Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Baada ya Tundu Lissu kujitosa kugombea uenyekiti wa CHADEMA ni wazi kutakuwa na mchuano mkali sana endapo Mbowe naye ataamua kugombea tena nafasi hiyo. Huo ushindani hautakuwa na afya kwa CHADEMA zaidi sana endapo Mbowe atashinda tena, kwa mantiki hiyo ni vyema basi Mbowe akaamua au akashauriwa kutogombea tena nafasi hiyo kwa sasa.
Hofu kubwa ya Wanachedema imekuwa kupatikana mtu atakayemrithi Mbowe ambaye hawezi kununulika au kutumika na chama tawala kuihujumu CHADEMA, katika eneo hilo Lissu anatosha na hakuna mtu anayeweza kumtilia mashaka.
Mambo ya faida kwa Mbowe kutokugombea tena uenyekiti ni pamoja na kumaliza kelele za ukanda, uchagadema, uchawa na kung'ang'ania madaraka ambazo Mbowe na CHADEMA wamekuwa wakirushiwa. Japo ni hoja zisizo na mashiko au uhalisia wowote wa maana kwa CHADEMA lakini hazikipi CHADEMA sura nzuri kwa sababu siasa wakati mwingi ni kuhusu muonekano (perception) kwanza ndipo mambo ya sera, uhalisia na ukweli yanafuata.