Mbowe: CHADEMA haijatengwa tusiuchafue msiba wa Mzee Mtei

upupu255

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2024
Posts
418
Reaction score
550
Mwenyekiti mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, ambaye pia ni mwanafamilia wa marehemu Mzee Edwin Mtei, amejibu hoja mbalimbali zilizoibuliwa mitandaoni zikidai kuwa CHADEMA haijapewa nafasi na hadhi inayostahili katika taratibu za kumuenzi muasisi wa chama hicho kabla ya mazishi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari, Mbowe amesema anasikitishwa na taarifa hizo akizitaja kuwa ni za uongo na zenye nia ya kuuchafua msiba huo, huku akisisitiza kuwa hakuna mtu wala kundi lililotengwa katika maandalizi ya mazishi ya marehemu Mzee Mtei.

Mbowe amesema familia inapenda kuona mwili wa marehemu ukipumzishwa kwa amani bila malumbano yoyote, akibainisha kuwa CHADEMA imepewa nafasi kubwa katika taratibu zote kuanzia zoezi la kuuchukua mwili Mochwari hadi shughuli za kumuaga na kumuenzi marehemu.

Ameongeza kuwa watu wengi waliopo msibani hapo ni wanachama na viongozi wa CHADEMA, jambo linalothibitisha kuwa chama hicho kimehusishwa kikamilifu katika kila hatua ya maandalizi ya msiba huo.

“Ninasikitishwa na baadhi ya watu wanaotaka kuuchafua msiba huu kwa kutoa taarifa za uongo. Hakuna aliyebaguliwa wala kutengwa. Kila mtu amepewa nafasi ya kumuenzi Mzee Mtei,” amesema Mbowe.

Mazishi ya Mzee Edwin Mtei yanatarajiwa kufanyika kesho, Jumamosi, katika makaburi ya nyumbani kwake Tengeru, jijini Arusha.

View attachment 3533305
Mbowe kujifanya mwanadiplomasia ndiyo kumechelewesha mageuzi ya demokrasia Tanzania. Kujifanya mstaarabu kwa wahuni ni dalili za woga au mtu aliyekuwa compromised.

Nina uhakika Edwin Mtei alikuwa anajivunia CHADEMA kama zao lake kama kazi nyingine yoyote aliyowahi kufanya huko nyuma. Katika msiba wake, CHADEMA haitakiwi kusukumwa pembeni au nyuma na yeye kama ana nia njema anatakiwa awe mstari wa mbele kuhakikisha hilo halitokei.
 
Anaogopa akisema ni msiba wa chadema yule mwenyekiti wa CCM atasusa.

Mbowe yupi compromised ndio maana anakosa misimamo
 
Huyo Mwenyekiti wa CCM kama kweli anamuheshimu Marehemu inatakiwa akubaliane na hali inayoandaliwa na wenyeji na atakayoikuta siyo kulazimisha kutengeneza mazingira ya yeye kuwa comfortable msibani. Siyo lazima kutamka au kutangaza ni msiba wa CHADEMA ila mazingira tu yanatakiwa yaseme kila kitu. Asiyetaka asije.

Hivi misiba mingapi inayohusu wafuasi wa CHADEMA imeingiliwa? Inasemekana hata msiba waliokuwa wameuandaa wa Lissu ulikuwa wa kuhakikisha shughuli inaenda kwa mwendokasi bila maombolezo ya maana na Mbowe anayajua yote haya.
 
Huu ni Msiba wa familia ya Mtei, Ambayo ipo n.a. inawajibika na Msiba wa Baba yao.

Ni kweli kwamba Freeman Mbowe ameoa mtoto wa Mzee Mtei, n.a. ni kweli Mwamba yuko kwenye Msiba n.a. anashiriki kama Mkwe na vilevile kama mwenyekiti mstaafu wa Chadema.

Hivyo basi tunapochangia humu kuhusu Msiba huu tuzingatie hilo

Nakala: Yericko Nyerere
 
Bila kujali kama kulikuwa na tuhuma hizo au hazikuwepo, wananchi wote tuwe pamoja katika kumpumzisha Marehemu Mtei, labda wale waliomfanya marehemu kuishi kwa simanzi kwa sababu ya kuwatendea uovu wa kila aina wanachama na wapenzi wa chama alichokianzisha.
CCM wasipohudhuria ni heri tu, maana hawawezi kujifanya wanampenda Mtei huku wakiendelea kuwatendea uovu wale wote wanaoonekana kuwa wafuasi wa chama alichokianzisha Mtei.
 
Mbowe kujifanya mwanadiplomasia ndiyo kumechelewesha mageuzi ya demokrasia Tanzania. Kujifanya mstaarabu kwa wahuni ni dalili za woga au mtu aliyekuwa compromised.

Nina uhakika Edwin Mtei alikuwa anajivunia CHADEMA kama zao lake kama kazi nyingine yoyote aliyowahi kufanya huko nyuma. Katika msiba wake, CHADEMA haitakiwi kusukumwa pembeni au nyuma na yeye kama ana nia njema anatakiwa awe mstari wa mbele kuhakikisha hilo halitokei.
Mbowe ni mlaghai hana diplomasia yoyote.
Mbowe ni aina ya wale watu wale ambao ni wachawi. Mbele ya macho ya watu huongea kwa upole, hujifanya wema, hujifanya na busara sana, lakini nyuma ya pazia ni nyoka.

Kuthibitisha nayosema kafatilie jinsi mambo aliyokua akifanya wakati wa chaguzi ndani ya chama. Alikua hataki heche awe mwenyekiti kanda ya Serengeti, akamfanyia hila sana
Akawa hataki pambalu awe mwenyekiti ka da ya Victoria, alikua anamtaka wenje. Kafanya uhuni na ujinga mwingi

Alikua hataki msigwa awe mwenyekiti nyasa, akamfanyia vituko vyote.

Mbowe ni mshenzi kama walivyo watawala
 
Mambo ya uchaguzi yameingiaje kwenye msiba wa Mtei?

Amandla...
 
Mbowe kujifanya mwanadiplomasia ndiyo kumechelewesha mageuzi ya demokrasia Tanzania. Kujifanya mstaarabu kwa wahuni ni dalili za woga au mtu aliyekuwa compromised.

Nina uhakika Edwin Mtei alikuwa anajivunia CHADEMA kama zao lake kama kazi nyingine yoyote aliyowahi kufanya huko nyuma. Katika msiba wake, CHADEMA haitakiwi kusukumwa pembeni au nyuma na yeye kama ana nia njema anatakiwa awe mstari wa mbele kuhakikisha hilo halitokei.
Chadema kwa kweli haitakiwi iwekwe pembeni kwenye msiba huu, ni chama kikubwa chenye heshima zake,na kwa mwasisi wake. Lakini kuna watu wa ovyo ovyo ,waropokaji,wasio na subra kama Heche,hao watengwe tu.
 
Back
Top Bottom