Mbowe baada ya kupewa pesa iliyotajwa kuwa ni fidia, alitakiwa kuweka wazi ili isionekane kuwa ni hongo

IFIKE wakati Mbowe ajiondoe mwenyewe, atakayeiua chadema ni ung'ang'anizi wake. Wananuka rushwa na wenje wake Jamii yote inajua sijui atatuambia Nini?

Asifikiri hiki ni chama chake, ni chama Cha watanzania, Anachotafuta ni aibu haijalishi ameshinda au kushindwa
 
Huu ni uongo mwingine. Mbowe hajalipwa fidia ya kukaa ndani. Badala ya kumuomba mtuhumiwa atoe ushahidi, mlitakiwa nyinyi mnaomtuhumu ndio muweke ushahidi unaowafanya kuamini hivyo. Hii ni character assassination 101. Insinuate vitu vya uongo bila ushahidi ukijua hamna namna ya ku prove otherwise.

Mnapaswa kuona aibu.

Amandla...
 
Lakini kwa nafasi yake kama kiongozi wa chama kikuu cha upinzani, na kwaajili ya kuleta uwazi katika uongozi, na kuzuia fikra za pesa hiyo kuonekana kuwa ni hongo, Mbowe alistahili kuweka wazi juu ya malipo hayo yanayotajwa kuwa ni fidia.
Naunga mkono hoja.
 
Kuna comment mbali mbali toka Twitter/ X wengine wanasema mbowe alilamba asali nono kwenye maridhiano, wengine wanasema alipewa 4B, wengine wanasema alipewa 7B, wengine wanasema kapewa 12B. Wengine wanasema kapewa advance ya 3B halafu atapewa 7B baada ya Uchaguzi baada ya bitozo kushinda kwa kishindo pia chama chake kitapewa majimbo, viti maalum na uwaziri, na baadhi ya makada watateuliwa kwenye nafasi mbalimbali, kiufupi inaitwa "nusu mkate" ambayo Tundu Lissu aliizungumzia




Hizi ni tetesi toka Twitter, sina uhakika kama ni ukweli au uzushi.


Ila tuweke masihara pembeni 12B sio hela ya Kitoto 🤣🤣 hata wewe Bams sijui kama ungeiacha🤣


Unaweza kuta kapewa hela zaidi ya hiyo 12B inayosemwa 🤣

Muda utazungumza
 
Cha ajabu wanasema chadema kipo sababu ya pesa za Mbowe pekee!! Unajiuluza mabilion yalikua yanaenda wapi mind you wabunge walikua wanachangishwa million 1 kila mwezi!!

Mambo ya aibu sana.
Kwenye mfumo wa fedha, CHADEMA ipo hovyo sana. Hakuna hata shilingi inayofika mkoani au wilayani. Pesa yote inatumiwa na wakubwa wachache makao makuu.
 
Ikumbukwe kuwa ni baada ya mambo hayo, Mbowe alimwalika Rais kuwa mgeni rasmi kwenye tamasha la BAWACHA, na akaamua kumpa tuzo.
Kwa mujibu wa Lisu, hiyo tuzo aliitoa Mbowe bila ya ridhaa ya kamati kuu ya chadema.

Asante sana Lisu, tuko na wewe mpk saccos itakaposambaratika kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…