Mbowe: Hayati Rais Magufuli alikuwa na kipaji cha uthubutu wa hali ya juu, hakuwa mvivu hata kidogo

Mbowe: Hayati Rais Magufuli alikuwa na kipaji cha uthubutu wa hali ya juu, hakuwa mvivu hata kidogo

Elitwege

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
5,294
Reaction score
10,970
Kuna video inazunguka mitandaoni ikimuonyesha mwenyekiti wa Chadema Freeman Mbowe akikiri kuwa hayati rais Magufuli alikuwa na kipaji cha uthubutu wa hali ya juu na alifanya maamuzi magumu kwelikweli ambayo kwa kiongozi wa kawaida asingeweza.

Mbowe amesema Magufuli hakuwa mvivu hata kidogo na alichapa kazi kwelikweli usiku na mchana na kuwataka Chadema kama wanataka kufanikiwa lazima waige tabia hiyo.

Kuanzia 11: 07



My take:
Mbowe ameamua kuwavua nguo makamanda? Ama kweli unafiki haulipi hata mwaka haujaisha nafsi zimeanza kuwasuta na kuanza kusema ukweli kuwa upingaji wao kwa Magufuli kumbe ulikuwa unafiki tu.
 
Mbona umeikata kabla ya kumalizika. Palikuwa na "lakini" pale.

Nisiache kukukumbusha, bila kusikiliza lakini iliyokuwa ikufuatia, utakuwa umemnukuu Mbowe out of context.
 
Mbowe : Hayati rais Magufuli alikuwa na kipaji cha uthubutu wa hali juu, hakuwa mvivu hata kidogo..

Siyo tu kwamba ^alikuwa na kipaji cha uthubutu wa hali ya juu.^ JPM alikuwa kiongozi na mtawala mwenye sifa kamili ya kutekeleza mambo adimu, adhimu, azali na azizi yaliyowashinda watu na viongozi wengi --

Ama kwa sababu ya woga wao au kutokana na kukosa njozi iliyofungamana na msukumo thabiti wa uzalendo usiotiliwa mashaka wala kuyumbishwa vyovyote vile.
 
Back
Top Bottom