Mbowe anaungwa mkono na Wajumbe wapiga kura wengi ndani ya CHADEMA, Lissu anaungwa mkono na umati mkubwa wa wapiga kelele

Kwamba kama sio katiba ya chama watu wanaomuunga mkono Lissu wangepiga kura wangemshinda Mbowe...vizuri!.
Na siasa ni watu, hivyo wajumbe watakuwa ni watu wajinga wakimchagua Mbowe ambaye hana watu wengi kuliko Lissu.
Lissu ni mtaji uchaguzi mkuu ujao!.
Mbowe ni liability!.
 
Umetumia kipimo gani?
 
Ni hivi, kwa sasa wakati ndio utaamua hatima ya cdm, hao wapiga kura wengi watakapoamua kinyume na mahitaji ya nyakati watakiona cdm ikiwa kama CUF. Wakati ni ukuta, muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa cdm umepita.
Uchaguzi huru na wa haki maana yake ni nini kama kundi moja linaingia kwenye uchaguzi kwa vitisho? Acheni wapiga kura watumie uhuru kufanya maamuzi yao. Vitisho vya kuua chama havimjengi hata huyo mnayempigia chapuo.
 
Siku ukugundua kuwa hata Benson kigaila na j. Myika kwa siri watampigia lissu si utajinyonga
 
Lissu havuki 30%, amini usiamini. Tutarudi hapa baada ya uchaguzi
Kifupi tambua Lissu atashinda kwa kishindo elewa hivyo na kama hutaki kuelewa hivyo subili hiyo trh uje urejee hiyo kauli yako


Hayupo mwanachadema awe mwenyewe,katibu au mjumbe wa mkutano mkuu taifa ambaye yeye chama ni Imani atakwenda kumpigia kura MBOWE.

Hata uchaguzi uliopita tulitamani saana HECHE agombee uenyekiti lakini wakaishia kuchukua fomu ambao hawana sifa Ili washindane na MBOWE

Mwaka huu imekuwa kama MUNGU tu kasaidia kachukua fomu mtu ambaye sifa zake tulizihitaji tangu uchaguzi uliopita anakuja patikana sasa

Nikuambie tena awamu hii MBOWE anapambana na wakati ambao haupo kwa upande wake
 
Endelea kuota ndoto za mchana, ila ukiona choo tu AMKA. Usije kata gogo kitandani
 
Hao unaowaita wapiga kelele ndio hao wanaopiga kura za ubunge,udiwani na uraisi.
Hao wajumbe tu wa mkutano mkuu hawana uwezo wa kumshindisha mtu hata udiwani tu.
Muda utazungumza
 
Kweli Watanzania kuna matatizo sana kwenye jamii zetu,yaani leo tunaitwa wapiga kelele kwa sababu tu tunatofautiana na nashangaa sana watu kuwa chawa tu kwa kiongozi chama cha upinzani, vipi tukose machawa kwenye serkali
 
Hao unaowaita wapiga kelele ndio hao wanaopiga kura za ubunge,udiwani na uraisi.
Hao wajumbe tu wa mkutano mkuu hawana uwezo wa kumshindisha mtu hata udiwani tu.
Muda utazungumza
kwahiyo gentleman,
unadhani hao wajumbe zaidi ya elfu1 wa mkutano mkuu wa chadema Taifa wanaenda kumchagua Rais, diwani au mbunge wa chadema Taifa, right?

ni muhimu zaidi kutuliza bongo gentleman kwenye mambo haya 🐒
 

Anao wajumbe????
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…