Mbowe: Hatutashiriki (CHADEMA) tena Uchaguzi wowote! Bado mifumo na Wasimamizi ni walewale

Mbowe: Hatutashiriki (CHADEMA) tena Uchaguzi wowote! Bado mifumo na Wasimamizi ni walewale

Nimemsikia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakati akihutubia Wananchi amerudia msimamo wa CHADEMA kutoshiriki chaguzi.

Amesema “Hatutashiriki Uchaguzi wowote, bado mifumo ya Uchaguzi ni ileile, Wasimamizi ni walewale, hapana, hatuna haraka ya kwenda kwenye Uchaguzi wowote mdogo wa Udiwani, Wabunge hata Mwenyekiti wa Mtaa hadi tupate mwafaka wa Kitaifa, na nafasi ya Chaguzi za Kidemokrasia”

Aidha, amewataka viongozi wastaafu na walioko madarakani wa CCM na wa Serikali, kuwaomba radhi Watanzania kutokana na dosari zilizojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020, ili kuleta utengamano wa Taifa.
=====

MY TAKE
Kama ACT, NCCR na vyama vingine vya upinzani vikiendelea kushiriki na kusaidiwa kushinda. Na hatimaye kuwa na wabunge wao wakuchaguliwa bungeni.

Hii haitachangia kuidhoofisha na kuisambaratisha Chadema?

Kutoshiriki uchaguzi ni mzuri kama vyama vyote vya upinzani vitakubaliana.

Hana ela na hana wagombea ndio shida wala sio mambo ya wasimazi

So yy alitaka msimamizi awe sugu au
 
Tuache kufanya mambo ya msingi ya maisha ya watu tuhangaike na tume huru au katiba mpya kisa tu chadema wapate madaraka? Kwani kama wao hawapo nn kinasimama?
Uwezo wako wa kufikiria ni 1kb acha wenye akili za 10GB wakusaidie. Hakuna chochote unachojua.
 
Uwezo wako wa kufikiria ni 1kb acha wenye akili za 10GB wakusaidie. Hakuna chochote unachojua.

Ww ndio ujui kitu
Katiba mpya inakusaidia ww au wanasiasa?

Wanasiasa wanataka katiba mpya kwa manufaa yao, ww unalialia katiba mpya ndio itakupa kazi ya kufanya ?
 
"Tusahau Katiba mpya kwa sasa "
Samia


Hata hiyo tume hawezi kuivuruga kama anampango wa kugombea 2025
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeundwa kisheria kwa mujibu wa Ibara ya 74 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977 na pia Wasimamizi wa Uchaguzi na wasaidizi wao wako kisheria kwa mujimu wa Sheria ya Taifa ya Uchaguzi Sura ya Kifungu cha 7 (1-5)na Sheia ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa sura ya 292 Kifungu cha 9 (1-6) ambazo wabunge akiwaemo Mbowe alipokuwa Mbunge alizipitisha na sasa anazikana mwenyewe. Aiache Tume ifanye kazi yake ya Uchaguzi kwa kufuata sheria kwani wakisusa Uchaguzi Vyama vya Siasa vingine vinashiriki Uchaguzi Huru na wa Haki
 
Better late than never but never late is better!

Nakubaliana na Mbowe.

Hakuna kushiriki chaguzi za kipuuzi mpaka kieleweke.
gomeni ivo ivo na ikiwezekana achaneni kabisa na siasa za tanzania
 
Nimemsikia Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe wakati akihutubia Wananchi amerudia msimamo wa CHADEMA kutoshiriki chaguzi.

Amesema “Hatutashiriki Uchaguzi wowote, bado mifumo ya Uchaguzi ni ileile, Wasimamizi ni walewale, hapana, hatuna haraka ya kwenda kwenye Uchaguzi wowote mdogo wa Udiwani, Wabunge hata Mwenyekiti wa Mtaa hadi tupate mwafaka wa Kitaifa, na nafasi ya Chaguzi za Kidemokrasia”

Aidha, amewataka viongozi wastaafu na walioko madarakani wa CCM na wa Serikali, kuwaomba radhi Watanzania kutokana na dosari zilizojitokeza kwenye Uchaguzi Mkuu wa 2020, ili kuleta utengamano wa Taifa.
=====

MY TAKE
Kama ACT, NCCR na vyama vingine vya upinzani vikiendelea kushiriki na kusaidiwa kushinda. Na hatimaye kuwa na wabunge wao wakuchaguliwa bungeni.

Hii haitachangia kuidhoofisha na kuisambaratisha Chadema?

Kutoshiriki uchaguzi ni mzuri kama vyama vyote vya upinzani vitakubaliana.
Ushirikiano ni mzuri lakini kila chama ni taasisi in its own right, hakuna chama kilichodhaminiwa na kingine kupata usajili; wanaotaka kushiriki washiriki ndio maana ya demokrasia ya vyama vingi, lakini watu wenye akili na maono mapana tutasubiri uwanja uwekwe sawia tucheze kwa haki!

Sent from my itel A32F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom