Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Huu ni uongo mwingine. Mbowe hajalipwa fidia ya kukaa ndani. Badala ya kumuomba mtuhumiwa atoe ushahidi, mlitakiwa nyinyi mnaomtuhumu ndio muweke ushahidi unaowafanya kuamini hivyo. Hii ni character assassination 101. Insinuate vitu vya uongo bila ushahidi ukijua hamna namna ya ku prove otherwise.Ni wazi kuwa Mbowe alilipwa pesa nyingi inayotajwa kuwa ni fidia ya yeye kukaa gerezani kwa kesi ya kusingiziwa, na pia kwa kuharibiwa biashara zake.
Lakini kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, na kwaajili ya kuleta uwazi katika uongozi, na kuzuia fikra za pesa hiyo kuonekana kuwa ni hongo, Mbowe alistahili kuweka wazi juu ya malipo hayo yanayotajwa kuwa ni fidia.
Kuna wafanyabiashara wa kubadilisha fedha za kigeni ambao pesa zao ziliporwa, serikali iliamua kuwarudishia, na iliwekwa wazi, ilitangazwa na vyombo vya habari, na hakuna aliyeshangaa. Lakini hiyo inayotajwa ni fidia kwa Mbowe, imeendelea kuwa ni siri, jambo linalozua maswali mengi.
Si serikali wala Mbowe, ambaye yupo tayari kuweka wazi, kwanza kukiri kuwa Mbowe alipewa pesa na Serikali, na pili kuweka wazi hiyo fidia ilikuwa ya kitu gani.
Kama ni kwa kuwekwa gerezani bila hatia, kuna wahanga wengi wameyapitia hayo magumu. Lakini kuna familia zimepoteza wapendwa wao kutokana na vyombo vya dola, Lisu alipigwa risasi msululu. Hivyo kama Serikali iliamua kumlipa fidia Mbowe kwa sababu ya kumweka jela kwa kumwonea, basi na hawa wengine nao wana haki ya kuipata fidia hiyo, ikiwezekana hata iliyo kubwa zaidi kwa waliopoteza wapendwa wao na waliopewa ulemavu kwa kupigwa risasi.
OMBI:
Mbowe aweke wazi juu ya malipo aliyopewa yalikuwa ni fidia ya nini na nini ili kuua fikra za kwamba pesa hiyo ilikuwa ni hongo. Ikumbukwe kuwa ni baada ya mambo hayo, Mbowe alimwalika Rais kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la BAWACHA, na akaamua kumpa tuzo. Isije ikawa ilikuwa ni tuzo ya shukrani ya yale aliyotendewa yeye binafsi, na siyo chama au umma wa watanzania.
Naunga mkono hoja.Lakini kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, na kwaajili ya kuleta uwazi katika uongozi, na kuzuia fikra za pesa hiyo kuonekana kuwa ni hongo, Mbowe alistahili kuweka wazi juu ya malipo hayo yanayotajwa kuwa ni fidia.
Kwenye mfumo wa fedha, CHADEMA ipo hovyo sana. Hakuna hata shilingi inayofika mkoani au wilayani. Pesa yote inatumiwa na wakubwa wachache makao makuu.Cha ajabu wanasema chadema kipo sababu ya pesa za Mbowe pekee!! Unajiuluza mabilion yalikua yanaenda wapi mind you wabunge walikua wanachangishwa million 1 kila mwezi!!
Mambo ya aibu sana.
Kwa mujibu wa Lisu, hiyo tuzo aliitoa Mbowe bila ya ridhaa ya kamati kuu ya chadema.Ikumbukwe kuwa ni baada ya mambo hayo, Mbowe alimwalika Rais kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la BAWACHA, na akaamua kumpa tuzo.