LGE2024 Mbowe anazungumza na Watazania muda huu makao makuu ya CHADEMA Dar es Salaam, akitoa tathmini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

LGE2024 Mbowe anazungumza na Watazania muda huu makao makuu ya CHADEMA Dar es Salaam, akitoa tathmini ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anazungumza na Watanzania muda huu kutoka makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huu muhimu, Mbowe anatarajiwa kuzungumzia masuala ya kisiasa, hali ya chama, na mustakabali wa taifa, huku akitoa mwongozo wa CHADEMA katika hatua zinazofuata kuelekea maendeleo ya demokrasia nchini.

Fuatilia hapa live akizungumza na watanzania kupitia Mkutano na waandishi wa Habari

Kwa niaba ya Kamati kuu ya CHADEMA, Freeman Mbowe, anatoa taarifa ya tathimini ya Kamati Kuu kuhusu Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika Novemba 27, 2024.

"Nimesimama hapa leo Jumanne Disemba 10, 2024 kwenye kikao cha wanahabari kwa niaba ya Kamati Kuu ya chama chetu (CHADEMA) kufikisha kwenu taarifa fupi ya tathimini ya Kamati Kuu kuhusiana na 'kilichoitwa' Uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika tarehe 27 Novemba 2024.

Natambua kwamba chama chetu kwa kipindi cha miaka saba (7) iliyopita kimepita chini ya tulichokiita mara nyingi 'bonde la uvuli wa mauti', kwamba wenzetu walio kwenye mamlaka walijaribu kila aina ya mbinu halali na haramu na nyingi zikiwa za haramu kuhakikisha kwamba wanauzika na kuuzima upinzani na demokrasia isishamiri katika nchi yetu, ni mwaka jana tu (2023) ambapo hatimaye tulirejeshwewa haki yetu ya Kikatiba ya kufanya shughuli za Kisiasa na baada ya hapo tumeanza program mbalimbali katika Taifa ikiwemo kufufua upya misingi ya Chama chetu katika maeneo mbalimbali ya Taifa letu kwani tulikuwa tumeporomoshwa kutoka kile ambacho kilikuwa nafasi kubwa ya mageuzi na nafasi kubwa ya CHADEMA katika uongozi wa Taifa letu.

Kukusanya takwimu tu za uchaguzi wa Serikali za Mitaa imekuwa ngumu kwasababu unahusisha watu wengi sana. Hata Waziri mwenyewe wa TAMISEMI (Mohamed Mchengerwa) ambaye amekuwa akitoa takwimu mara kwa mara hajawahi kutoa data zinazohusiana na wajumbe wa serikali za vijiji au wajumbe wa serikali za vijiji mchanganyiko au wajumbe wa serikali za vijiji kundi la wanawake.

Waziri katika taarifa zote anazotoa pamoja na kuwa na Serikali yote na wao ndio waliosimamia Uchaguzi, hadi leo hajawahi kutamka takwimu zozote za waliogombea, waliopita kwenye Serikali yake na hata kwenye vyama vingine vya upinzani ambazo yeye ana dhamana ya kutangazia umma.

Hii inaonesha ukubwa wa takwimu ambazo zinahitajiwa kukusanya, kwahiyo sisi kama chama tulijaribu vilevile bila kukimbilia kuzungumza lolote, ilikuwa ni lazima sisi CHADEMA tujitahidi kukusanya data kadiri tuwezavyo, hata sasa hatujaweza kukusanya kwa asilimia 100 lakini bado tumeona tuna nafasi nzuri tunaweza kutoka tukazifikisha kwenu Watanzania.

