Mbowe anaungwa mkono na Wajumbe wapiga kura wengi ndani ya CHADEMA, Lissu anaungwa mkono na umati mkubwa wa wapiga kelele

Mbowe anaungwa mkono na Wajumbe wapiga kura wengi ndani ya CHADEMA, Lissu anaungwa mkono na umati mkubwa wa wapiga kelele

Kwamba kama sio katiba ya chama watu wanaomuunga mkono Lissu wangepiga kura wangemshinda Mbowe...vizuri!.
Na siasa ni watu, hivyo wajumbe watakuwa ni watu wajinga wakimchagua Mbowe ambaye hana watu wengi kuliko Lissu.
Lissu ni mtaji uchaguzi mkuu ujao!.
Mbowe ni liability!.
 
Usichokijua ni Kwamba

Team Mbowe ina watu wazito wachache (Wapiga kura)
Team Lisu ina watu wengi (Wasiopiga kura)

Team Mbowe inauhakika wa Ushindi kwenye box la kupiga kura ndio maana hawana kelele
Team TAL haina watu kwenye kura ndio maana wanalazimisha Mbowe ajitoe
Umetumia kipimo gani?
 
Ni hivi, kwa sasa wakati ndio utaamua hatima ya cdm, hao wapiga kura wengi watakapoamua kinyume na mahitaji ya nyakati watakiona cdm ikiwa kama CUF. Wakati ni ukuta, muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umepita.
Uchaguzi huru na wa haki maana yake ni nini kama kundi moja linaingia kwenye uchaguzi kwa vitisho? Acheni wapiga kura watumie uhuru kufanya maamuzi yao. Vitisho vya kuua chama havimjengi hata huyo mnayempigia chapuo.
 
Usichokijua ni Kwamba

Team Mbowe ina watu wazito wachache (Wapiga kura)
Team Lisu ina watu wengi (Wasiopiga kura)

Team Mbowe inauhakika wa Ushindi kwenye box la kupiga kura ndio maana hawana kelele
Team TAL haina watu kwenye kura ndio maana wanalazimisha Mbowe ajitoe
Siku ukugundua kuwa hata Benson kigaila na j. Myika kwa siri watampigia lissu si utajinyonga
 
Lissu havuki 30%, amini usiamini. Tutarudi hapa baada ya uchaguzi
Kifupi tambua Lissu atashinda kwa kishindo elewa hivyo na kama hutaki kuelewa hivyo subili hiyo trh uje urejee hiyo kauli yako

Hayupo mwanachadema awe mwenyewe,katibu au mjumbe wa mkutano mkuu taifa ambaye yeye chama ni Imani atakwenda kumpigia kura MBOWE.

Hata uchaguzi uliopita tulitamani saana HECHE agombee uenyekiti lakini wakaishia kuchukua fomu ambao hawana sifa Ili washindane na MBOWE

Mwaka huu imekuwa kama MUNGU tu kasaidia kachukua fomu mtu ambaye sifa zake tulizihitaji tangu uchaguzi uliopita anakuja patikana sasa

Nikuambie tena awamu hii MBOWE anapambana na wakati ambao haupo kwa upande wake
 
Endelea kuota ndoto za mchana, ila ukiona choo tu AMKA. Usije kata gogo kitandani
 
Friends, ladies and gentlemen.

Kwa kifupi kabisa, ukipima kwa jicho la rohoni kabisa, numbers of votes zinamfavor chairman Mbowe, huku useless mass popularity ikimfavor vice chairman Lisu, ikiwa uchaguzi wa ndani wa chadema utafanyika mwaka huu 2024 au 2025.

There is no way Lissu can beat Mbowe in the ballot box, because Mbowe has real numbers, than Lisu has.

Uchaguzi ni mchakato unaozingatia na kutegemea zaidi numbers kwa washindani ili kushinda.

Ni dhahiri kanda za Pwani, Nyasa, Victoria na Kaskazini ni ngome imara za mwenyekiti wa sasa wa chadema Taifa, na tayari katika ujumla wake zimejipambanua kumuunga mkono.

Kanda ya kati, nadhani sote tunafahamu uhasama kati ya Lissu na Kigaila. Ni majirani wasioelewana hawa.Tuchukulie kanda hiyo itakua imegawanyika.

Kanda ya Viktoria kwa kamanda Ezekia Wenje, kama kawaida Taifa zima linafahamu, huyo ndie makamu mwenyekiti wa chadema Taifa ajae, ambae pia anamuunga mkono Dr. Freeman Aikaeli Mbowe kua mwenyekiti wa chadema Taifa.

Nguvu ya Ezekia Wenje kisiasa ndani ya chadema, imemlazimisha na kumtoa mtu maarufu sana ulingoni kwenye kinyang'anyiro cha uongozi wa chama Taifa.

Kanda za Serengeti, Magharibi, Kusini n.k ni kama wanatafuta platforms na namna ya kujipambanua wako upande wa Mbowe au Lisu.

Kwa ujumla, mizizi ya mwenyekiti wa chadema Taifa wa sasa ni mirefu, imara na imejikita sana ndani ya chadema. Kuing’oa yahitajika mipango mikakati ya kisayansi, Lakini pia nguvu, bongo kali, ushawishi wa hali na mali na jitihada za ziada. Asilimia kubwa ya viongozi wa chadema wa kanda, mikoa na wilaya wanatokana na mapendekezo na baraka za mwenyekiti wa chadema wa sasa.

Kwa maoni na mtazamo wako kisiasa, kati ya kanda 10 za kiutawala zilizopo chadema, unadhani ni kanda zipi zinanaweza kuunga mkono azma ya Tundu Lisu kua mwenyekiti wa chadema Taifa badala ya Freeman Mbowe?🐒

Mungu Ibarki Tanzania
Hao unaowaita wapiga kelele ndio hao wanaopiga kura za ubunge,udiwani na uraisi.
Hao wajumbe tu wa mkutano mkuu hawana uwezo wa kumshindisha mtu hata udiwani tu.
Muda utazungumza
 
Kweli Watanzania kuna matatizo sana kwenye jamii zetu,yaani leo tunaitwa wapiga kelele kwa sababu tu tunatofautiana na nashangaa sana watu kuwa chawa tu kwa kiongozi chama cha upinzani, vipi tukose machawa kwenye serkali
 
Hao unaowaita wapiga kelele ndio hao wanaopiga kura za ubunge,udiwani na uraisi.
Hao wajumbe tu wa mkutano mkuu hawana uwezo wa kumshindisha mtu hata udiwani tu.
Muda utazungumza
kwahiyo gentleman,
unadhani hao wajumbe zaidi ya elfu1 wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wanaenda kumchagua Rais, diwani au mbunge wa chadema Taifa, right?

ni muhimu zaidi kutuliza bongo gentleman kwenye mambo haya 🐒
 
Machawa ya mzee Mbowe hayana hata aibu ,hivi jaribuni kuweka wasifu wa msomi Lissu na wasifu wa mzee Mbowe ndio mtajua kuwa makelele yote mnayorushia Lissu ni kwa ajili ya jambo moja tu, Lissu ni mkuwbwa mno kwa mzee Mbowe kwa Fikra ,mawazo na akili kwa ujumla .Acheni uwoga jamani ,kama mnavyojiita cham cha demokrasia ni wakati wa kuthitisheni hilo na si porojo.

Anao wajumbe????
 
Back
Top Bottom