Mbowe: Hatutashiriki (CHADEMA) tena Uchaguzi wowote! Bado mifumo na Wasimamizi ni walewale

Hahahhaa.... Si wamesema matatizo yote kaondoka nayo Magufuli na sasa wako huru? Wanaogopa nini sasa?

Kwani hawa wanaoshangilia humu siyo bavicha?
ungekuwa profitable wewe kenge usingekua unambwata huko lumumba
 
Better late than never but never late is better!

Nakubaliana na Mbowe.

Hakuna kushiriki chaguzi za kipuuzi mpaka kieleweke.
Kisipoeleweka mtafanyaje? Kwani sasa hivi kinaeleweka? Si mfanye sasa hivi hicho mnachofikiri mtakifanya ili cha moto mkipate.

Wimbo wa tume huru na katiba mpya mlishaambiwa msahau kwani hamjui hata mnachokitaka kwenye hiyo tume huru na katiba mpya kama si kuleta vurugu tu kwenye nchi.

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar iliwakubalia kuunda hiyo mnayoiita tume huru. Kiuhalisia tume hiyo ni tume ya vyama vya siasa. Kati ya wajumbe 10 wa tume hiyo 6 wakatoka chama tawala akiwemo mwenyekiti wa tume na wajumbe 4 wakatoka chama kikuu cha upinzani, CUF wakati huo. Kilichotokea kwenye uchaguzi mkuu uliofuata wa mwaka 2015 hakijawahi kutokea pengine hapa duniani!. Wajumbe wa tume walitwangana makonde, furniture na makaratasi ya ofisi zilivunjwa vunjwa. Hatima mwenyekiti wa tume akatangaza kuufuta uchaguzi mkuu huo.

Kwenye jaribio la kutengeneza katiba mpya kila mtu anakumbuka kilichotokea kwenye bunge la katiba kuanzia tu kwenye kutunga kanuni za kuendesha bunge hilo. Makaburi yalifukuliwa, waasisi wa taifa hili walitukanwa matusi mazito mazito hadi ya nguoni. Baada ya kunge hilo kutafuna matrillioni ya fedha wapinzani walilikimbia bunge na kuahidi kuzunguka nchi nzima kuwashawishi wananchi wasiipigie kura ya ndiyo hiyo katiba mpya iliyopendekezwa.

Sasa ni mjinga gani atawaelewa nyinyi wapinzani mnaoililia tena hiyo katiba mpya mliyoikataa. Si mseme tu wazi vitu gani mhimu sana mnavyovitaka kwenye hiyo katiba mpya. Kama ni mambo ya serikali tatu hayo sahauni. Kama ni ya wagombea binafsi na rais mteule kupingwa mahakamani: ni kiasi tu cha kupeleka msuada bungeni na ukipita kwa idadi ya wabunge inayotakiwa kikatiba jambo hilo linakuwa ruksa. Vile vile hata hilo la tume huru yenu ya uchaguzi ni kiasi tu cha kujenga hoja nzito ya composition ya hiyo National Electoral Commission mnavyotaka iwe na kupeleka mswaada bungeni ukajadiliwa na kama una mantiki utapitishwa aidha bila mabadiliko au kwa mabadiliko kiasi. Vivo hivyo hayo madaraka ya rais mnayotaka apunguziwe nk.

Mambo ya kukimbilia kufumua katiba yote na kuunda mpya hasa kwa mashinikizo ya kisiasa ni ya hatari sana. Hata nchi za ulaya, amerika, china nk hakujawahi kufanyika kitu kama hicho. Katiba zao ni zile zile ila huwa zinafanyiwa marekebesho madogo au makubwa pale inapohitajika. Katiba ni dynamic. Katiba ni mwongozo wa sheria za nchi. Katiba inaongoza utungaji wa sheria zetu. Unapofuta katiba ya zamani na kutunga katiba mpya ili katiba hiyo mpya iweze kutekelezwa inabidi sheria zote za nchi zitungwe upya kutekeleza katiba mpya. Tusitake mambo ya kuigaiga. Kenya wametunga katiba mpya kinachotokea huko baada ya katiba mpya sote tunakishuhudia - ni vurugu mechi.
 
Washawishi na vyama vingine vyenye nguvu/wafuasi wengi kuwa na msimamo kama wa kwao...
 
Chadema washiriki au wasishiriki uchaguzi bado wataendelea kubaki juu daima
 
Chadema imeishakufa Ila hawataki kusema tu.
 
Hahahhaa.... Si wamesema matatizo yote kaondoka nayo Magufuli na sasa wako huru? Wanaogopa nini sasa?

Kwani hawa wanaoshangilia humu siyo bavicha?
Wanaoshangilia humu NI CCM ASILIA ,WANAONUNA HUMU NI SUKUMA GANG AU MATAGA AU CCM MPYA
 
Aànze Augustino Mrema kwanza kupisha damu mpya
 
SIMUSEME TUUU MNAOGOPA KUGARAGAZWA ASUBUHII?? ACHENI SISI TUNAENDELEA KUWAPAMBANIA WATANZANIA
 
Hivi ndio vipaumbele.
1. Tume huru ya uchaguzi
2. Katiba mpya

Tuache kufanya mambo ya msingi ya maisha ya watu tuhangaike na tume huru au katiba mpya kisa tu chadema wapate madaraka? Kwani kama wao hawapo nn kinasimama?
 
Tulisema hivi.
Zitto ameshaanza kuaminisha uchaguzi ulikuwa huru na haki!
Mtazamo wangu kitakachofuatia:
1) Vyamba vingine vya upinzani kushiriki (sio Chadema kwa sasa) chaguzi ndogo zijazo!
2) Kuimba uchaguzi ulikuwa huru na haki.
3) Upinzani kushinda baadhi ya chaguzi!
4) Baadhi ya vyama vya upinzani vitavyo shiriki chaguzi ndogo kumwaga baadhi kwa staili ya kule twitter!
5) Baadhi ya wana Chadema kuanza ku question kususia uchaguzi!

Mimi naunga mkono kususia uchaguzi kwa ajili ya tume huru na katiba mpya. Lakini kama wapinzania wengine wangeshiriki pia. I hope Chadema wana plan la sivyo hii ndio itakwenda kuwa kaburi Lao!
 
Waulizwe ACT Wazalendo walichofanywa jana
 
Du! Hata wewe
Huu msimamo wa Chadema wa kususia uchaguzi kwa ajili ya tume huru na katiba mpya ni mzuri Lakini kama asilimia kubwa ya vyama vya upinzani wangekuwa na msimamo sawa!! Ubinafsi ndio itakayo kwamisha tume huru na katiba mpya!
Zitto kashasema uchaguzi ulikuwa huru na haki. Kitakachofuatia lazima ACT ishinde baadhi ya chaguzi ili kuipa madai yake nguvu!
Mark my words...ACT watashinda baadhi ya chaguzi!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…