Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 78,790
- 128,275
Mbowe anafanya logical non sequitur fallacy.Mbowe anaona vijana wake anao walea na kuwaleta mjini wana dharau. Lakini anasahau inawezekana kabisa wana nia njema ya kuiokoa Chadema na Tanzania. Kwa Watanzania wengi wnakubaliana na Lissu na wengine kwamba ni lazima mabadiliko yafanyike kwa manufaa ya umma.
Nimeona Leo Mbowe akimkaripia mwandishi kwamba yeye anajua ana Hotel nje yenye thamani ya mamilioni ya dollar huko uwingereza sasa anamuulizaje maswali kwamba yeye kalamba asali. Lissu hajawahi kuhoji Mbowe kuwa na uwezo yeye nia yake kubwa ni kuokoa taifa na kuamini tunahijahi kuamsha watu kupambana na katiba. Mbowe anatakiwa kujitoa kwenye dhana kwamba mawazo tofauti ya mwenendo wa chama ni dharau kama sio hivyo kwanini uongelee mambo ya kutoa nyumba kwa Lissu?
Wakati cha msingi ni mwenendo wa nchi kwa ujumla. Heche na Lissu wanaogopea nchi na hawana nia yeyote ya dharau kwa Mbowe lakini Mbowe kwa kukataa kukaa pembeni hawana namna zaidi ya kushindana naye kwa manufaa ya nchi
Sisemi Mbowe kalamba asali au hajalamba.
Ila, hoja ya kusema Mbowe ni tajiri hivyo hawezi kulamba asali haina mashiko.
Watu wanasema kutoa ni moyo, usambe utajiri. Kinyume chake pia, kupenda pesa ni moyo, usambe umasikini.
Kuna watu masikini na hawapendi rushwa.
Kuna watu masikini wanapenda rushwa.
Kuna watu matajiri hawapendi rushwa.
Kuna watu matajiri wanapenda rushwa.
Kwani ukiwa tajiri ndiyo huwezi kulamba asali?
Hoja ya kusema Mbowe tajiri hivyo hawezi kulamba asali haina mashiko.
Unavyozidi kupata hela ndiyo matumizi yako yanazidi.
Elon Musk kawa tajiri namba moja hapa duniani, kaona dunia haimtoshi anatafuta hela za kuhamisha watu kuwapeleka Mars.
Sasa kama Elon Musk, tajiri namba moja duniani, bado anatafuta hela, Mbowe ana utajiri gani wa kusema hawezi kupenda hela zaidi kwa sababu yeye tajiri?
That is a poor argument.
And it shows why Mbowe cannot lead, he is not sharp, he does not have logical argument.
This is a logical fallacies, several fallacies actually.
There is a non sequitur, as well as argument from authority.