila hatua,” anasema Mbowe.

“Sasa tukija kuangalia haya mabadiliko yanayotolewa hapa ni mapambo tu, hayajaweza kutibu majeraha yaliyokuwepo. Na Rais anatoka na kauli nzuri nzuri, kwamba tutakuwa na tume huru, tutakuwa na chaguzi huru ni vizuri, hata Magufuli alisema hivyo.”

“Mheshimiwa [Abdulrahman] Kinana naye amesema tutakuwa na uchaguzi huru viongozi wengi wa Chama Cha Mapinduzi wanasema tutakuwa na chaguzi huru. Tunashukuru kwa hayo matamko ya matumaini lakini je, kweli mifumo yetu ina akisi hivyo?

Hatujafika kikomo

Akijibu malalamiko haya ya wadau ambao moja kwa moja walielekeza shutuma zao kwa Serikali inayoongozwa na CCM kada wa chama hicho Profesa Palamagamba Kabudi ameeleza kuwa wao walisikiliza maoni ya wadau na mabadiliko yataendelea kufanyika kwani bado hayajafika kikomo.

Kabudi ameyataja baadhi ya mambo ambayo yalipendekezwa na yakaainishwa kwenye sheria hizo kuwa ni pamoja na suala la wagombea kupita bila kupingwa pamoja na Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi kufanyiwa usaili.

“Mawazo yote yaliyotolewa ni mawazo mazuri kwa sababu unapotaka kufanya maboresho ni lazima uwe tayari kusikiliza,” anasema Kabudi ambaye pia ni Mbunge wa Kilosa.

“Na kwa Chama cha Mapinduzi kimeamua kwa kuyakubali mengi yaliyokuja kutoka kwa wadau. Na yale ambayo yalionekana kabisa kwamba mwaka 2020 na 2019 yameleta shida hapakuwa na tashishwi katika kuyakubali.”

“Kwa hiyo kwa ujumla Chama cha Mapinduzi mabadiliko mengi yaliyofanyika [ni] mabadiliko ambayo hajafika ukomo na ni vizuri kabisa kama nilivyosema huo ni mchakato, ni mwendo, ni safari unamwagilia maji ili mmea ukue. Kwa hiyo yapo mengi yamefanyiwa kazi lakini hatua iliyochukuliwa ni hatua sahihi na mwendo sahihi.”

Matonyinga Makaro ni mwandishi wa The Chanzo kutoka mkoani Mwanza. Kwa mrejesho, anapatikana kupitia matonyingamakaro@gmail.com
 

SIKU YA PILI MKUTANO WA KITAIFA KUTAFAKARI NA KUJENGA UELEWA JUU YA SHERIA ZA UCHAGUZI ZILIZOPITISHWA

Prof. Palamagamba Kabudi atafuta uhalali wa hali iliyopo kwa kujibanza nyuma ya katiba, kuwa siyo sisi chama kongwe dola tunaitaka hali hii ila ni hii katiba niliyonayo mkononi ndiyo inatuchelewesha siyo sisi CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=xyn2C1c5McY


Prof. Palamagamba Kabudi analaumu utamaduni wa wanasheria Tanzania kutofanya rejea wakati wenzentu wanafanya, lakini amesahau hukumu za kesi nyingi nyingi za umma (Public Law) Tanzania hazikuwa zinachapishwa ili kuzuia umma kufanya uchambuzi wa hukumu za majaji katika mahakama zetu, je hilo lilitokana na uamuzi wa makusudi kuficha hukumu hizo ? Kwa manufaa ya nani ? Na kwa Sababu zipi

TOKA MAKTABA :

16 April 2024
Dar es Salaam, Tanzania

NGULI WA SHERIA WAKUTANA JUKWAA MOJA, UZINDUZI KITABU CHA MWAKA CHA KESI ZA UMMA 2022.. TANZANIA YEARBOOK PUBLIC LAW 2022

View: https://m.youtube.com/watch?v=aA9LchsP9uo

Majumuisho ya kesi mkakati zilizotolewa tangu miaka ya nyuma kuanzia 1983 hadi 2022 na maamuzi ya hukumu yakiangaziwa kwa kina kuona maamuzi ktk hukumu hizo

Ambazo Tanganyika Law Report walijitahidi kuchapisha zilizolenga kesi mashuhuri zilizowahi zilizosikilizwa Tanzania kwa ajili ya rejea kwa wadau wa sheria na umma kwa ujumla wanaotaka kufahamu kesi mkakati za masuala kama ya kisiasa, haki za binadamu, kijamii, kiuchumi.