Ambayo tumeyaona na ambayo tungependa kuyafikisha kwenu ni kama ifuatavyo; uchaguzi huu wa Serikali za Mitaa 2024 ulianza kuharibika katika hatua za kwanza kabisa ambapo baada ya kuwa tumetoka katika 'bonde la uvuli wa mauti'

Baada ya malalamiko mengi ya wadau ili tuweze kuwa na chaguzi zenye haki, zenye uhuru, zenye uwazi, lazima pafanyike mabadiliko ya msingi ya sheria za uchaguzi, mnakumbuka mambo haya yote yalisukumwa vilevile na hitaji kubwa la Katiba baadae ikaonekana Katiba inaweza kuwa vigumu kuipata katika ujumla wake basi tufanye tunachokiita mabadiliko madogo kuboresha sheria za msingi za uchaguzi, kuanzisha Tume Huru ya Uchaguzi ya kweli sio Tume Huru ya Uchaguzi ya jina, na mapendekezo kadha wa kadha yakawa yametolewa lakini kwa bahati mbaya wenzetu kwenye mamlaka kama kuna kilichopita basi ni asilimia tatu au asilimia nne, tukalazimishwa kuingai katika mzunguko mwingine wa uchaguzi, kimsingi tukitumai sheria zilezile na kanuni zilezile za zamani ambazo zilikuwa zimepakwa mafuta kuoneakana ni sheria mpya au kanuni mpya

Bunge mtakumbuka nalo lilipisha sheria ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kusimamia uchaguz wa serikali za mitaa lakini kwa makusudi kabisa serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na Bunge lake hawakutengeneza sheria wezeshi kwa hatua hii kuweza kukamilika kwa hiyo tukajikuta tunalazimisha kurudi katika uchaguzi tukitumia mfumo uleule wakitumia mamlaka na Wizara ya TAMISEMI kama ambavyo ilikuwa miaka ya nyuma.

Baada ya kutafakari matukio yaliyotokea katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa tarehe 27 Novemba, 2024, Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) imeazimia yafuatayo:

1. Kamati Kuu inatangaza kwamba uchaguzi wa tarehe 27 Novemba, 2024 haukuwa halali, huru na haki, bali ulikuwa ni uporaji na uhalifu wa kiuchaguzi.

2. Kamati Kuu inalaani vikali mauaji, vipigo, majeraha, na ukamataji wa wagombea, mawakala, viongozi na wanachama kabla, wakati na baada ya uchaguzi huo uliofanywa na Jeshi la Polisi.

3. Kamati Kuu inawapongeza wagombea wote waliojitokeza kugombea kupitia CHADEMA kwa ujasiri wao.

4. Kamati Kuu inawapongeza wadau wote waliojitokeza hadharani na kulaani uchafuzi wa uchaguzi huu, ambao ni hatari kwa uhai wa taifa letu, na inatoa rai kwa wadau wengine kusema hadharani misimamo yao kuhusu uchaguzi huu.

5. Kamati Kuu imethibitisha kuwa hakuna utashi wa kisiasa (political will) kutoka kwa Rais, viongozi na mfumo mzima wa Serikali ya CCM kuhusu uboreshaji wa mifumo ya uchaguzi ili kuleta chaguzi huru, haki na zinazoaminika nchini. Kauli zao haziaminiki tena, na ni lazima pawepo na maboresho ya kisheria kuhusu mifumo ya uchaguzi nchini.

6. Kamati Kuu inatoa wito kwa wadau wote nchini, wakiwemo vyama vya siasa, taasisi za dini, makundi ya kijamii, asasi za kiraia, wasomi, wakulima, wafanyabiashara, watu mashuhuri katika jamii, na wananchi wote kuunganisha nguvu za pamoja kudai mifumo huru ya uchaguzi nchini.

7. Kamati Kuu inawahimiza wananchi wa maeneo yote yaliyotangazwa na viongozi wa serikali za mitaa ambao walihusika na kuharibu uchaguzi wa tarehe 27 Novemba, 2024, kuwanyima ushirikiano viongozi na watendaji wa mitaa/vijiji na kata walioshiriki katika uhalifu huo.

8. Kamati Kuu itaendelea kushinikiza kudai Katiba Mpya na mabadiliko ya sheria na mifumo ya uchaguzi ili kuwezesha uchaguzi huru na wa haki kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025.

9. Kamati Kuu itaendelea kushinikiza kuundwa kwa Tume Huru ya Uchaguzi na watumishi wake waajiriwe na Tume, watakaosimamia uchaguzi wowote nchini kwa mujibu wa sheria, badala ya kuendelea na mfumo wa sasa wa kuazima watumishi wa Ofisi ya Rais (TAMISEMI) kusimamia chaguzi.

