Deo Meck Mbagi
JF-Expert Member
- Apr 19, 2015
- 360
- 525
MBOWE HATAFUTI URAIS, BALI ANATAFUTA NJIA YA KUPIGA PESA
- Ni mjasiriasiasa mbobezi, Kwake muhimu ni pesa na sio huduma kwa wananchi
- Anafahamu katika dunia ya leo hakuna mtu anaweza chagua Rais aliyepata sifuri darasani na kuacha Rais mwenye PHD
- Anajua akigombea yeye atakusanya pesa kwa wahisani wao kama mgombea urais na kuzisweka mfukoni kama ilivyo ada yake
- Tayari Lema kaanza kumshugulikia Lissu maana ndio tishio la Mbowe kwenye kupeperusha bendera ya Chadema
Pazia la kutangaza nia kwa mgombea urais kupitia chadema limefungwa juzi ambako wanachama watano wa Chadema wamejitokeza, wanaume wanne na mwanamama mmoja.
Ambapo Mwenyekiti wa chadema ambaye tayari jimbo lilimshinda na wananchi wa jimbo hilo kumzomea na kusababisha mkutano wake kukatishwa pia amejitokeza na kujitangaza kama mgombea.
Mtu ambaye Jimbo dogo la Hai limemshinda, mtu ambaye pesa za michango ya wabunge kashindwa kuzilinda na kaishia kuzifisadi hakika hana uwezo wa kuongoza Taifa letu.
Ila tunaomjua Mbowe tunafahamu kuwa yeye aliacha ujasiriamali na akaamua kuwa mjasiriasiasa, Kwake yeye siasa ni mradi wa njia ya mkato katika kupata utajiri na wazazi wenza kwa kuwaahidi ubunge wa Viti Maalum kama ilivyothibitika juzi katika IGIZO ambalo director wa IGIZO alikosea script.
Kutangaza nia kwa Mbowe ni kama alivyofanya 2005 kwani baada ya uchaguzi huo ndio aliweza kujenga nyumba anayoishi Mikocheni kwani pesa aliyoomba kwa wafadhiri mbalimbali kwa ajili ya kampeni alitumia kidogo na nyingi akatunza kwa ajili yake.
Mbowe anafahamu hana uwezo wa kushinda Jimbo, hivyo malengo yake ni kuwa mgombea urais huku akijua hana uwezo wa kushinda bali atatumia jukwaa hilo kukusanya michango na kuendelea kujinufaisha kupitia siasa kama ilivyo ada yake siku zote.
Ni dhahiri Mbowe hana uwezo wa kuwa Rais, hat ukiangalia kitaaluma ni mtu asiye na taaluma zaidi ya ujanja ujanja wa kuunga hapa na pale. Dunia ya leo hauwezi chagua Rais ambaye ni form four failure na ukaacha Rais mwenye PHD na mwenye uwezo mkubwa kama Rais Dr. John Magufuli.
Hilo Mbowe analijua vyema na anafahamu kwamba hakuna mtanzania mzembe anayeweza kufikiri mtu kama yeye anaweza kuwa Rais, mtu ambaye ni mlevi wa kupindukia ambaye anapata majanga katika ulevi na kutaka kutengeneza taharuki kwenye jamii kuwa alivamiwa na watu watatu, kumbe watu hao ni ndugu ambao ni: John Walker, Konyagi na K Vant.
Jana sote tumesikia maneno ya Mbunge aliyemaliza muda wake na ambaye wananchi walishamchoka, Godbless Lema wa Arusha Mjini. Amesikika akimponda Lissu kuwa tayari anajiona mgombea urais wakati bado. Lema kama mndani wa siri wa Mbowe anajua walichopanga, hivyo Lissu asahau kabisa suala la kuwa mgombea wa chadema kwani wenye chama chao wanataka kupiga pesa za kustaafia maana wanajua chama kimeshapoteza mvuto kwa watanzania na tunachoenda kufanya ni kukizika hapo October 25, 2020.
Hivyo Lissu ahesabu maumivu tu maana wenye chama chao, wamiliki wana jambo lao na ni kutumia jukwaa la uchaguzi kukusanya mabilioni. Wala dhamira sio kushinda kwani wanafahamu mgombea wao hauziki hata bure, na hata movie ya kujitafutia umaaruru pia ilibuma, ni kama nyani akikaribia kufa basi miti yote huteleza.
Tukutane kwa debe hapo October 25, 2020.
For God and My Country.
Deo Meck
Kada mtiifu wa CCM.