Miaka 10 hadi sasa Tanganyika Law Report walikuwa hawajawahi kuchapa. Kazi data huwezi kuzipata katika mtandao wa TANZLII Home - TanzLII , hivyo kitabu hiki cha leo kitakuwa na mambo mengi mazito yaliyowahi kufika mbele ya mahakama zetu za Tanzania


Manguli wa sheria jaji mstaafu O Chande wa Tanzania,, Dr. Willy Mutunga – Chief Justice Republic of Kenya, (2011-2016) Jenerali Ulimwengu, prof. Issa Shivji na wengine wanatoa maoni ya haki za jinai mapungufu ya 2019 ya Plea Bargain, Kesi ya Mtikila, Makampuni, maslahi ya umma kuanzia 1983 hadi 2022 na kitakuwa kinatoka kila mara kuangali jinsi zinavyoamuliwa na manguli hawa wa Yearbook kukosoa inapobidi ....
 

SIKU YA PILI MKUTANO WA KITAIFA KUTAFAKARI NA KUJENGA UELEWA JUU YA SHERIA ZA UCHAGUZI ZILIZOPITISHWA

Prof. Palamagamba Kabudi atafuta uhalali wa hali iliyopo kwa kujibanza nyuma ya katiba, kuwa siyo sisi chama kongwe dola tunaitaka hali hii ila ni hii katiba niliyonayo mkononi ndiyo inatuchelewesha siyo sisi CCM


View: https://m.youtube.com/watch?v=xyn2C1c5McY


17 April 2024

JUKWAA LA SAUTI YA WATANZANIA, MJADALA MPANA KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI

LIVE : TUNDU LISSU ANAONGEA KUHUSU SHERIA ZA UCHAGUZI, TEUZI ZA,WAJUMBE WA TUME HURU YA UCHAGUZI N.K NA JINSI RAIS ALIVYO NA MAMLAKA YA KUTEGUA


Sheria mpya za uchaguzi ya Tume Huru ya Uchaguzi athari zake kwa uchaguzi mkuu 2025 na ule wa serikali za mitaa pia vijiji mheshimiwa Tundu Lissu anaongezea kwa kina mazungumzo yake ya awali aliyofanya wiki iliyopita ktk kituo cha radio cha Clouds FM.

Leo mheshimiwa Tundu Lissu anajikita kwa kina zaidi kuhusu Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi jina lake tu lina mushkeli mkubwa na inakinzana na Katiba hivyo ni batili .......

katiba ambayo ni sheria mama haitambui Tume Huru ya Taifa Uchaguzi inapingana na jina la Tume ya Uchaguzi hilo ni la kwanza ... hivyo msidanganywe

Jina la Tume ya Uchaguzi ilianza kutumika 1961 (tanganyika constitution order in Council 1961) kufuatia amri ya Malkia au Mfalme wa Uingereza kupitia Privy Council ....

Katiba ya Jamhuri 1962 ikalirithi jina Tume ya Uchaguzi na mwaka 1965 Katiba ya Mpito ya Jamhuri ya Muungano mwaka 1965 na iliendelea hadi 1977 Tume ya Uchaguzi na hadi leo 2024 jina halijabadilika ......

Tundu Lissu anageukia sasa kuchambua ..... Tume Ya Uchaguzi na kinga ya kushitakiwa ni kuwa ..... haitafuata maelekezo au amri ya mtu yeyote. Tume ya Warioba olisema hiyo siyo kweli kwa Tume ya Uchaguzi ni ya Rais na inateuliwa na kutenguliwa na Rais hivyo Tume ya Uchaguzi hupokea amri na maelekezo kutoka kwa mwenye Tume ya Uchaguzi ambaye ni Rais ... juzuu ya Tume ya Warioba imesisitiza hivyo Tume ya Uchaguzi haina uhuru katika uwajibikaji ...


Uundwaji wa majimbo ya uchaguzi Tanzania ni tofauti na nchi zingine, maana Tanzania majimbo yanaibuliwa huku kukiwa na nia ya kushinda uchaguzi ..... na mwenye maamuzi ya mwisho kuhusu mipaka na majimbo mapya yapo chini ya rais

Rais ndiye anayeitengeneza Tume ya Uchaguzi na kuondoa wajumbe wa Tume. Rais ndiyo anaye toa na kutwaa haya madaraka ni absolute power hivyo Tume hii ni ya Rais pekee...
 
Hawa watu hawalitaki mema taifa hili. Hawa wanatafuta damu za watu zimwagike, ndipo wajue kuwa wanayofanya ni hatari kwa nchi yetu.
Halitakuwa jambo jema kushikana makoo sisi kwa sisi waTanzania. Hawa wapuuzi ndio inafaa watafutiwe njia ya kutiwa adabu.
Wamekosa ustaarabu hao watu.
Ila wajue tu hakuna marefu yasiyo na mwisho..

Wangekuwa na hekima walau kidogo wangeruhusu sanduku la kura kuamua kwa haki. Bahati mbaya sikio la kufa halisikii dawa
 
Back
Top Bottom