Mbowe: CHADEMA haipo kumbeba Rais Samia, atabebwa na chama chake

Mbowe: CHADEMA haipo kumbeba Rais Samia, atabebwa na chama chake

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
Dodoma/ Dar. Kufuatia kauli ya mbunge wa Makambako, Deo Sanga ya kuitaka Chadema kutosimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema watasimamisha wagombea ngazi zote kwa kuwa bado wanapambana na CCM.

Mbali na ombi la Chadema kutosimamisha mgombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Sanga pia alimwomba Mbowe na chama chake kutoa msamaha kwa wabunge 19 wa viti maalumu.

Sanga (CCM) alitoa ombi hilo kwa Chadema bungeni jijini Dodoma juzi wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kwa mwaka wa Fedha 2023/23, huku akisema Mbowe hawezi kukataa maombi yake.

Sanga ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe alitoa sababu za kutosimamisha mgombea kwenye nafasi hiyo ya juu akisema inatokana na namna ambavyo amekuwa akifanya Kazi nzuri na Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo ya maridhiano.

“Ombi langu kwa Mbowe, kwa sababu anataka kuwafanyia maendeleo Watanzania na mama ameshafanya kazi kubwa dunia inamwelewa, 2025 Mbowe tulia mwachie mama.

“2025 Mbowe shiriki na wabunge, shiriki na madiwani, nafasi ya urais mwachie mama,” alisema.
Kuhusu wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa Chadema, Sanga alisema.

"Mbowe alishasamehe, naomba asamehe zaidi na hawa wabunge 19 na mmoja wa wajimbo atangaze msamaha pia ili afungue ukurasa mpya, kwenye Urais amwachie mama aendelee bila kusimamisha mgombea."

Akizungumza jana kwa simu na Mwananchi, Mbowe alisema Chadema haipo kwa ajili ya kumbeba Rais Samia.

"Sipendi sana kucomment in person kuhusu Sanga, lakini Chadema haipo kwa ajili ya kumbeba Rais Samia, atabebwa na chama chake (CCM).

Tutapambama na Chadema kitakuwa na wagombea wa urais wazuri sina wasiwasi na hilo.
"Useme tumwachia Rais Samia….kwamba kuruhusu mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba lakini iliporwa kwa miaka saba yaani tumsifu kwa sababu hiyo?”

Mbowe alisema suala la kufutwa kwa kesi iliyokuwa ikimkabili haikuwa fadhila, bali ni wajibu.

"Mama Samia kuruhusu mikutano ya hadhara na kukubaliana na mchakato wa Katiba, huu ni wajibu wake amechelewa kuufanya hatuwezi kumpongeza kwa hilo.Sheria ya mitandao na vyombo vya habari bado changamoto kwa hiyo nchi haiendeshwi kwa hisani ya Rais kwa taasisi na mifumo imara

"Sasa viongozi kama kina Sanga ndio wapambe au tunawaita chawa, kama Rais Samia ni kiongozi imara tutamjaribu katika utumishi wake," alisema Mbowe

Via Mwananchi.

=====

Pia soma:
Deo Sanga: Mbowe 2025 shiriki na madiwani na wabunge, urais muachie Samia
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema chama chake kitasimamisha wagombea katika ngazi zote kuanzia Uchaguzi wa Serikal za Mitaa 2024 hadi Uchaguzi mkuu wa 2025 kwa sababu bado kinapambana na CCM.

Mbowe ametoa ufafanuzi huo kufuatia ombi la mbunge wa Makambako ambaye pia ni Mjumbe wa Vikao Vya Juu Vya CCM aliyeitaka Chadema isisimamishe mgombea Urais 2025 bali wajikite kwenye Udiwani na Ubunge.

Source: Mwananchi
 
Mwambie Mbowe kama uko naye jirani amwambie Samia wezi wa CAG watakamatwa lini?
 
Mbowe-chadema.jpg

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Freeman Mbowe ametoa kauli hiyo ikiwa ni majibu kwa Mbunge wa Makambako, Deo Sanga aliyemtaka Mbowe kutosimamisha Mgombea wa Urais katika Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Mbowe amesema "CHADEMA tutapambana na tutakuwa na Wagombea wa Urais wazuri, Rais Samia kuruhusu Mikutano ya Hadhara ni wajibu wake na amechelewa, hatuwezi kumpongeza kwa hilo.

Akizungumza na Mwananchi, Mbunge huyo wa zamani wa Jimbo la Hai, amesema suala la yeye kufutiwa kesi ya Ugaidi iliyokuwa ikimkabili haikuwa fadhila ya Rais bali wajibu.

=============

Kufuatia kauli ya mbunge wa Makambako, Deo Sanga ya kuitaka Chadema kutosimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema watasimamisha wagombea ngazi zote kwa kuwa bado wanapambana na CCM.

Mbali na ombi la Chadema kutosimamisha mgombea urais kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2025, Sanga pia alimwomba Mbowe na chama chake kutoa msamaha kwa wabunge 19 wa viti maalumu.