10. Kamati Kuu inatoa wito kwa jumuiya ya kimataifa na taasisi zake kuchukua hatua dhidi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuendeleza utawala wa kidikteta na kutokuwepo kwa uchaguzi huru, haki na wa kuaminika nchini.

Makamu Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu

Kuanzia 2015 hakuna ushindani, hawataki uchaguzi na ukweli wa Mungu ni kwamba sisi (CHADEMA) hatujashindwa uchaguzi na CCM tumeshindwa uchaguzi na Jeshi la Polisi, tumeshinda uchaguzi na Idara ya Usalama wa Taifa, tumeshindwa uchaguzi na mfumo mzima wa Tawala za Mikoa (TAMISEMI), Wakuu wa mikoa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi na watumishi wao wote sio CCM

Sasa maana yake ni kwamba tatizo letu la msingi ni mfumo wa uchaguzi, huu unaofanya Polisi, Usalama wa Taifa, JWTZ, watumishi wa umma badala ya kusmamia uchaguzi na kutenda haki wanakuwa wao ndio wapambanaji wa uchaguzi huo, na vilevile wanaamua nani anashinda, na tukisema tunaenda hivihivi itatokea tena mwaka ujao (2025), na itatokea tena kwenye uchaguzi wowote utakaofanyika

Ni tatizo la mfumo, na jibu la tatizo la mfumo ni 'No Reforms, No Election' (bila mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi, hakuna uchaguzi), sio kususia ni kuzuia uchaguzi hiyo ndiyo njia
 
Haya

Hapa KAZI TU 🐼

Mmetoka kwenye bonde la uvuli wa mauti au ndio mmeingia? Sijaelewa hiyo sentence
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anazungumza na Watanzania muda huu kutoka makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huu muhimu, Mbowe anatarajiwa kuzungumzia masuala ya kisiasa, hali ya chama, na mustakabali wa taifa, huku akitoa mwongozo wa CHADEMA katika hatua zinazofuata kuelekea maendeleo ya demokrasia nchini.

Fuatilia hapa live

Anaweweseka sana mwamba wa kaskazini dah maskini Freeman Mbowe, akina Lisu wanamuhangaisha sana mbaba wa watu jaman, hadi huruma aise 🐒
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anazungumza na Watanzania muda huu kutoka makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huu muhimu, Mbowe anatarajiwa kuzungumzia masuala ya kisiasa, hali ya chama, na mustakabali wa taifa, huku akitoa mwongozo wa CHADEMA katika hatua zinazofuata kuelekea maendeleo ya demokrasia nchini.

Fuatilia hapa live

CCM DAIMA
 
20240701_192614.jpg

Mbowe ni mwamba kabisa mtoto wa mjini amekuja mjini kutenengeza pesa. Aachi pesa.
 
Nilianza kuvutiwa na hiki chama nikiwa mdogo sana hadi leo hakishiki dola kwanini
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anazungumza na Watanzania muda huu kutoka makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huu muhimu, Mbowe anatarajiwa kuzungumzia masuala ya kisiasa, hali ya chama, na mustakabali wa taifa, huku akitoa mwongozo wa CHADEMA katika hatua zinazofuata kuelekea maendeleo ya demokrasia nchini.

Fuatilia hapa live

mbona kuna story tofauti
 
tushamzoea hana jipya kaona siku nyingi hajaongea kwenye press kwahiyo ni kawaida hakuna jipya
 
Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, anazungumza na Watanzania muda huu kutoka makao makuu ya chama hicho, Mikocheni, jijini Dar es Salaam. Katika mkutano huu muhimu, Mbowe anatarajiwa kuzungumzia masuala ya kisiasa, hali ya chama, na mustakabali wa taifa, huku akitoa mwongozo wa CHADEMA katika hatua zinazofuata kuelekea maendeleo ya demokrasia nchini.

Fuatilia hapa live

Tunasubiri kwa hamu kusikia kamanda amesema nini.
 
Back
Top Bottom