Sanga (CCM) alitoa ombi hilo kwa Chadema bungeni jijini Dodoma juzi wakati akichangia hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi kwa mwaka wa Fedha 2023/23, huku akisema Mbowe hawezi kukataa maombi yake.

Sanga ambaye ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe alitoa sababu za kutosimamisha mgombea kwenye nafasi hiyo ya juu akisema inatokana na namna ambavyo amekuwa akifanya Kazi nzuri na Rais Samia Suluhu Hassan katika mambo ya maridhiano.

“Ombi langu kwa Mbowe, kwa sababu anataka kuwafanyia maendeleo Watanzania na mama ameshafanya kazi kubwa dunia inamwelewa, 2025 Mbowe tulia mwachie mama.

“2025 Mbowe shiriki na wabunge, shiriki na madiwani, nafasi ya urais mwachie mama,” alisema.

Kuhusu wabunge 19 wa viti maalumu waliofukuzwa Chadema, Sanga alisema, "Mbowe alishasamehe, naomba asamehe zaidi na hawa wabunge 19 na mmoja wa wajimbo atangaze msamaha pia ili afungue ukurasa mpya, kwenye Urais amwachie mama aendelee bila kusimamisha mgombea."

Akizungumza jana kwa simu na Mwananchi, Mbowe alisema Chadema haipo kwa ajili ya kumbeba Rais Samia.

"Sipendi sana kucomment in person kuhusu Sanga, lakini Chadema haipo kwa ajili ya kumbeba Rais Samia, atabebwa na chama chake (CCM). Tutapambama na Chadema kitakuwa na wagombea wa urais wazuri sina wasiwasi na hilo.

"Useme tumwachia Rais Samia….kwamba kuruhusu mikutano ya hadhara ambayo ipo kikatiba lakini iliporwa kwa miaka saba yaani tumsifu kwa sababu hiyo?”

Mbowe alisema suala la kufutwa kwa kesi iliyokuwa ikimkabili haikuwa fadhila, bali ni wajibu.

"Mama Samia kuruhusu mikutano ya hadhara na kukubaliana na mchakato wa Katiba, huu ni wajibu wake amechelewa kuufanya hatuwezi kumpongeza kwa hilo.Sheria ya mitandao na vyombo vya habari bado changamoto kwa hiyo nchi haiendeshwi kwa hisani ya Rais kwa taasisi na mifumo imara

"Sasa viongozi kama kina Sanga ndio wapambe au tunawaita chawa, kama Rais Samia ni kiongozi imara tutamjaribu katika utumishi wake," alisema Mbowe.

MWANANCHI
 
Tunamshauri Deo Sanga pia jimbo la Makambako akae pembeni ampishe mgombea wa CHADEMA.
 
Buyu lake la asali limepungua huyo!

Samia amuongezee tafadhali
 
Mwenyekiti wa Chadema mh Freeman Mbowe amesema chama chake kitasimamisha wagombea katika ngazi zote kuanzia Uchaguzi wa Serikal za Mitaa 2024 hadi Uchaguzi mkuu wa 2025 kwa sababu bado kinapambana na CCM.

Mbowe ametoa ufafanuzi huo kufuatia ombi la mbunge wa Makambako ambaye pia ni Mjumbe wa Vikao Vya Juu Vya CCM aliyeitaka Chadema isisimamishe mgombea Urais 2025 bali wajikite kwenye Udiwani na Ubunge.

Source: Mwananchi
ASIMAMISHE tu tumewachoka wabunge wa ndiyo ipite nao wakapite huko mitaani.waliishatunyanyasa sana wafanyakazi nao wameteswa sana na mambo mengi kubwa zaidi ni kikokotoo kinawamaliza.hao wabunge wa ndio nao waje kitaa wakutane na kikokotoo cha mtaani.
 
Nilimsikia yule Ndondocha akimpigia magoti Mwamba pale Bungeni.

Ati Mwamba asigombania Urais wa Jamhuri.
 
Dodoma/ Dar. Kufuatia kauli ya mbunge wa Makambako, Deo Sanga ya kuitaka Chadema kutosimamisha mgombea urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe amesema watasimamisha wagombea ngazi zote kwa kuwa bado wanapambana na CCM.
Naunga mkono hoja, Chadema isimamishe mgombea urais kushindana na mgombea wa CCM ila nimewashauri kama CCM itasimamisha mgombea Mwanamke, Chadema nayo isimamishe Mwanamke Iwapo Watanzania wataamua 2025 twende na Mwanamke, mnaonaje tukiwashauri CHADEMA wasimamishe Mwanamke? Maana Mwanaume kushindwa na Mwanamke ni aibu!

Ila ikitokea Mwanamke huyo mgombea wa CCM ni Samia, then nimewashauri Kama Upinzani unataka mafaniko ya kweli iachane na 2025 lengo liwe 2030
P
 
Back
Top Bottom